Maambukizi ya PID ni maambukizi yanayosababishwa na magonjwa ya zinaa yasiyotibiwa au maambukizi mengine. Takwimu inaonyesha karibia watu zaidi ya milioni 1 hupatwa na maambukizi ya PID kila mwaka. Katika wanawake 8 mmoja anaweza kukutwa na maambukizi ya PID likionyesha matatizo ya uzazi. Mbali na madhara, lakini bado ugonjwa huu unaweza ukatibiwa mapema na kuzuia mwanamke asiwe na masumbufu katika kupata mimba.

NUKUU: Watu wengi hupenda kuuliza kuwa PID ni japokuwa wamepata vipimo na wakapewa kadi ya vipimo kuwa tatizo ni PID lakini hawajapewa maana ya neno hili!
Kwa kawaida PID ni maambukizi katika viungo vya uzazi vya mwanamke yaliyosababishwa na maambukizi ambayo hayakutibiwa kama vile magonjwa ya ngono(kisonono, pangusa) au maambukizi mengine zaidi, yanayokuwa ukeni. Bakteria wanaokuwa ukeni au mlango wa kizazi wanaweza kuingia kwenye mirija ya uzazi na vifuko vya mayai na kusababisha maambukizi.
Dalili za PID huwa ni pamoja na:
- Maumivu ya tumbo la chini
- Homa
- Kutokwa na uchafu ukeni wenye harufu kali
- Kuhisi hali ya kuwaka moto ukeni
- Kupata hedhi mara mbili ndani ya mwezi mmoja
- Kuhisi maumivu makali wakati wa tendo la ndoa
Wakati magonjwa ya zinaa ndio chanzo kikubwa, PID inaweza pia kutokea wakati wa utaratibu ufuatao wa matibabu:
- Kujifungua
- Mimba kuharibika
- Kutoa mimba
- Kizazi kulegea
- Kuweka kitanzi au kufunga kizazi
Je, Madhara Ya Maambukizi Ya PID Ni Nini?
Wanawake wengi wanapopatwa na tatizo hili hulichukulia kama hali ya kawaida katika afya ya miili yao, na hivyo hufanya kama kulifuga na kuishi nalo kwa muda mrefu ambapo baadaye husababisha madhara makubwa kama haya:
- Michubuko kwenye mirija ya uzazi ambayo hupelekea mirija kuziba
- Vivimbe kwenye vifuko vya mayai(ovarian cysts)
- Mirija ya uzazi kujaa maji
Kuchubuka kwa mirija ya uzazi kunaweza kusababisha maumivu ya nyonga ya muda mrefu. Kuziba kwa mirija ya uzazi kunaweza kuzuia mbegu zisiweze kulifikia yai, hali ambayo inaweza kupelekea ugumba.
Wakati wa ujauzito, kuziba kwa mrija wa uzazi kunaweza kusababisha mimba kutunga nje ya kizazi(ectopic pregnancy). Tatizo la mimba kutunga nje ya kizazi huongeza vihatarishi vya mirija kupasuka, hali ambayo inaweza kusababisha maumivu, kutokwa na damu ukeni au uchafu. Kila mwaka, wanawake karibia 100,000 hupatwa na hali ya kutokupata mimba kutokana na maambukizi ya PID.
Jinsi Ya Kukinga, Kupima Na Kutibu Maambukizi Ya PID
Njia pekee ya kuzuia maambukizi ya PID ni kujiepusha na mambo ya ngono. Vinginevyo, kufanya tendo la ndoa kwa kutumia kinga kunaweza kusaidia vihatarishi vya maambukizi ya PID. Kuwa na mpenzi mmoja bila kuchepuka pia kunaweza kusaidia sana kujiepusha na maambukizi ya PID.
Hakuna kipimo chochote cha PID, bali daktari anaweza kuangalia historia ya tatizo lako kutokana na maelezo yako au vipimo ulivyowahi kufanya kama vile kupima magonjwa ya zinaa, au vipimo vya Ultrasound kuangalia matatizo yoyote. Kwakuwa dalili za PID huonekana kuwa za kawaida sana, basi wanawake ndio maana hushindwa kujali juu ya maambukizi haya. Kwahiyo daktari anaweza kukupatia vidonge vya antibiotic ili kupambana dhidi na maambukizi.
Je, Wanawake Wenye PID Wanaweza Kupata Mimba?
Wanawake wengi wanagundua mapema dalili za PID wanaweza kupunguza vihatarishi vyao vya kutokewa na uharibifu wa kudumu na kuwa wajawazito. Mbaya zaidi, wanawake wenye historia ya PID wanatafuta mtaalamu wa matatizo ya uzazi ili ahusike na madhara ya PID. Hivyo, PID inaweza kuzuiwa kuendelea na, kupitia madawa mbalimbali hasa ya asili, mwanamke anaweza kupata ujauzito.
Ndugu msomaji makala yetu hii inaishia hapa, napenda kukaribisha kipindi cha maswali na maoni kutoka kwako, ubarikiwe sana!
Pia unaweza kutuma namba yako ya WHATsAP tukaweza kukuunganisha na GROUP letu ili uweze kupata masomo zaidi ya afya.
Je, Unahitaji Pia Huduma?
Wasiliana nasi kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626,
Arusha-Mbauda Maua
Karibuni sana!