Ugonjwa wa mshipa wa nyonga huwa ni maumivu ambayo hupenya na kuingia kwenye mshipa wa nyonga, ambao hugawanyika kutoka kiunoni na kushuka kwenye mapaja na matako kuelekea chini kwenye mguu. Kwa kawaida ugonjwa wa nyonga huathiri sehemu moja tu ya mwili wako.
Ugonjwa wa nyonga mara nyingi hutokea pale pingili ya mgongo inapogandamiza sehemu ya mshipa wa fahamu. Hali hii husababisha uvimbe, maumvu na mara nyingi huwa kunakuwa na hali ya kufa ganzi katika mguu ulioathirika.
NUKUU: Ingawa maumivu yanayoambatana na ugonjwa wa nyonga yanaweza kuwa makali, lakini bado ugonjwa huu unaweza kutibiwa pasipo oparesheni ndani ya wiki chache tu. Watu wenye maumivu makali ya nyonga yanayoambatana na madhaifu ya mguu au kukosa choo au mabadiriko kwenye kibofu kunaweza kupelekea kufanyiwa upasuaji.
Je, Dalili Zake Zinakuwaje?
Maumivu yanayopenya kwenye kiuno na kushuka na kuelekea kwenye tako na kushuka chini mpaka nyuma ya mguu, huwa ni dalili ya ugonjwa wa mshipa wa nyonga. Unaweza usijisikie vizuri popote kule unapopitia mshipa wa fahamu, lakini inafaa kufuata mshipa unakopita kutoka kiunoni, matakoni na nyuma ya mguu wako na kisigino.
Maumivu yanaweza kutofautiana sana, yanaweza kuwa ya kawaida au makali, au kuhisi kama kitu kinachoma kama moto. Wakati mwingine inaweza kuonekana kama mshituko wa umeme. Inaweza kuwa hali mbaya unapokohoa au kupiga chafya, au kukaa kwa muda mrefu nako kunaweza kuongeza dalili kuwa mbaya zaidi. Kwa kawaida sehemu moja ya mwili wako huathiriwa.
NUKUU: Baadhi ya watu pia wana hali ya misuli kufa ganzi au kukaza katika maeneo yao ya mguu ulioathirika. Unaweza ukapatwa na maumivu katika sehemu moja ya mguu na kufa ganzi katika eneo jingine la mguu wako.
Je, Ni Kipindi Gani Unapaswa Ufike Hospitali Ili Uonane Na Daktari?
Maumivu ya kati ya ugonjwa wa mshipa wa nyonga mara nyingi hutoweka kwa muda tu. Fika hospitali haraka ikiwa kama maumivu yamezidi kuwa makali zaidi ya wiki moja, au kama hali inaendelea kuwa mbaya zaidi. Pata matibabu haraka ikiwa kama;
- Unakosa choo kwa muda mrefu
- Una maumivu makali ya ghafla kiunoni au mguu kufa ganzi au msuli kudhoofika
Je, Nini Husababisha Tatizo Hili?
Ugonjwa wa nyonga hutokea pale mshipa wa nyonga unapobanwa sana na pingiri ya uti wa mgongo. Ni mara chache sana mshipa wa fahamu unaweza kubanwa na uvimbe au kuharibiwa na ugonjwa kama vile kisukari.
Mambo hatarishi ya ugonjwa wa nyonga ni kama ifuatavyo;
- Umri kuwa mkubwa
- Uzito wa mwili kuwa mkubwa
- Kubeba mizigo mizito au kufanya kazi nzito ya kujigeuza mara kwa mara
- Kukaa muda mrefu
- Ugonjwa wa kisukari
Je, Madhara Yake Yanakuwaje?
Ingawa watu wengi hupona kabisa daima ugonjwa wa mshipa wa nyonga, lakini mara nyingi bila matibabu, ugonjwa huu unaweza kusababisha uharibifu wa kudumu wa mshipa wa nyonga. Jitahidi kutafuta matibabu kwa haraka bila kuchelewa ikiwa kama;
- Unahisi mguu kufa ganzi
- Unahisi kukosa choo kwa muda mrefu
- Unahisi mguu au paja kuuma
Je, Unahitaji Huduma Ili Kuondoa Tatizo Hili?
James Herba Clinic tuna dawa nzuri kabisa zenye uwezo mkubwa wa kuponya tatizo hili nazo ni NEOTONIC na FRESH HERB.
Kwa mawasiliano naomba utupigie kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626.
Pia kama unahitaji kujifunza zaidi katika darasa letu unaweza ukatuma namba zako za WHATSAP au TELEGRAM ukaunganishwa na JUKWAA(GROUP) letu au ukabonyeza link yetu ya telegram hii: t.me/jamesherbalclinic.
Karibuni sana!