Figo zetu zinafanya kazi kubwa sana kwa ajili ya afya yetu. Huchuja damu yetu, hutengeneza homoni, kunyonya madini, hutoa mkojo, huondoa sumu, na kupunguza asidi. Kwa hiyo, kama moja ya viungo muhimu zaidi katika mwili wako, figo zako zinastahili kutunzwa sana na kuzipenda ipasavyo.
Uharibifu au kupungua kwa uwezo wa figo zako mara nyingi kunaweza kutotambuliwa kwa muda wa miaka mingi kwani figo zako bado zinaweza kufanya kazi yake kwa uwezo kidogo wa 20%. Kwa hivyo magonjwa ya figo mara nyingi huitwa “Magonjwa ya Kimya kimya”. Ndiyo maana ni muhimu sana kuzijali na kuzitunza kabla ya kuchelewa.
Hapa kuna orodha ya tabia 10 za kawaida ambazo huweka shinikizo nyingi kwenye figo zako na zinaweza kusababisha uharibifu mkubwa kwa muda.
- Kutokunywa Maji Mengi Ya Kutosha
Kazi muhimu zaidi ya figo zako ni kuchuja damu na kuondoa sumu na taka taka mwilini. Usipokunywa maji ya kutosha wakati wa mchana sumu na takataka huanza kulundikana na zinaweza kusababisha madhara makubwa mwilini mwako.
- Kuchelewesha Kutimiza Wito wa Asili mara kwa mara
Tunapohisi kukojoa, wengi wetu hupuuza kwenda kukojoa kwa sababu tunakuwa na shughuli nyingi au tunajizuia kuingia kwenye mabafu au vyoo vinavyoingiwa na watu wengi. Kuzuia mkojo mara kwa mara huongeza shinikizo la mkojo na kunaweza kusababisha figo zako kushindwa kufanya kazi, au kuwa na mawe kwenye figo, nk. Kwa hiyo sikiliza mwili wako wakati viungo vyako vya mwili vinapohitajika kufanya jambo fulani.
- Utumiaji Wa Sukari Nyingi Sana
Utafiti wa kisayansi unaonyesha kuwa watu wanaotumia vinywaji 2 au zaidi vya sukari kwa siku wana uwezo mkubwa wa kuwa na protini kwenye mkojo wao.
Kuwa na protini kwenye mkojo wako ni ishara ya mapema kwamba figo zako hazifanyi kazi zake kama ipasavyo.
- Chumvi Nyingi Kwenye Chakula
Mwili wako unahitaji sodiamu au chumvi ili kufanya kazi vizuri. Watu wengi hata hivyo hutumia chumvi nyingi ambayo inaweza kuongeza shinikizo la damu na kuweka msongo mkubwa kwenye figo. Kama kanuni nzuri ya kidole gumba, si zaidi ya gramu 5 za chumvi zinapaswa kuliwa kila siku.
- Upungufu Wa Madini Na Vitamini
Ulaji wa lishe nzuri iliyo kamili yenye mboga za majani na matunda, kwa ujumla ni muhimu kwa afya yako kwani huzifanya figo zako kufanya kazi vizuri. Mapungufu mengi ya madini au vitamini yanaweza kuongeza hatari ya mawe kwenye figo au figo kushindwa kufanya kazi. Vitamini B6 na madini ya magnesiamu, kwa mfano, ni muhimu sana kwa ajili ya kupunguza hatari ya mawe kwenye figo.
- Protini Ya Wanyama
Ulaji wa protini, hasa nyama nyekundu huongeza mzigo wa kimetaboliki kwenye figo zako.
Kwa hivyo protini nyingi katika lishe yako inamaanisha kuwa figo zako zinapaswa kufanya kazi kwa bidii na hii inaweza kusababisha uharibifu wa figo au kutofanya kazi zake kwa wakati.
- Kukosa Usingizi
Wote tunajua umuhimu wa kupumuzika vizuri usiku. Tatizo sugu la kukosa usingizi linahusishwa na magonjwa mengi yakiwamo na magonjwa ya figo. Wakati wa usiku mwili wako hurekebisha tishu za figo zilizoharibika, kwa hiyo upe mwili wako muda wa kutosha wa kujiponya na kujirekebisha.
- Matumizi Ya Madawa Ya Kupunguza Maumivu
Watu wengi sana hutumia dawa za kutuliza maumivu kwa ajili ya magonjwa yao na maumivu yao madogo madogo, wakati kuna tiba nyingi za asili na salama zinazopatikana. Unapotumia kwa muda mrefu madawa ya kutuliza maumivu unaweza kusababisha uharibifu mkubwa wa ini na figo. Ukipatwa na tatizo la figo au ini, basi tafakari sana ujue nini ulianza kutumia hapo awali.
- Matumizi Ya Pombe
Pombe ni sumu kali ambayo inaweka mkazo mwingi kwenye figo na ini.
- Tabia Ya Unywaji Wa Kahawa
Kama vile chumvi, kafeini inaweza kuongeza shinikizo la damu na kuweka mkazo zaidi kwenye figo zako. Unapotumia kahawa kwa muda mrefu au kwa kupita kiasi, unaweza kusababisha uharibifu kwenye figo zako.
Ili kuwa na afya njema na kuepuka matatizo ya figo ni muhimu kula vyakula vingi vibichi, visivyokobolewa na ikiwa utaweka akilini mwako maelezo hayo juu na kuepuka kwa makini tabia hizi, figo zako hazitakuwa na mkazo wa mara kwa mara na mwili wako utakushukuru kwa hilo.
Ninakushukuru kwa kusoma nakala hii. Nakusihi usisome tu kama karatasi au gazeti la michezo ili kujua taarifa ya michezo, bali soma kwa ajili ya afya yako njema. Tukutane sote kwa afya njema.
Pia unaweza kutuma namba yako ya WHATSAP ili tuweze kukuunganisha na darasa letu la masomo ya afya.
Je, Unahitaji huduma? Pia wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626,
Arusha-Mbauda,
Karibu sana!