Uchafu Mweupe Unaotoka Ukeni; Je, Ni Muda Gani Hubadirika Na Kuwa Sio Wa Kawaida (Mbaya)?

Ndugu mpendwa, je umewahi kutokwa na uchafu mweupe ukeni muda mrefu na ukaweza kuhisi kuwa unaweza kubadirika na kuwa sio wa kawaida? Basi katika makala hii utaweza kujifunza na kuelewa kutokwa na uchafu mweupe ukeni kunamaanisha nini, na je nini kisababishi chake na ni kipindi gani uchafu huu unakuwa sio wa  kawaida.

Na ieleweke kuwa kila mwanamke katika umri wake wa kuzaa inampasa kuwa na mabadiriko katika mzunguko wake wa hedhi. Kutambua kuwa uchafu ni wa kawaida na jinsi gani homoni huathiri hali ya utokaji wa uchafu wako, ni jambo muhimu sana kulifahamu.

Je, Uchafu Mweupe Unaotoka Ukeni Unakuwaje?

Uchafu mweupe wa kawaida unaotoka ukeni hutengenezwa na seli za ukeni, bakteria wa asili, pamoja na ute utelezi kutoka kwenye shingo au mlango wa kizazi. Uchafu huu unaweza ukawa na rangi tofauti. Unaweza ukawa mweupe na mzito au mwepesi kama majimaji. Pia baadhi ya wanawake wanaweza kutokwa na uchafu wenye rangi ya njano au kahawia.

Uchafu utokao ukeni ni njia moja wapo rahisi ya kuufanya uke wako kuwa msafi ili  kuufanya usiweze kushambuliwa na maambukizi. Wanawake wanapenda kuwa na mazoea ya kutumia marashi au sabuni zenye harufu kali ili kuoshea sehemu za uke na kusababisha kuharibu kabisa utendaji kazi huu wa asili unaohusika katika kutoa uchafu nje ya uke.

Discharge Woman Royalty-Free Images, Stock Photos & Pictures | Shutterstock

NUKUU: Kuwepo kwa hali ya kutokwa na uchafu mweupe usiokuwa na harufu yoyote, wala vichomi ni hali ya kawaida kabisa. Pia uchafu mweupe unaotoka ukeni unaweza ukabadirika kuwa wa njano ikiwa kama utapigwa hewa muda mrefu.

Je, Ni Jinsi Gani Mzunguko Wako Wa Hedhi Unaweza Kuathiri Hali Yako Ya Kutokwa Na Uchafu Mweupe Ukeni?

Mzunguko wa hedhi hufanyika kati ya vipindi 2. Siku ya kwanza ya mzunguko wa hedhi ndio siku ya kuanza hedhi. Wanawake wenye siku za mzunguko wa kawaida wa siku 28, hali yao ya upevushaji mayai huanza kati ya siku 12-16. Upevushaji mayai ni njia inayotumika ili kulitoa yai kwenye kijifuko cha yai. Unaweza ukaziona dalili  za upevushaji kuwa zikifanyika kwa kuona ishara kama vile matiti kuuma, maumivu chini ya tumbo, nk.

Kabla ya upevushaji, kiwango cha homoni ya estrogen hupanda juu. Hivyo basi, kiwango cha homoni ya estrogen kinapokuwa juu husababisha shingo ya kizazi kutoa utoko au uchafu mweupe wenye kuteleza kama ute wa yai la kuku. Hali hii hujitokeza kabla ya kupevusha na kusaidia mwendo wa shahawa au mbegu ziweze kufika na kurutubisha yai la mwanamke. Ili kuweza kutambua jambo hili, unaweza kuingiza kidole au vidole vyako ukeni vikiwa visafi na ukachovya tu ili kuona muonekano wa utoko au uchafu unaotoka kule. Ikiwa kama ni wa kuteleza na wenye rangi nyeupe kama ute wa yai la kuku, basi, hicho ndicho chaweza kuwa kipindi chako cha upevushaji yai lako.

NUKUU: Baada ya upevushaji, huwa kuna muongezeko wa homoni ya progesterone. Hali hii husababisha kutokwa na uchafu mweupe mzito kabla ya kipindi cha hedhi kuwadia. Upana wa kipindi chako sio mbaya.

Je, Uchafu Unaokuwa Sio Wa Kawaida Unakuwaje?

Utoko au uchafu unaotoka ukeni kwa kawaida huwa ni mweupe, wakati mwingine huwa wa kahawia. Unaweza ukawa wa majimaji au mzito wakati wa mzunguko wako wa hedhi. Hata hivyo, kuwepo kwa harufu mbaya kwenye utoko au uchafu unaotoka ukeni ni hali ambayo sio ya kawaida. Endapo kama uchafu wako utakuwa sio wa kawaida, zipo dalili utakazoziona kama vile:

  • Homa
  • Muwasho sehemu za uke
  • Harufu mbaya kama shombo la samaki
  • Uchafu wenye rangi ya njano kama usaha vile

50+ Black Woman Pelvic Pain Stock Photos, Pictures & Royalty-Free Images - iStock

NUKUU: Endapo kama utaona aina hii ya uchafu ukikutoka ukeni, basi tambua kuwa sio wa kawaida ni mbaya kabisa. Inakupasa ufike hospitali yoyote ya wilaya au mkoa ili kufanya uchunguzi wa vipimo haraka.

Je, Nini Vinasababisha Kutokwa Na Uchafu Ukeni?

  1. Kusafisha Au Kupiga Bomba Ukeni

Hii ni kutumia njia ya kupiga bomba au kuosha kwa maji ukeni. Hali hii inaweza kuharibu muonekano wa asili wa uke kwa mwanamke. Katika uke kuna bakteria wazuri na wabaya pia. Bakteria wazuri ni wale wanaolinda uke wanaitwa Lactobaillus. Kumbuka kuwa unapoosha uke wako kwa njia kama hiyo unauathiri pia unasababisha bakteria wabaya kuongezeka. Hali hii inaweza kusababisha bakteria ukeni(Bacterial Vaginosis) kwa wanawake na kutokwa na uchafu mweupe ukeni kama cream.

  1. Kupaka Madawa Makali Sehemu Za Uke

Madawa ya antibiotics wanayotumia baadhi ya wanawake kupaka sehemu za uke ili kutibu maambukizi, mara nyingi husababisha madhara sehemu hizo. Madawa haya huua bakteria wazuri wa asili pamoja na wabaya. Hali hii husababisha kuota kwa bakteria wa fangasi kwakuwa madawa haya huwa hayaui vimelea wa fangasi, wala hayaondoi tatizo la fangasi maeneo hayo. NUKUU: Uchafu utokao ukeni kwasababu ya fangasi kwa kawaida huwa mweupe mzito kama maziwa mgando wala hauna harufu. Inapokuwapo hali kama hii, wanawake huweza kupatwa na muwasho pamoja na maumivu makali wakati wa kukojoa.

  1. Upevushaji

Kabla na baada ya upevushaji, uchafu au utoko unaotoka ukeni huwa msafi mweupe tena wenye kulendemka kama ute wa yai la kuku.

  1. Kujamiiana

Wakati wa kujamiiana, huwa kuna muongezeko wa kiwango cha utoko mweupe kwa wanawake. Hii husaidia mbegu za mwaname kusafiri bila kizuizi chochote njiani na hulainisha uke ili kumfanya mwanaume au mwanamke kujisikia raha wakati wa tendo la ndoa.

  1. Ujauzito

Wanawake wengi wanapokuwa wajawazito mara nyingi hutokwa na utoko au uchafu mweupe ukeni. Uchafu au utoko huonekana kuwa mweupe tena msafi.

Je, Uchafu Mbaya Unaomtoka Mwanamke Unawezaje Kutibiwa?

Ikiwa kama utaona unatokwa na uchafu mweupe mzito kama maziwa mtindi, basi, tambua kuwa hayo ni maambukizi. Yafaa sana ukafika hospitali mapema ili kufanya uchunguzi wa vipimo. James Herbal Clinic tuna dawa nzuri za asili zenye uwezo mkubwa wa kuondoa tatizo hilo.

Pia unaweza kutuma namba yako ya WHATSAP tukakuunganisha na darasa letu la masomo ya afya.

Je, unahitaji huduma? Basi, wasiliana nasi kwa namba hizi: 0768 559 670/0712 181 626,

Arusha-Mbauda,

Karibu sana!

 

2 thoughts on “Uchafu Mweupe Unaotoka Ukeni; Je, Ni Muda Gani Hubadirika Na Kuwa Sio Wa Kawaida (Mbaya)?

  1. Je kipindi mwanamke ndo anatokwa na ute je ni sahihi kushiriki tendo?

    Na ni wakati gani sahihi kushiriki tendo kama nna hitaji mtoto?

    1. Kipindi kizuri kushiriki tendo la ndoa ni pale anapokuwa katika siku zake za hatari.
      Lakini pia unapohitaji kushiriki kama umemuandaa unaweza kushiriki bila tatizo kabisa ila usifanye hivyo wakati akiwa katika hedhi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *