TOFAUTI KATI YA UCHAFU WA KAWAIDA NA USIO WA KAWAIDA UTOKAO UKENI.

Baadhi ya uchafu utokao ukeni huwa ni ishara ya kuonyesha afya ya uke wako. Je, unafahamu tofauti iliyopo kati ya uchafu wa kawaida na usio wa kawaida utokao ukeni?  Kutokwa na uchafu ukeni ni sehemu ya asili ya kuwa mwanamke, lakini wakati mwingine mabadiriko ndani yake yanaweza kuonyesha tatizo fulani.

Matokeo ya picha ya images of women affected by PID

Sasa hebu tuangalie aina tofauti za uchafu unaotoka ukeni ili kwamba uweze kujua kwamba ni muda gani uchafu wako unakuwa sio wa kawaida.

 

 

  1. Uchafu Wa Asili Unaotoka Ukeni

 

 

Kazi kubwa ya uke wako ni kutoa uchafu unaokuwa kwenye mfuko wa uzazi pamoja na viungo vyote vya mfumo wa uzazi. Asidi ya asili inayokuwa kwenye uke wako hufanya kazi ya kuzuia maambukizi na husababishwa bakteria wazuri wa asili wanaokuwa ukeni mwako.

Matokeo ya picha ya image of white dicharges

NUKUU: Katika siku ya kawaida uke wako hujisafisha wenyewe kwa kutoa uteute msafi mweupe wenye utelezi. Uwiano wa asili wa uke unaweza kuharibiwa na kitu chochote kinachoingizwa ndani ukeni.

 

  1. Uchafu Wa Kawaida

 

 

Kwanza, yafaa vyema kuelewa kwamba wanawake wote hutokwa na uchafu ukeni. Tezi ndani ya uke wako au mlango wa kizazi hutoa kiwango kidogo cha uteute ambao hutiririka nje ya mwili wako kila siku, huku ukiwa umebeba seli zilizozeeka.

Uchafu wa kawaida ukeni mwako husaidia kusafisha uke, pamoja na kuufanya uwe laini na usiwe na maambukizi wala vimelea wengine. Uke unakuwa hauna harufu mbaya hata kidogo. Uchafu wa kawaida ukeni mara nyingi huonekana msafi au kama maziwa vile pale unapokauka juu ya chupi yako au nguo ya ndani.

Matokeo ya picha ya image of egg like dicharges

Mara nyingi unaweza kuona uchafu ambao ni mzito wenye kuvutika kama kamba kamba vile. Unaweza ukauita mweupe msafi na wenye kuteleza kama kamasi vile.

 

Mambo ambayo yanaweza kutoa uwiano sawa wa asidi ya asili ukeni na kupelekea kuwapo kwa maambukizi, ni pamoja na;

 

  • Kutia vitu vibaya ukeni kama vile asali, pipi kifua, maji ya limao, nk
  • Kuoshea maji ya ukoko
  • Kuoshea vitu vyenye marashi makali ukeni
  • Ujauizito
  • Kisukari
  • 1.     Kipindi Cha Hedhi Huathiri Uchafu Utokao Ukeni

 

 

 

  • Mzunguko wako wa hedhi una kazi kubwa katika aina ya uchafu unaotoka ukeni unauona katika mzunguko wa mwezi mzima. Takribani ya nusu kati ya vipindi vya hedhi, utaona muongezeko wa uchafu wa kawaida ambao unakuwa mweupe kama ute wa yai la kuku. Hali hii huongeza unyevunyevu na uchafu unaoashiria yai kupevuka. Huu ni wakati wa siku za hatari na unaweza ukapata ujauzito.

Matokeo ya picha ya image of egg like dichargesJe, unafahamu kwamba unaweza kupatwa maambukizi kwa urahisi sana kabla au wakati wa ujauzito? Hii ni kwasababu ya uwiano wa kawaida wa asidi ya asili ukeni kutofautiana wakati wa mzunguko wako wa hedhi, na kusababisha kiwango cha asidi kushuka chini siku chache kabla na wakati wa hedhi.

 

1.     Dalili Za Uchafu Usio Wa Kawaida

 

 

Ni muhimu sana kutambua ishara za uchafu usio wa kawaida utokao ukeni kwasababu inaweza kuwa ishara ya maambukizi au magonjwa mengine katika mwili wako. Unapoona hali ya kutokwa na uchafu ukeni ambao unatoka na kuongezeka ghafla, basi hii inaweza kuwa ni ishara ya tatizo. Badiriko jingine ambalo linaweza kuashiria tatizo ni uchafu ambao ni wenye rangi ya njano yenye kung’aa au wenye rangi ya ukijani.

Matokeo ya picha ya image of white dicharge on the underwearNUKUU: Uchafu mzito wa mabonge bonge au kila uchafu wa majimaji unaweza pia kuashiria kwamba kuna kitu kinakosekana ukeni mwako.

Baadhi ya dalili zinazoweza kuashiria maambukizi ni pamoja na;

  • Mabadiriko katika rangi, mnato kama maziwa ya mgando
  • Muwasho, au kutojisikia vizuri sehemu za uke
  • Uke kuwa na hali ya kuwaka moto wakati wa kukojoa
  • Kutokwa na damu hata kama sio kipindi cha hedhi
  • Harufu kali ikiambatana na uchafu wenye rangi ya njano, ukijani, au kijivu mweupe.
  • Kama unatokwa na uchafu ukeni pamoja na ishara nilizozitaja hapo awali, basi unapaswa ufike hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi na matibabu.

Je, Ni Aina Gani Tofauti Za Uchafu Zinazoashiria?
·        Ikiwa kama uchafu wako ni mweupe na mzito na wenye mabonge na una muwasho ukeni au hali ya kuwaka moto, basi hii inaashiria kabisa kuwa una maambukizi ya fangasi sehemu za siri
·        Kama una uchafu ambao ni mwingi kuliko kawaida, ambao ni wenye majimaji na wenye rangi ya  kijivu na wenye harufu mbaya kama shombo la samaki, hii inaashiria kuwa una bakteria ukeni.
·        Kama unatokwa na uchafu ukeni ambao huongezeka ghafla katika kiwango, ambao ni wa kijani au njano ambao una harufu mbaya, au unasababisha dalili za ukeni, basi unapaswa kufika hospitali na kumuona daktari ili kuweza kupima na kujua chanzo ili kupata matibabu.

 

1.     Maambukizi Ya Kawaida Ukeni

 

 

Visababishi vya kawaida vya uchafu usio wa kawaida ukeni ni pamoja na;

 

·        Malengelenge(Trichomoniasis)

 

·        Pangusa(Chlamydia)

 

 

·        Kisonono(Gonorrhea)

 

·        Kusahau kuondoa ped ukeni

 

 

·        Maambukizi mengine ya zinaa

 

·        Fangasi sehemu za siri

 

 

·        Bakteria ukeni

 

Asanteni sana ndugu wapendwa kwa kusoma makala hii, napenda niishie hapa tutaonana kipindi kingine….

 

Je, unahitaji huduma kutoka James Herbal Clinic? Tupigie kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626

 

Arusha-Mbauda

 

Karibuni sana!

One thought on “TOFAUTI KATI YA UCHAFU WA KAWAIDA NA USIO WA KAWAIDA UTOKAO UKENI.

  1. Habari dokta, me natokwa na ute wa rangi ya njano mzito na hauna harufu sema tu nawashwa ila sio sana sasa sijui ni shida, halafu naomba uni add kwenye group whats up 0755921889

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *