Sababu 4 Zinazofanya Uvimbe Kuota Kwenye Shingo Ya Kizazi

Uvimbe mdogo hutokeza kwenye shingo ya kizazi, ambao kitaalamu huitwa, “Cervical Polyp”. Uvimbe huu unaweza kusababisha kutokwa na damu ukeni. Daktari anaweza kupima na kugundua uvimbe huo. Kwa kawaida uvimbe huchunguzwa na kukatwa ili kufanyiwa vipimo. Katika namna nyingine, uvimbe unaoota na kuchomoza kwenye shingo ya kizazi huendelea kukua na hivyo kusababisha hali kuwa mbaya baadaye.

Uvimbe Kutokeza Kwenye Shingo Ya Kizazi Ni Nini?

Vivimbe vinavyoota kwenye shingo ya kizazi huwa ni vidogo, navyo huota juu ya shingo ya kizazi au sehemu ya uwazi wa shingo ya kizazi. Shingo ya kizazi huungana na mfuko wa uzazi(uterus) mpaka kwenye uke. Uvimbe unaochomoza na kutokeza kwenye shingo ya kizazi, mara chache huwa ni saratani; hata hivyo baadhi ya vivimbe hivi vidogo vidogo vinaweza kubadirika na kuwa saratani.

Aina Ya Vivimbe Vinavyoota Na Kuchomoza Kwenye Shingo Ya Kizazi

  •  Vivimbe vidogo vinavyoota kwenye tabaka la juu la shingo ya kizazi(Ectocervical polyps)
  •  Vivimbe vidogo ambavyo huota ndani ya uwazi wa shingo ya kizazi(Endocervical polyps)

Je, Dalili Zake Zinakuwaje?

Watu wengi huwa hawana dalili za uvimbe unaotokeza kwenye shingo ya kizazi. Lakini ikiwa kama una dalili, basi unaweza kuziona kama hizi zifuatazo:

  • Kutokwa na damu ukeni nyingi kwa muda mrefu
  •  Kutokwa na damu ukeni baada ya kushiriki tendo la ndoa
  • Kutokwa na damu ukeni hata baada ya hedhi au unapofikia umri wa kukoma hedhi
  • Kutokwa na uchafu ukeni wenye harufu mbaya, wenye rangi kama usaha au wenye rangi ya njano.

Je, Uvimbe Unaoota Kwenye Shingo Ya Kizazi Huwa Na Muonekano Gani?

Vivimbe vingi huota na kurefuka, na kuwa na umbo kama tawi ambalo huchomoza na kutokeza nje ya shingo ya kziazi. Huwa ni vivimbe vilaini au vyenye kubonyea kama sponji, na vyenye rangi ya wekundu,  pinki kidogo au weupe wa ukijivu. Baadhi ya vivimbe hivi huwa na shina refu na vinaweza kuzidi kukua. Vinaweza kuvuja damu pale unapovigusa.

Je, Nini Husababisha Vivimbe Hivi?

Wanawake wengi huwa na tatizo hili ambalo huwasumbua kwa muda mrefu, nao hushindwa kutambua nini visababishi vyake. Lakini vyanzo vya vivimbe hivi huwa ni hivi vifuatavyo:

  • Uvimbe wa muda mrefu kwenye shingo ya kizazi
  • Maambukizi ya magonjwa ya zinaa
  • Maambukizi ya fangasi ukeni
  • Maambukizi katika via vya uzazi au PID

NUKUU: Pia unaweza kufungua Link hizo hapo chini ili ujue zaidi:

  1. Haya Ndio Mambo 6 Yanayomfanya Mwanamke Kupatwa Na Tatizo La PID
  2. Mambo 4 Unayoweza Kuyakosea Katika Kutambua Maambukizi Ya Fangasi Ukeni.

Je, Madhara Yake Ni Nini?

Vivimbe au uvimbe unapoota kwenye shingo ya kizazi unapozidi kukua na kusababisha kutokwa na damu ukeni kwa mfululizo kwa muda mrefu, husababisha mwanamke kushindwa kubeba ujauzito. Pia humfanya mwanamke kukosa hamu ya tendo la ndoa kutokana na mvurugiko wa homoni.

Je, Suluhisho Lake Ni Nini?

James Herbal Clinic tunazo dawa nzuri zenye uwezo mkubwa wa kuzuia uvimbe usiendelee na hivyo kukomeza dalili na vyanzo vya ugonjwa huu. Pia unaweza kutuma namba yako ya whatsAp tukuunganishe na darasa letu.

Je, unahitaji huduma? Basi wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626.

Arusha-Mbauda,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *