Mambo Makuu 5 Yanayosababisha Miguu Au Mwili Kuvimba (Edema)

Kuvimba kwa mwili ni hali inayosababishwa na umajimaji mwingi unaojikusanya kwenye tishu za mwili, amabayo kitaalamu tunaita “edema”. Edema inaweza kuathiri sehemu yoyote ya mwili. Lakini kuna uwezekano mkubwa wa kuonekana kwenye miguu na mikono.

Madawa na ujauzito vinaweza kusababisha mwili kuvimba. Inaweza pia kuwa matokeo ya ugonjwa, kama vile moyo kushindwa kufanya kazi, ugonjwa wa figo, matatizo ya ini, nk.

Kuvaa nguo zisizo za kubana na kupunguza matumizi ya chumvi nyingi kwenye chakula mara nyingi hupunguza mwili kuvimba (edema). Pale ugonjwa unposababisha mwili kuvimba, basi ndipo unahitaji matibabu, haraka.

Je, Dalili Zake Zinakuwaje?

Dalili za kuvimba kwa mwili huwatatanisha wengi sana lakini, ishara au dalili zake huwa kama hizi zifuatazo:

  • Kuvimba kwa miguu au mikono
  • Ngozi ya mwili kumelemeta
  • Ngozi kubonyea pale inapobonyezwa
  • Tumbo kuvimba na kuwa kubwa kuliko kawaida
  • Miguu kuhisi kuwa mizito

Je, Chanzo Chake Ni Nini?

Edema hutokea wakati mishipa midogo ya damu mwilini, inayojulikana pia kama kapilari, inapovuja maji. Maji hukusanyika kwenye tishu zilizo karibu. Hali hii ya kuvuja majimaji husababisha uvimbe.

Visababishi vyake ni pamoja na:

  • Kukaa sehemu moja kwa muda mrefu
  • Kula vyakula vyenye chumvi nyingi
  • Kuwa mjamzito

Kuvimba kwa mwili kunaweza pia kuwa madhara ya matumizi ya madawa kama vile:

  • Madawa ya presha ya kunda
  • Madawa ya kupunguza uvimbe au maumivu
  • Kushuka kwa homoni ya estrogen
  • Madawa fulani ya kisukari yanayoitwa thiazolidinediones
  • Dawa zinazotumika kutibu maumivu ya mishipa

Wakati mwingine edema inaweza kuwa ishara ya hali mbaya zaidi, ndio maana kuna mambo makuu 5 yanayoweza kusababisha hali hii. Magonjwa ambayo yanaweza kusababisha edema ni pamoja na:

  • Moyo Kushindwa Kusukuma Damu Ya Kutosha:Moyo kushindwa kusukuma damu ya kutosha husababisha chumba kimoja au viwili vya moyo kushindwa kusukuma damu vizuri. Matokeo yake, damu hurudi kwenye miguu, na kwenye vifundo na hatimaye kusababisha kuvimba. Kushindwa kwa moyo kusukuma damu kunaweza pia kusababisha uvimbe katika eneo la tumbo. Hali hii pia inaweza kusababisha maji kukusanyika kwenye mapafu. Inajulikana kama edema ya mapafu, hii inaweza kusababisha kushindwa kupumua.
  • Kuharibika Kwa Ini:Uharibifu huu wa ini kutokana na ini kuvimba unaweza kusababisha maji kukusanyika kwenye eneo la tumbo na kwenye miguu. Mkusanyiko wa maji katika eneo la tumbo huitwa ascites.
  • Ugonjwa Wa Figo:Ugonjwa wa figo unaweza kusababisha mkusanyiko wa maji na chumvi kwenye damu. Uvimbe wa mwili inaohusishwa na ugonjwa wa figo kwa kawaida hutokea kwenye miguu na maeneo ya macho.
  • Figo Kuharibika:Uharibifu wa mishipa midogo ya kuchuja damu kwenye figo inaweza kusababisha ugonjwa wa nephrotic. Katika ugonjwa wa nephrotic, kupungua kwa viwango vya protini katika damu kunaweza kusababisha mwili kujaa maji (edema).
  • Kudhoofika Au Kuharibika Kwa Mishipa Miguuni:Hali hii, inayojulikana kama madhaifu ya mishipa ya moyo kushindwa kurudisha damu, hudhuru vali za njia moja kwenye mguu. Vali za njia moja huifanya damu kupita kwenye mwelekeo mmoja. Uharibifu wa vali huruhusu damu kujikusanya kwenye mishipa ya mguu na kusababisha uvimbe.

Je, Madhara Yake Ni Nini?

Ugonjwa wa edema usipotibiwa husababisha madhara haya yafuatayo:

  • Uvimbe ambao husababisha maumivu makali
  • Kushindwa kutembea
  • Miguu kukakamaa
  • Ngozi kuwasha
  • Kuongezeka kwa madhara kwenye eneo lililovimba
  • Michubuko kwenye eneo lililovimba
  • Damu kutembea kidogo sana
  • Mishipa ya ateri kusafirisha damu taratibu sana
  • Ngozi kupatwa na vidonda

Je, Nini Suluhisho Lake?

James Herbal Clinic tunazo dawa nzuri kabisa zenye uwezo mkubwa wa kuondoa ugonjwa wa edema. Unahitaji huduma, naomba wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626,

Pia unaweza kutuma namba yako ya WHATSAP ili tukuunganishe na darasa letu la masomo ya afya ambalo utajifunza mara kwa mara.

Arusha-Mbauda

Karibu sana!