Bawasiri ni uvimbe unaokuwa na mishipa iliyotuna ambayo hupatikana ndani au maeneo ya chini (njia ya haja kubwa).
Kwa namna nyingine, bawasiri huwa haionyeshi dalili, na watu wengine hata hawatambui kuwa wanalo tatizo hilo. Walakini, dalili zinapotokea, zinaweza kuwa kama hivi:
- Kutokwa na damu kwenye njia ya haja kubwa baada ya kujisaidia
- Kuhisi muwasho maeneo ya njia ya haja kubwa
- Uvimbe kutokeza nje ambao unapaswa kurudishwa baada ya kujisaidia
- Kutokwa na ute utelezi sehemu ya njia ya haja kubwa baada ya kujisaidia
- Vidonda, wekundu na uvimbe maeneo ya njia ya haja kubwa.
Je, Nini Husababisha Ugonjwa Huu?
Sababu halisi ya bawasiri, wengi hushindwa kuifahamu, lakini inahusishwa na kuongezeka kwa shinikizo katika mishipa ya damu ndani na maeneo na njia yako ya haja kubwa. Shinikizo hili linaweza kusababisha mishipa ya damu kwenye njia ya haja kubwa kuvimba.
Matukio mengi yanafikiriwa kuwa yanasababishwa na shida nyingi pale unapoenda kujisaidia halafu kinyesi kinatoka kigumu kwasababu na kukosa choo kwa muda mrefu kutokana na ulaji wa vyakula vilivyosindikwa au kukobolewa kama vile ugali wa sembe, mikate myeupe, maadazi, chips, nk.
Mambo mengine ambayo yanapelekea upate ugonjwa wa bawasiri ni kama haya yafuatayo:
- Kuwa mnene kupita kiasi
- Tishu za mwili kuwa dhaifu kutoka na umri kuwa mkubwa
- Kuwa mjmzito
- Kunyanyua vitu vizito
- Kikohozi cha muda mrefu
- Kukaa chini muda mrefu
Je, Nini Cha Kufanya Ili Kuzuia Na Kutibu Bawasiri?
Dalili za bawasiri mara nyingi hutulia baada ya siku chache, bila kuhitaji matibabu. Bawasiri ambayo hutokea wakati wa ujauzito mara nyingi hupona baada ya kujifungua.
Walakini, kufanya mabadiliko ya mtindo wa maisha ili kupunguza mzigo kwenye mishipa ya damu ndani na maeneo ya njia ya haja kubwa mara nyingi hupendekezwa. Hizi zinaweza kujumuisha:
- kunguza ulaji wa vyakula vilivyokobolewa au vilivyosindikwa, bali tumia matunda, mgogamboga, ngano au mkate unaotokana na ngano haijakobolewa, karanga, nk
- kunywa vinywaji vingi, hasa maji ya kunywa. Epuka sana vinywaji vya viiwandani, soda, kahawa na pombe
- usichelewe kwenda haja kubwa, kumbuka unapokaa muda mrefu bila kwenda choo, kinyesi hutoka kigumu,
- epuka madawa ya vidonge yanayosababisha kukosa choo kama vile, vidonge vya kupunguza maumivu vyenye wingi wa codeine,
- punguza uzito kama una uzito mkubwa
- fanya mazoezi mara kwa mara,
Hatua hizi pia zinaweza kupunguza hatari ya kurudi kwa bawasiri, au hata kupata bawasiri mara ya kwanza.
Ndugu msomaji, makala yetu inaishia hapa, naomba nikaribishe kipindi cha maswali na maoni yako.
Je, Nini Suluhisho Lake?
James Herbal Clinic tunazo dawa nzuri kabisa zenye uwezo mkubwa wa kuondoa tatizo hili kwa muda mfupi tu.
Unahitaji huduma? Basi wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626.
Pia unaweza kutuma namba yako ya WhatsAp ili tukuunganishe kwenye darasa letu la masomo ya afya.
Arusha-Mbauda,
Karibuni Sana!