Mambo 4 Ya Kutisha Yanayosababisha Mbegu Za Mwanaume Kuwa Chache.

Unaweza usijue kwamba una tatizo la mbegu kuwa chache (Oligospermia), umejaribu kumtungisha mwanamke mimba ili upate mtoto lakini hujafanikiwa. Vipimo vinaweza kuonyesha kwamba una mbegu chache kuliko idadi ya kawaida ya mbegu. Lakini nipende kukupa maumaini kwamba yapo matibabu ya asili yanayoweza kuondoa tatizo hili tena kwa urahisi kabisa.

Mbali na kujulikana kama idadi ndogo ya manii, lakini bado kiwango hicho kiko chini mno.  Kiwango cha chini sana cha mbegu za kiume(chini ya mbegu milioni 5 katika mililita 1 ya shahawa) hujulikana kama kiwango cha chini mno.

Nini Tofauti Kati Ya Maneno Haya Mawili, “Oligospermia Na Azoospermia?

Oligospermia inamaanisha kwamba una kiwango cha mbegu kinachopimika kwenye manii, lakini idadi ndogo kuliko kawaida. Azoospermia, maana yake ni kwamba hakuna mbegu kwenye manii zako.

Kuwa na idadi ndogo ya mbegu za kiume ni sababu kuu ya utasa. Unaweza kuwa tasa ikiwa kama umekuwa ukijaribu kumpatia mwanamke mimba lakini ikashindikana kwa mwaka mzima na hajapata mimba. Hii inamaanisha kwamba angalau kwa mwaka mzima umekuwa ukishiriki tendo la ndoa bila kutumia kinga kama vile kondom.

Je, Dalili Za Mbegu Kuwa Chache Zinakuwaje?

Dalili kuu za idadi ndogo za mbegu ni kushindwa kutungisha mimba mwanamke baada ya mwaka mmoja uliokuwa ukishiriki tendo la ndoa bila kutumia kinga ya aina yoyote.

Je, Nini Husababisha Idadi Ya Mbegu Kuwa Chache?

Yapo mambo mbalimbali ambayo yanaweza kusababisha kupatwa na hali ya idadi ya mbegu kuwa chache au magonjwa mengine ya mbegu.

Orodha ya visababishi ni Pamoja na:

  • Magonjwa, ikiwa Pamoja na maambukizi, homoni na kuziba kwa mirija
  • Sumu kwenye mazingira
  • Joto
  • Madawa

Maradhi Na Magonjwa

Baadhi ya magonjwa haya ambayo yanaweza kusababisha kuwa na kiwango kidogo cha mbegu ni Pamoja na:

  • Magonjwa ya kurithi kama vile kutokwa na ute mzito kwenye uume, nk
  • Maambukizi kama vile magonjwa ya zinaa, maambuki kwenye njia ya mkojo(UTI), na magonjwa ya virusi kama vile mapunye.
  • Maswala kama vile kiwango kidogo cha homoni ya testosterone Pamoja na mapungufu mengine ya homoni. Hali ya tezi za uzazi kushindwa kuzarisha homoni za kutosha.
  • Vizuizi ambavyo huzuia mbegu kutoka mwilini mwako.

1. Sumu

Sumu sio nzuri kwenye maeneo yoyote ya mwili wako, ikiwa Pamoja na idadi ya mbegu. Baadhi ya sumu zipo kwenye mazingira hususani mercury, shaba, na cadmium.

2. Joto

Korodani zako hufanya kazi nzuri mno katika joto maalumu, ambalo ni dogo kiasi kuliko joto la mwili wako. Hali zinazohuasiana na joto zinazoathiri uzarishaji wa manii ikiwa Pamoja na:

  • Kuwa na korodani ambazo hazijashuka. Kama korodani zikiwa bado juu, ujue kwamba ni za moto mno.
  • Kuvimba kwa mishipa ya neva inayokuwa kwenye korodani. Mishipa hii midogo inapovimba na kujisokota inaweza kuwa mikubwa na inaweza kuongeza joto kwenye korodani.
  • Kuoga maji ya moto kwa muda mrefu. Sababu hii inaweza kubadirishwa, idadi yako ndogo ya mbegu inaweza kuongezeka mara unapoacha kuoga maji ya moto

Fika hospitalini au duka la madawa ikiwa kama unadhani dawa unazotumia zinaweza kuwa zinasababisha matatizo. Usiache kutumia dawa ulizopewa maelekezo na daktari wako wala usipende kutumia madawa bila kupata maelekezo kutoka kwa daktari wako.

Mpendwa msomaji bila shaka nimefikia mwisho wa makala yetu, nipende kukaribisha kipindi cha maswali na maoni yako, karibu sana.

Pia tuna darasa letu kwenye GROUP la WHATSAPP, hivyo unaweza kutuma namba yako ya Whatasap ili uweze kuungana nasi katika kujifunza zaidi.

Unahitaji huduma, unaweza kuwasiliana nasi kupitia namba hizi: 0768 559 670 au 0712181626,

Arusha-Mbauda,

Karibuni sana!

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *