Na ieleweke kuwa, moyo ni msuli ambao husukuma damu na kuifanya isafiri mwili mzima.
Damu inayokuwa na kiwango kidogo cha oksijeni husukumwa kuelekea kwenye mapafu, ambapo hewa ya oksijeni hujazwa tena. Hivyo basi, hewa ya oksijeni inapoingia kwenye damu husukumwa tena na moyo na kusafirishwa kila mahali mwilini mwako. Ile hali ya moyo kusukuma damu hujenga msukumo kama shinikizo fulani.
NUKUU: Ikiwa kama mtu ana ugonjwa wa shinikizo la juu la damu, inamaanisha kwamba kuta za mishipa yake ya ateri tayari zimeshakuwa ngumu na hivyo hazina uwezo wa kutanuka na kuruhusu damu isafiri kwa kiwango chake kinachotakiwa.
Je, Nini Husababisha Ugonjwa Wa Shinikizo La Juu La Damu?
Kwa kawaida visababishi vya ugonjwa wa shinikizo la juu la damu huwa ni vingi, navyo ni kama ifuatavyo:
- Ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi, vilivyokobolewa au kusindikwa,
- Matumizi ya vyakula vyenye chumvi nyingi sana
- Unene wa kupindukia
- Kuwa na kitambi
- Kutokufanya mazoezi
- Unywaji pombe
- Uvutaji sigara
- Msongo wa mawazo
- Umri mkubwa
- Magonjwa ya figo
- Kisukari
- Madhara katika tezi ya thyroid na adrenal
Je, Dalili Zake Zinakuwaje?
Ugonjwa wa shinikizo la juu la damu kwa kawaida huwa ni hali ya ukimyakimya. Watu wengi hushindwa kutambua dalili zozote. Inaweza ikagharimu miaka mingi sana ili kuja kuweza kuzitambua dalili zake. Hata hivyo, dalili hizi zinaweza kuonekana kupitia magonjwa mengine. Lakini inapofikia hali ya ugonjwa kuongezeka na kuwa shinikizo la juu la damu, basi dalili zake huwa kama ifuatavyo:
- Kichwa kugonga
- Kushindwa kupumua vizuri
- Kutokwa na damu puani
- Kizunguzungu
- Kifua kuuma
- Maluweluwe ya macho
- Damu kwenye mkojo
Je, Ni Watu Gani Wanaokabiriwa Na Tatizo Hili La Shinikizo La Juu La Damu?
- Kina mama wajawazito
- Wanawake wanaotumia njia ya mpango wa uzazi
- Watu wenye wanene sana na wenye vitambi
- Watu wanywaji wa pombe sana
- Wavutaji wa sigara sana
- Watu wapendao kula vyakula vyenye mafuta sana na chumvi nyingi.
Je, Madhara Yake Ni Nini?
Kwa kawaida ugonjwa huu unapoendelea kwa muda mrefu huku ukitumia madawa ya vidonge, madhara yake yaweza kuwa ni matatizo ya kisukari, kukosa hamu au hisia ya tendo la ndoa, pia wanaume kupungukiwa nguvu za kume.
Je, Suluhisho Lake Ni Nini?
James Herbal Clinic tunazo dawa nzuri kabisa zenye uwezo mkubwa wa kuondoa na kuzuia ugonjwa wa moyo. Pia unaweza kutuma namba yako ya WHATSAP tukakuunganisha na darasa letu la masomo ya afya.
Ikiwa kama unahitaji huduma, basi tupigie: 0768 559 670/0712 181 626,
Arusha-Mbauda,
Karibu sana!