Lehemu (cholesterol) ni mafuta yenye kuganda, yenye kuonekana kama nta ambayo hupatikana kwa asili katika seli zote za mwili. Lehemu hutumika kujenga seli, kutengeneza homoni, na husaidia katika kuyeyusha chakula tumboni. Ini lako linaweza kutengeneza vyote unavyohitaji. Lakini pia lehemu hupatikana katika vyakula vya wanyama kama vile maziwa, mayai, pamoja na mafuta yaliyosindikwa, nk.
NUKUU: Lehemu inapozidi kuwa nyingi hukusanyika kama chembechembe za mafuta kwenye kuta za mishipa ya ateri. Chembechembe hizi hujengeka taratibu, pamoja na damu iliyoganda ili kujenga utando kwenye kuta za mishipa ya ya damu. Matokeo yake ni ugonjwa wa moyo.
Hatimaye mgando wa mafuta huu huifanya damu kushindwa kutiririka kwenye mishipa yako ya ateri. Moyo wako unaweza kushindwa kupata hewa ya oksijeni ya kutosha kama inavyohitajika, hali ambayo huongeza hatari ya shambulio la moyo. Kupungua kwa mtiririko wa damu kwenye ubongo wako kunaweza kusababisha kiharusi.
Je, Dalili Zake Zinakuwaje?
Muongezeko wa kolestero huwa hauna dalili za moja kwa moja za nje. Vipimo vya damu ni njia pekee ya kutambua kiwango kikubwa cha mafuta kwenye damu. Dalili zinaweza kuwa zile shinikizo la juu la damu kama vile:
- Miguu kuuma au kuwaka moto
- Kifua kubana au kuuma
- Shambulio la moyo
Je, Nini Husababisha Lehemu Kwenye Damu?
Lehemu(cholesterol) hubebwa kupitia damu ikiwa imeambatana na protini. Mchanganyiko wa protini na kolestero kitaalamu huitwa, “Lipoprotin”. Unaweza kuwa umesikia aina tofauti za kolestero, hasa aina za kolestero ambazo lipoprotein hubeba.
Hapa kuna baadhi ya mambo juu ya lehemu ambayo yanaweza kukusaidia kuelewa hali halisi, nayo ni:
- Low-Density Lipoprotein(LDL)
Hii huwa ni lehemu iliyoganda kwenye mishipa ya ateri na huwa mbaya zaidi katika mwili wako. Ni nzuri sana inapokuwa kidogo. Zipo njia mbalimbali za asili unazoweza kutumia ili kupunguza lehemu mwilini.
Hii huwa ni hali ya mlundikano wa mafuta mabaya katika mwili mzima. Mafuta haya hujengeka ndani ya kuta za mishipa yako ya ateri, na kuifanya kuwa migumu na kushindwa kutanuka pale damu inaposukumwa na moyo wako.
- High-Density Lipoprotin(HDL)
Hii ni aina ya lehemu ambayo husafisha mishipa yako ya ateri na huwa nzuri sana kwa afya yako. Inapokuwa nyingi, ndivyo inavyoonyesha ubora wake.
Mambo Hatarishi
Mambo ambayo yanaweza kuongeza hatari ya mafuta kwenye damu (cholesterol) ni pamoja na:
- Lishe duni: Kula mafuta ya mgando, yanayopatikana katika bidhaa za wanyama, na mafuta ya siagi, kama vile blue band, Cowboy, Kasuku, Kimbo, nk. Vyakula vilivyo na kolesteroli nyingi, kama vile nyama nyekundu na bidhaa za maziwa zilizojaa mafuta, pia huongeza mafuta (cholesterol) mwilini.
- Unene
- Kutokufanya Mazoezi: Mazoezi husaidia kuongeza HDL ya mwili wako, au kuweka kiwango kizuri cha mafuta mwilini.
- Uvutaji Sigara: Uvutaji wa sigara huharibu kuta za mishipa yako ya damu, na kuifanya iwe na uwezekano wa kukusanya mrundikano wa mafuta.
- Kisukari: Sukari ya juu ya damu huchangia kiwango cha juu cha mafuta kwenye damu (HDL) au kupunguza kiwango cha mafuta kwenye damu (LDL). Sukari ya juu kwenye damu pia huharibu kuta za mishipa ya damu.
NUKUU: Wakati mwingine hii inaitwa Lehemu “nzuri”. Inafyonza mafuta au lehemu kwenye damu na kuirudisha kwenye ini. Kisha ini huiondoa kabisa kwenye mwili. Viwango vya juu vya lehemu (cholesterol) vinaweza kupunguza hatari ya ugonjwa wa moyo na kiharusi.
Je, Madhara Yake Ni Nini?
Cholesterol ya juu inaweza kusababisha mkusanyiko mkubwa wa mafuta kwenye kuta za mishipa ya moyo (atherosclerosis). Mgandamano wa mafuta haya unaweza kupunguza mwendo wa damu kupitia mishipa yako, ambayo inaweza kusababisha matatizo, kama vile:
- Maumivu ya kifua: Iwapo mishipa inayoupa moyo wako damu (mishipa ya moyo) imeathirika, unaweza kuwa na maumivu ya kifua (angina) na dalili nyingine za ugonjwa wa mishipa ya ateri moyo.
- Shambulio la moyo: Kama mgandamano wa mafuta kwenye mishipa ukibanduka, mabonge ya damu yanaweza kujengeka donge la damu linaweza kutokea mahali palipopasuka, huziba mtiririko wa damu au kukatika na kuziba ateri kwenye mkondo wake. Ikiwa mtiririko wa damu kwenye sehemu ya moyo wako utakoma, basi utapata mshtuko wa moyo.
- Kiharusi: Kama vile inavyokuwa kwenye mshtuko wa moyo, vile vile ikiwa mtiririko wa damu kwenye sehemu ya ubongo wako imezibwa na mabonge ya damu, basi kiharusi hutokea.
Jinsi Ya Kujiepusha Na Ugonjwa Huu
Mabadiliko yale yale ya maisha yenye afya ya moyo ambayo yanaweza kupunguza kolesteroli yako yanaweza kukusaidia kukuzuia kuwa na kiwango kikubwa cha kolesteroli mara ya kwanza. Ili kuzuia kiwango kikubwa cha cholesterol, unaweza:
- Kula mlo wenye chumvi kidogo unaojumuisha matunda, mboga mboga na nafaka nyingi
- Punguza kiasi cha mafuta ya wanyama na tumia mafuta mazuri kwa kiasi
- Punguza uzito wa mwili wako
- Acha kuvuta sigara
- Fanya mazoezi mara kwa mara.
- Acha matumizi ya pombe.
Je, Nini Suluhisho Lake?
James Herbal Clinic tunazo dawa nzuri zenye uwezo mkubwa wa kuondoa magonjwa ya moyo. Unahitaji huduma wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626. Pia unaweza kutuma namba zako za WHATSAP ili tuweze kukuunganisha kwenye darasa letu la masomo ya afya.
Arusha-Mbauda,
Karibu sana.