Je, Nini Husababisha Vipindi Vya Hedhi Kubadirika?
Mzunguko wa hedhi huhesabiwa kuanzia siku ya kwanza kipindi cha hedhi kinapoanza. Hedhi yako inakuwa yenye kubadirika ikiwa kama ina siku 38 au kama kuchelewa kwake hutofautiana.
Vipindi vya hedhi kubadirika vinaweza kuwa na visababishi vikubwa, kuanzia hali ya kutokuwa na uwiano sawa wa homoni pamoja na hali zingine, na hali hizi zinapaswa kufanyiwa uchunguzi na daktari. Hapa unaweza kuona visababishi na dalili za tatizo hili.
- Ujauzito
Ujauzito unaweza kukufanya ukakosa kipindi cha hedhi au ukaona matone tu ya damu. Dalili zingine za mimba inapokuwa change zinaweza kuwa kama ifuatavyo:
- Kutapika
- Kichefuchefu
- Kuhisi harufu mbaya
- Matiti kuuma
- Kuhisi uchovu
NUKUU: Kama ukikosa hedhi au kuona mabadiriko katika kipindi cha hedhi na huku unafanya tendo la ndoa, basi unaweza ukafanya vipimo vya ujauzito nyumbani au unaweza kwenda kumuona daktari ili aweze kupima aone kama ni mjamzito.
Ikiwa kama una ujauzito, na unahisi maumivu makali kwenye nyonga au maeneo ya tumbo la chini ambayo hudumu kwa dakika kadhaa, basi muone daktari aweze kupima ikiwa kama una tatizo la mimba kutunga nje ya kizazi au mimba kuporomoka.
- Matumizi Ya Madawa Ya Uzazi Wa Mpango
Madawa ya mpango wa uzazi yanaweza kusababisha vipindi vya damu ya hedhi kubadirika. Vidonge hivi vinaweza kusababisha hali ya kutokwa na matone ya damu kwa muda wa siku 2 au kusababisha damu ya hedhi kuwa nyepesi.
Unaweza ukaona hapo juu jinsi inavyokuwa kwa wanawake pale wanapotokwa na matone ya damu.
- Kunyonyesha
Prolactin ni homoni ambayo inahusika katika kuzarisha maziwa. Prolactin huzuia homoni za uzazi na kusababisha damu ya hedhi kutoka kidogo tu au kutokuona kabisa hedhi hata kidogo wakati unaponyonyesha.
NUKUU: Vipindi vyako vya hedhi vinaweza kurejea muda mfupi baada ya kuachisha mtoto kunyonya.
- Mabadiriko(Perimenopause)
Mabadiriko haya hujitokeza kabla mwanamke hajakoma hedhi. Hali hii kwa kawaida huanza mwanamke anapofikia umri wa miaka 40, lakini yanaweza kujitokeza mapema.
Mwanamke anaweza akaona dalili za kukosa hedhi zinazoweza kudumu kwa muda wa miaka 4-8, zikianza na mabadiriko kwenye mzunguko wa hedhi. Kupanda na kushuka kwa viwango vya homoni ya estrogen katika kipindi hicho kunaweza kusababisha mzunguko wa hedhi kuwa mrefu au mfupi.
Dalili zingine za mabadiriko haya huwa kama ifuatavyo;
- Kutokwa na jasho jingi mida ya usiku
- Kukosa hamu ya tendo la ndoa
- Kukosa usingizi
- Uke kuwa mkavu
- Vivimbe Kwenye Vifuko Vya Mayai
Vipindi vya hedhi kubadirika huwa ni ishara au dalili za vivimbe kwenye vifuko vya mayai. Kama una vivimbe kwenye vifuko vya mayai, unaweza ukakosa hedhi mwezi mmoja au miezi kadhaa na inapokuja hedhi unaweza kutokwa na damu nyingi sana huku ikiwa na mabonge.
NUKUU: Vivimbe kwenye vifuko vya mayai vinaweza pia kusababisha mambo yafuatayo:
- Ugumba
- Kuwa na vinyweleo vingi usoni
- Kuwa na sura ya kiume
- Kuwa na mwili mkubwa au unene
- Matatizo Ya Tezi Ya Thyroid
Tezi ya thyroid inapokuwa na uwezo mdogo wa kufanya kazi, inaweza kusababisha kupata vipindi vya hedhi vyenye damu nyingi na kuongezeka kwa kiwango cha maumivu ya tumbo kama vichomi au chango. Unaweza pia kuhisi uchovu, kuhisi baridi na uzito wa mwili kuongezeka.
NUKUU: Kiwango kikubwa cha homoni ya thyroid ambacho huonekana kwenye tezi, kinaweza kusababisha vipindi vya hedhi kuwa vifupi na kutokwa na damu ya hedhi chache tu huenda kama matone kidogo kwa muda wa siku 1-2, halafu inapotea. Pia unaweza kuona dalili kama hizi zifuatazo:
- Uzito wa mwili kupungua ghafla
- Kuwa na mashaka au wasiwasi
- Mapigo ya moyo kwenda mbio
NUKUU: Kuvimba maeneo ya chini ya shingo yaweza kuwa ni dalili nyingine inayoonyesha matatizo ya tezi ya thyroid.
- Uvimbe Katika Mfuko Wa Kizazi(Uterine Fibroids)
Fibroid huwa ni uvimbe ambao huota kwenye kuta za mfuko wa uzazi. Vivimbe hivi vingi huwa sio saratani na vinaweza kutofautiana ukubwa kwani huanza kuota kama kijimbegu Fulani na huendelea kukua na kuzidi kuwa mkubwa.
