Kutokwa damu kwa muda mrefu kitaalamu tunaita, “Menorrhagia” yaani kutokwa na damu nyingi ya hedhi kwa muda mrefu au kutokwa na damu mfululizo bila kukoma. Ingawa kutokwa na damu nyingi ya hedhi ni jambo la kawaida, lakini wanawake wengi msikubali kutokwa na damu nyingi mpaka kufikia hali ya kuishiwa na damu mwilini.
NUKUU: Unapokuwa na hali ya kutokwa na damu nyingi ya hedhi, kumbuka kwamba huwezi kufanya shughuli zako kwa amani hasa unapokuwa hedhini kwasababu unapoteza damu nyingi na kupatwa na hali ya vichomi tumboni. Kama ukihofia hedhi yako kwakuwa una hali hiyo ya kutokwa na damu nyingi ya hedhi, basi nakushauri ufike hospitali bila kuchelewa. Yapo matibabu mengi juu ya tatizo hili la kutokwa na damu nyingi ya hedhi.
Je, Dalili Zake Zinakuwaje?
Dalili na viashiria vya kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi huwa kama ifuatavyo:
- Pedi kulowana haraka zaidi kila baada ya lisaa limoja
- Uhitaji wa kuweka hata pedi 2 kwa mara moja
- Uhitaji wa kuamka usiku ili kubadiri pedi tena
- Kutokwa na damu muda mrefu zaidi ya wiki
- Kutokwa na mabonge ya damu makubwa
- Kuzuia shughuli zako za kila siku kwasababu ya kutokwa na damu nyingi
- Dalili za kuishiwa damu kama vile mwili kuchoka, au kupungukiwa pumzi
Je, Unaweza Kufika Hospitali Kipindi Gani?
Unaweza kutafuta msaada wa huduma ya matibabu kabla hujafanya vipimo ikiwa kama utaona dalili hizi:
- Kutoka nyingi sana na kulowanisha pedi ndani ya lisaa limoja
- Kutokwa na damu ya hedhi mara 2 ndani ya mwezi mmoja
- Kutokwa na damu ya hedhi mfululizo bila kukoma
- Kutokwa na damu ikiwa kama ulishawahi kukoma hedhi
Je, Nini Husababisha Hali Hii?
Zipo sababu mbalimbali zinazopelekea kuwepo kwa hali hii nazo ni kama ifuatavyo;
- Kutokuwa Na Uwiano Sawa Wa Homoni(Hormonal Imbalance)
Katika mzunguko wa hedhi wa kawaida, uwiano kati ya homoni ya estrogeni na progesterone inasimamia kujenga ukuta au ngozi laini ya tumbo la uzazi(endometrium), ambayo ndiyohubanduka wakati wa hedhi. Kama hali ya kutokuwa na uwiano sawa wa homoni ikitokea, basi ngozi laini ya ukuta wa kizazi inaendelea kuwa kubwa au nene zaidi kupita kiasi na mwishowe hubanduka na kumwagwa kwa njia ya kutokwa na damu nzito ya hedhi.
NUKUU: Magonjwa yanayoweza kusababisha kutokuwa na uwiano sawa wa homoni(hormonal imbalance) ni pamoja na vivimbe vidogovidogo kwenye vifuko vya mayai(polycystic ovarian syndrome), unene, kisukari au matatizo ya thyroid.
- Vifuko Vya Mayai Kutokufanya Kazi
Kama vifuko vyako vya mayai havitoi mayai(yaani havipevushi mayai) wakati wa mzunguko wa hedhi, basi mwili wako hauwezi kutengeneza homoni ya progesterone, kama inavyokuwa wakati wa mzunguko wa kawaida wa hedhi. Hali hii hupelekea kuwepo kwa hali ya kutokuwa na uwiano sawa wa homoni na inaweza kusababisha kutokwa na damu nzito, nyingi ya hedhi.
- Uvimbe Wa Fibroid
Uvimbe huu ambao sio salatani kwenye tumbo la uzazi huonekana katika umri wako wa kuzaa. Uvimbe kwenye kizazi unaweza kusababisha kutokwa na damu nyingi ya hedhi au inaweza ikatoka kwa muda mrefu sana kwa mfululizo bila kukoma ikiwa kama tatizo hili halitatibiwa na kuondoka mwilini mwako.
- Adenomyosis
Hali hii hutokea pale tezi kwenye ukuta wa tumbo la uzazi zinapoingizwa ndani ya msuli wa tumbo la uzazi, na mara nyingi husababisha kutokwa na damu nyingi ya hedhi na maumivu makali sana ya tumbo wakati wa hedhi.
- Shida Za Ujauzito
Hali ya kutokwa na damu nyingi nzito ya hedhi, inaweza kutokana na mimba kuharibika. Chanzo kingine cha kutokwa na damu nyingi wakati wa uajuzito ni pamoja na eneo lisilo la kawaida la kondo(placenta), kama vile kondo kushuka chini au kukaribia kwenye shingo ya kizazi.
- Salatani Ya Kizazi
Salani ya kizazi na salatani ya shongo ya kizazi vinaweza kusababisha kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi, hasa kama unakaribia umri wa kukoma hedhi.
Je, Vihatarishi Vinakuwaje?
Vihatarishi hutofautiana kulingana na umri ikiwa kama una magonjwa mengine ambayo yanaweza kuelezea hali yako ya kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi. Katika mzunguko wa kawaida, kuachiliwa kwa yai kwenye vifuko vya mayai huamsha uzarishaji wa homoni ya progesterone mwilini mwako, homoni ya mwanamke ambayo inashughulika sana katika kufanya vipindi vya hedhi visiwe vya kubadirika. Kama yai lisipotolewa, basi homoni pungufu ya progesterone inaweza kusababisha kutokwa na damu nyingi sana ya hedhi.
Hali ya kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi kwa wasichana walio katika umri wa ujana hutokana na kutokupevushwa kwa yai. Wasichana mabinti hasa hupatwa na hali hii katika mwaka wa kwanza baada ya kipindi chao cha kwanza cha hedhi.
Hali ya kutokwa damu nyingi ya hedhi ukiwa katika umri mkubwa hutokana na uvimbe tumboni, hasa fibroid, na vivimbe vya tishu ndani ya msuli wa ukuta wa uzazi. Hata hivyo matatizo mengine kama vile salatani ya kizazi, matatizo ya kutokwa na damu, madhara ya matumizi ya madawa na ugonjwa wa ini au figo yanaweza kuchangia hali hii.
Je, Madhara Yake Yanakuwaje?
Hali ya kutokwa na damu nyingi tena kwa muda mrefu wakati wa hedhi inaweza kusababisha madhara haya yafuatayo:
- Kuishiwa Damu Mwilini
Hali ya kutokwa na damu nyingi ya hedhi kwa muda mrefu inaweza kusababisha kupungukiwa damu mwilini kwa kupunguza kiwango au idadi ya mzunguko wa chembe nyekundu za damu. Idadi ya chembe nyekundu za damu zinazozunguka hupimwa kwa hemoglobin, ambayo ni protini inayosaidia chembe hai nyekundu za damu kubeba hewa ya oksijeni na kuipeleka kwenye tishu za mwili wako.
Upungufu wa madini ya chuma hutokea kadiri mwili wako unavyojaribu kujirekebisha upya kwa ajili ya chembe hai nyekundu zilizopotea kwa kutumia hifadhi yako ya madini ya chuma ili kutengeneza protini nyingi zaidi za hemoglobin, ambazo zinaweza kubeba oksijeni kwenye chembe hai nyekundu za damu. Hali ya kutokwa na damu nyingi hedhini inaweza kupunguza viwango vya madini ya chuma ya kutosha ili kuongeza vihatarishi vya kupungua kwa madini ya chuma na kusababisha kupungukiwa damu mwilini.
Dalili na viashiria ni pamoja na ngozi kuwa nyeupe, mwili kuchoka sana kuishiwa nguvu. Ingawa lishe huwajibika sana katika janga hili la kupungukiwa madini ya chuma, lakini tatizo huwa ni tatanishi pale damu inapotoka nyingi wakati wa vipindi vya hedhi.
Nipende kuishia hapa ndugu mpendwa msomaji kwa makala yetu ya leo.
James Herbal Clinic pia tunatoa vipindi vyetu endelevu kila siku kwa njia ya mtandao wa TELEGRAM na WHATSSAP. Hivyo unaweza kutuma namba yako ukaweza kuunganisha na darasa letu.
Ikiwa kama unahitaji huduma, basi tupigie kwa namba hizi; 0752389252 au 0712181626.
Arusha Mbauda,
Karibuni Sana.
Naomb kuunganishwa somo zuri 0758039530 whtsph