Mzunguko wako wa hedhi unaweza kuonyesha mambo mengi juu ya afya ya mwili wako. Sasa leo naomba uelewe jinsi ya kuanza kuhesabu mzunguko wako wa hedhi na jinsi gani unaweza kufanya pale mzunguko wa hedhi unapobadirika.
Je, unafahamu ni lini kipindi chako cha hedhi kilianza au ni muda gani hedhi iliisha? Kama hufahamu, basi unapaswa uanze kuwa na tahadhari tena kuwa makini. Kuweka alama ya vipindi vyako vya mzunguko wa hedhi kunaweza kukusaidia kuelewa ni kipindi gani cha kawaida kwako, kipindi cha kuvusha mayai, na kutambua mabadiriko muhimu kama vile kukosa hedhi, au kipindi cha hedhi kisichotabirika. Japokuwa kubadirika kwa mzunguko wa hedhi mara nyingi huwa sio tatizo sana, lakini wakati mwingine inaweza kuwa ishara au dalili ya matatizo yaliyomo mwilini mwako.
Je, Mzunguko Wa Hedhi Ni Nini?
Mzungo wa hedhi ni mabadiriko yanayojitokeza kila mwezi katika mwili wa mwanamke pale unapojiandaa ili apate ujauzito. Kila mwezi, kati ya kifuko kimoja cha yai hutoa yai likiwa limekomaa, hali ambayo kitaalamu tunaita, “Ovulation”.
NUKUU: Muda huo huo, mabadiriko ya vichochezi au homoni hukiandaa kifuko cha uzazi(uterus) kwa ajili ya ujauzito. Kama upevukaji wa yai ukiwadia na yai likashindwa kurutubishwa, basi ngozi laini inayokuwa kwenye ukuta wa mfuko wa kizazi(uterus) hubanduka kupitia uke. Hiki ndio kipindi cha hedhi.
Je, Kipindi Gani Cha Hedhi Ambacho Ni Cha Kawaida?
Mzunguko wa hedhi ambao huhesabiwa kuanzia siku ya kwanza ya kipindi cha hedhi mpaka siku ya kwanza ya kipindi kinachofuata, huwa haufanani kwa kila mwanamke. Mzunguko wa hedhi lazima uonekane kila siku 21-35 na kudumu muda wa siku 2-5. Kwa miaka michache ya kwanza baada ya hedhi kuanza, mzunguko wa muda mrefu huwa ni jambo la kawaida. Hata hivyo, mzunguko wa hedhi huonekana kufupika na kutobadirika kadiri unavyozidi kuwa na umri mkubwa.
NUKUU: Mzunguko wako wa hedhi sharti urefu wake kila mwezi usibadirike, wala damu yako ya hedhi isiwe nyepesi wala nyingi sana, wala kusiwepo na maumivu. Hivyo hedhi inapaswa iwe ya kawaida kabisa.
Kumbuka kwamba matumizi ya madawa ya uzazi wa mpango yanaweza kuharibu mzunguko wako wa hedhi. Hivyo James & Ferdinand Herbal Clinic tunakushauri uonane na daktari mapema pale unapoona dalili kama hizo.
Unapokaribia muda wa kukoma hedhi, mzunguko wako wa hedhi huanza kubadirika tena. Hata hivyo, kwasababu hatari ya salatani ya tumbo la uzazi huongezeka kadiri umri wako unavyozidi kuongezeka. Hivyo basi, jitahidi sana kufika hospitali haraka ili kumweleza daktari matatizo ya kubadirika kwa hedhi yanapokutokea.
Je, Unawezaje Kuweka Alama Ya Mzunguko Wako Wa Hedhi?
Ili kutambua nini kilicho cha kawaida kwako, basi nakushauri uanze kuweka kumbukumbu kwenye Kalenda ya mzunguko wako wa hedhi. Anza kuweka alama kila mwezi ya tarehe ya hedhi yako inapoanza. Fanya hivyo kila mwezi ili uweze kugundua kama vipindi vyako vya hedhi havibadiriki.
Kama vipindi vyako vya hedhi vinaendelea vizuri, basi pia weka kumbukumbu ya mambo yafuatayo kila mwezi:
- Tarehe Ya Mwisho: Je, kipindi chako cha hedhi kinadumu muda gani? Je, ni muda mrefu au mfupi kuliko kawaida?
- Mtiririko Wa Damu: Weka kumbukumbu ya mtiririko mkubwa wa damu. Je, ni damu nzito au nyepesi kuliko kawaida? Je, ni mara ngapi unabadirisha ped? Je, umepitisha damu yoyote iliyoganda?
- Kutokwa Na Hedhi Isiyo Ya Kawaida: Je, unatokwa na damu ya hedhi mara mbili kwa mwezi?
- Mumivu: Elezea maumivu yoyote yanayoambatana na hedhi yako. Je, maumivu unayahisi kuwa makali kuliko kawaida?
Je, Nini Husababisha Mzunguko Wa Hedhi Kubadirikabadirika?
Mzunguko wa hedhi kubadirika unaweza kuwa na visababishi mbalimbali hasa kama ifuatavyo:
- Ujauzito au kunyonyesha
- Vivimbe kwenye vifuko vya mayai
- Yai kushindwa kukomaa
- Maambukizi ya magonjwa katika via vya uzazi(PID)
- Uvimbe kwenye tumbo la uzazi(fibroid)
- Utumiaji wa vyakula vibaya, uzito wa mwili kupungua au kufanya mazoezi mazito
Je, unahitaji huduma? Tupigie kwa namba zifuatazo: 0752389252 au 0712181626
Arusha-Mbauda pia Njombe-Makambako
Karibuni sana!