Uvimbe wa fibroid unaweza kusababisha vipindi vyako vya hedhi kuwa vyenye maumivu sana na vyenye damu nyingi mno hata kukufanya ukaishiwa damu mwilini. Unaweza pia kupatwa na dalili kama hizi:
- Maumivu ya nyonga
- Maumivu ya kiuno
- Maumivu kwenye miguu
- Maumivu wakati wa tendo la ndoa
NUKUU: Vivimbe vingi vya fibroid vinahitaji matibabu ya haraka kabla havijakua sana.
- Ugonjwa Wa Endometriosis
Hii huwa ni hali ambapo tishu ambayo kwa kawaida hutanda juu ya mfuko wa kizazi(uterus), inapoota nje ya mfuko wa kizazi. Ugonjwa huu huathiri mwanamke 1 kati ya wanawake 10 walio katika umri wa kuzaa.
Wanawake wenye ugonjwa huu mara nyingi huwa wanahisi maumivu maeneo ya tumbo la chini, maumivu wakati wa hedhi, au maumivu wakati wa tendo la ndoa, kutokwa na damu nyingi sana wakati wa hedhi, kukosa hedhi kwa muda mrefu, kupata hedhi mara 2 ndani ya mwezi mmoja, na wanashindwa kupata ujauzito kwa urahisi.
Dalili zingine zinaweza kuwa kama ifuatavyo:
- Tumbo la chakula kuuma
- Maumivu makali wakati wa haja kubwa
- Maumivu makali wakati wa tendo la ndoa au baada ya tendo la ndoa
- Ugumba
NUKUU: Vipimo vinahitajika sana ili kugundua ugonjwa huu. Dalili za ugonjwa huu zinaweza kuondoka mara tu unapotumia dawa.
- Kuwa Na Mwili Mkubwa Au Mnene Sana
Unene unaonyesha kusababisha mzunguko wa hedhi kubadiri badirika. Utafiti unaonyesha kwamba, hali ya kuwa na uzito mkubwa au unene inapelekea kusababisha matatizo ya viwango vya homoni ambayo yanaweza kuingiliana na mzunguko wako wa hedhi.
NUKUU: Kuwa na uzito mkubwa kwa muda mfupi pia kunaweza kusababisha mzunguko wa hedhi kubadirika. Uzito mkubwa wa mwili na vipindi vya hedhi kubadirika ni ishara za matatizo ya vivimbe kwenye vifuko vya mayai, na yanapaswa yafanyiwe uchunguzi na daktari wako.
- Uzito Wa Mwili Kupungua Kwa Kasi Na Ulaji Mbaya
Kupotea kwa uzito kwa kasi sana kunaweza kusababisha vipindi vyako vya hedhi kusimama. Kutokutumia kalori nyingi za kutosha kunaweza kuingiliana na uzarishaji wa homoni zinazohitajika kwa ajili ya kupevusha yai.
NUKUU: Kiwango cha uzito wa mwili wako kupungua kinaweza kukadiriwa kuwa chini ya 18.5. Pamoja na kukoma kwa vipindi vya hedhi, pia unaweza kupatwa na dalili za uchovu wa mwili, kichwa kuuma na nywele kunyonyoka.
Nakushauri ufike hospitali endapo kama;
- Uzito wako wa mwili umepungua
- Una tatizo la kutokuhisi kula chakula
- Kufanya Mazoezi Kupita Kiasi
Mazoezi mazito nay a muda mrefu yanaonyesha kuingiliana na homoni zinazohusiana na mzunguko wa hedhi.
Kukimbia mbio za masafa marefu, na wanawake wanaohusika katika mazoezi hayo mara nyingi hupatwa na tatizo la kutokupata hedhi kabisa.
- Msongo Wa Mawazo
Utafiti unaonyesha kwamba msongo wa mawazo unaweza kuingiliana na mzunguko wako wa hedhi mara baada ya kuingilia sehemu ya ubongo inayoongoza homoni ambazo zinarekebisha mzunguko wako. Vipindi vyako vinapaswa kuerejea katika hali ya kawaida baada ya msongo wako wa mawazo kupungua.
- Matumizi Ya Madawa
Madawa fulani yanaweza kuingilia mzunguko wa hedhi, hasa;
- Madawa ya kuongeza homoni
- Madawa kwa ajili ya tezi ya thyroid
- Madawa ya vidonge kwa ajili ya ugonjwa wa kifafa
- Vidonge vya asprin na ibuprofen
NUKUU: Nakushauri muone daktari mapema ili aweze kukupatia ushauri.
- Salatani Ya Shingo Ya Kizazi
Saratani ya shingo ya kizazi inaweza kusababisha mabadiriko kwenye mzunguo wa hedhi, pamoja na kupata vipindi vya hedhi mara 2 ndani ya mwezi mmoja au kutokwa na damu nyingi sana ya hedhi. Kutokwa na damu wakati wa tendo la ndoa au baada ya kumaliza tendo la ndoa au kutokwa na uchafu mbaya ukeni ni ishara zingine na dalili za salatani.
Je, unahitaji huduma? Tupigie kwa namba hizi hapa: 0752389252 au 0712181626
Arusha-Mbauda
Karibuni sana.
Somo lenu lipo vizuri natamani ninifunze zaidi kupitia nyie
Jiunge na darasa letu tu katika mtandao wa telegram utapata masomo mengi