Ni kawaida kushangaa endapo kama rangi au uchafu unatoka mara kwa mara ukeni kuwa ni wa kawaida au unahitaji kuchunguzwa. Uchafu utokao ukeni unaweza kuwa na rangi nyingi, na viashiria mbalimbali ili kuonyesha kuwa mwili una afya.
Katika makala hii tunaenda kujifunza ili tujue je, ute unaolinda maeneo ya uke unakuwa na rangi gani?
Je, Uchafu Unaotoka Ukeni Huwa Ni Kitu Gani?
Uchafu utokao ukeni huwa ni majimaji fulani yanayotengenezwa kutoka kwenye tezi ndogo zinazokuwa ukeni na kwenye mlango wa kizazi. Maji maji haya huvuja kutoka ukeni kila siku ili kuondoa seli zilizochoka pamoja na mabaki, ili kuufanya uke pamoja na njia ya mfumo wa uzazi uwe katika hali yenye afya nzuri.
Kiwango cha uchafu unaotoka ukeni kinaweza kutofautiana kwa kila mwanamke. Rangi, uzito, na kiwango vinaweza pia kubadirika kila baada ya siku, kutegemeana na mazingira ya mwanamke anapokuwa hedhini:
- Siku ya 1-5
Mwanzoni mwa mzunguko wa hedhi, uchafu unaotoka ukeni mara nyingi huwa mwekundu au wenye damudamu, kadiri mwili unavyotumia nguvu kuliondoa gamba laini linalokuwa juu ya ukuta wa mfuko wa kizazi.
- Siku ya 6-14
Kipindi cha hedhi kinachofuata, mwanamke anaweza kuona damu kidogo ikitoka ukeni kuliko kawaida. Yai linapoanza kukua na kukomaa, basi ute utelezi unaokuwa kwenye mlango wa kizazi utabadirika na kuwa wenye rangi ya kijivu au mweupe au wa njano. Mwanamke anaweza kuwa mzito.
Unaweza ukaona hapo juu kwenye picha jinsi uchafu huu unavyokuwa.
- Siku ya 14-25
Siku chache baada ya yai kupevuka, ute utelezi hubadirika na kuwa mwepesi wenye kuteleza, kama ute wa yai la kuku vile. Baada ya yai kupevuka, ute hubadirika na kuwa wenye rangi ya kijivu, mweupe au wa njano, na wenye kunata.
Hizi ni siku ambazo huwa ni za hatari ambazo mwanamke anapata ujauzito kwa urahizi kabisa.
- Siku ya 25-28:
Ute utelezi unaokuwa kwenye shingo ya kizazi hubadirika na kuwa mwepesi, na mwanamke anaweza kuuona kidogo tu, kabla hajaingia kwenye kipindi kingine cha hedhi.
- Uchafu Wenye Rangi Nyekundu
Uchafu huu mwekundu unaweza kutofautiana, kwani unaweza kuwa wenye rangi yenye kung’aaa au nyekundu sana. Uchafu mwekundu huwa ni matokeo ya damu ya hedhi kuanza kutoka.
Damu ya hedhi hutokea, kwa wastani, kwa kila mzunguko wa siku 28, ingawa kiwango cha kati huwa ni siku 21 na 35. Hedhi huwa ni ya siku 3-5.
NUKUU: Mwanamke yeyote anayepata hedhi mara mbili ndani ya mwezi mmoja, anapaswa afike hospitali mapema ili kumuona daktari. Ingawa kuna visababishi vingi hafifu vya kumfanya mwanamke apate hedhi mara mbili kwa mwezi, lakini navyo vinaweza wakati mwingine kuwa viashiria vya matatizo mabaya baadaye.
Mwanamke yeyote aliyefikia hali ya kukoma hedhi na kutokuona hedhi kwa takribani mwaka mmoja, anapaswa amuone daktari mapema ikiwa kama anapatwa na hali ya kutokwa na damu ukeni. Hii yaweza kuwa ni dalili ya salatani.
- Uchafu Mweupe
Uchafu mweupe unaweza kuongezeka, unaweza ukawa kama maziwa vile au wa njanonjano kwa mbali. Endapo mwanamke hatakuwa na dalili zingine, basi uchafu mweupe unaweza kuwa kiashiria kabisa cha kilainishio kizuri chenye afya ukeni mwake. Utakuta uke wake uko katika hali nzuri hata anapokutana kimapenzi na mwenzi wake hakutakuwa na shida yoyote zaidi ya kufurahia tendo la ndoa.
NUKUU: Hata hivyo, endapo kama uchafu mweupe utakuwa mzito kama maziwa mtindi vile na kuwa na harufu mbaya, basi hii yaweza kuwa dalili za maambukizi. Muhusika anapaswa afike hospitali haraka bila kuchelewa ili kumuona daktari wa vipimo.
Uchafu mweupe wenye kunata, na wenye harufu mbaya mara nyingi huwa ni wenye maambukizi ya fangasi, ambao pia unaweza kusababisha muwasho ukeni.
- Uchafu Wenye Rangi Ya Njano Na Ukijani
Kama uchafu una rangi ya njano njano, inaweza isiashirie tatizo kwako. Hali hii hasa inaweza ikasababishwa kubadirika kutokana na vyakula unavyotumia.
Uchafu ambao ni wa njano kabisa, unjano wenye ukijani, au kijani yenyewe, mara nyingi huwa ni dalili za bakteria au maambukizi ya magonjwa ya zinaa. Jitahidi kumuonda daktari mapema endapo kama uchafu ni mzito na wenye harufu mbaya.
- Uchafu Wenye Rangi Ya Pink
Uchafu unaweza kuwa wenye rangi ya pinki kwa mbali au kabisa. Mara nyingi huwa unakuwa na damudamu kidogo. Uchafu wenye rangi ya pinki kwa kawaida hujitokeza huku ukiwa na matone ya damu damu kabla ya kipindi cha hedhi kuwadia. Hata hivyo, inaweza pia kuwa ishara ya damu kutoka pale yai linapojipachika kwenye ukuta wa tumbo la uzazi ujauzito unapoingia.
NUKUU: Baadhi ya wanawake hutokwa na matone ya damu damu baada ya yai kupevuka, hali ambayo pia inaweza kusababisha kutokwa na uchafu wa pink. Uchafu unaweza kuwa wenye rangi ya pink baada ya kufanya tendo la ndoa, endapo kama tendo lenyewe limesababisha maumivu kidogo au muwasho ukeni au maeneo ya mlango wa kizazi.
- Uchafu Msafi
Uchafu wa kawaida huwa ni msafi mweupe. Unaweza kuwa mwepesi au ukawa na uzito kama ute wa yai vile. Mwanamke anaweza akatokwa na uchafu mweupe msafi, mwepesi kabla yai halijapevuka, au wakati hisia au nyege zinapompanda, au anapopata ujauzito.
- Uchafu Wenye Rangi Ya Ukijivu
Uchafu unaotoka ukeni huku ukiwa na rangi ya kijivu huwa sio mzuri, na inaweza kuwa dalili za maambukizi ya bakteria wajulikanao kama, “Bacterial Vaginosis(BV)”.
Bakteria hawa kwa kawaida husababisha dalili zingine ukeni kama vile;
- Muwasho
- Hali ya kama moto ukeni
- Harufu mbaya ukeni
- Hali ya wekundu maeneo ya mashavu ya uke au mlango wa uke
NUKUU: Mwanamke yeyote anayetokwa na uchafu wenye rangi kama ukijivu pamoja na dalili zake hizo anapaswa kufika hospitali haraka sana bila kuchelewa.
Je, Ni Lini Unapaswa Kumuona Daktari?
Nakushauri umuone daktari ikiwa kama uchafu una harufu au muonekano usi wa kawaida . Mwanamke napaswa pia kutafuta tiba endapo kama anapatwa na dalili kama zifuatazo:
- Muwasho
- Maumivu au kutojisikia raha
- Uchafu mzito kama maziwa ya mgando
- Kutokwa na damu mara mbili kwa mwezi au baada ya hedhi kukoma
- Kutokwa na damu baada ya kufanya tendo la ndoa
- Kutokwa na damu kila mara baada ya kufanya tendo la ndoa
- Kutokwa na uchafu wenye rangi ya njano, ukijivu, au kijani
- Kutokwa na uchafu wenye harufu mbaya
- Kuhisi maumivu makali wakati wa kukojoa
NUKUU: Daktari atapima maeneo ya nyonga. Pia anaweza kuchukua uchafu kidogo ili kufanya vipimo.
Je, unahitaji huduma? Tupigie kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626
Arusha-Mbauda
Karibuni sana