VIJUE VYANZO VYA HOMA YA MANJANO, DALILI ZAKE, MADHARA YAKE NA TIBA ZAKE.

Homa ya manjano ni hali ambayo ngozi, weupe wa macho(sclera) Pamoja na membreni hubadirika na kuwa za njano. Rangi hii ya njano husababishwa na kiwango kikubwa cha bilirubin, nyongo yenye rangi ya njano machungwa. Nyongo ni uteute unaotengenezwa n aini. Bilirubin hutengenezwa mmeng’enyo wa chembe nyekundu za damu.

Homa ya manjano inaweza kusababishwa na tatizo katika kila hatua tatu katika uzarishaji wa bilirubin.  Kabla ya uzarishaji wa bilirubin, unaweza ukapata kile kinachoitwa homa ya manjano kubwa kutokana na muongezeko wa bilirubin uliosababishwa na:

  • Kurudia kunyonya kiwango kikubwa cha mkusanyiko wa damu iliyoganda chini ya ngozi(hematoma)
  • Chembe za damu huharibiwa na kuondolewa kwenye mkondo wa damu kabla ya mzunguko wake wa Maisha haujaisha(hemolytic anemias)

Wakati wa uzarishaji wa bilirubin, homa ya manjano inaweza kusababishwa na:

  • Virusi, hasa Hepatitis A, Hepatitis B na C ya muda mrefu, na maambukizi ya virusi vya Epstein-Barr.
  • Pombe
  • Matatizo yak inga ya mwili
  • Madawa hasa penicillins, chlorpromazine na estrogenic au anabolic steroids

Baada yay a bilirubin kutengenezwa, homa ya manjano inaweza kusababishwa na kupasuka kwa mrija wa nyongo kutokana na:

  • Mawe kwenye figo
  • Kuvimba kwa kibofu cha nyongo
  • Saratani ya kibofu cha nyongo
  • Kuvimba kwa kongosho

Je, Dalili Zake Zinakuwaje?

Wakati mwingine, mtu anaweza asiwe na dalili za homa ya manjano, na hali inaweza kupatwa kwa ajali. Dalili mbaya inaweza kutegemeana na sababu mbalimbali na ugonjwa unavyoweza kupatikana kwa haraka au polepole.

Ikiwa kama umepatwa ugonjwa wa manjano kwa njia ya maambukizi, basi unaweza ukawa na dalili zifuatazo:

  • Homa
  • Baridi
  • Maumivu yatumbo
  • Dalili kama mafua
  • Badiriko kwenye rangi ya Ngozi
  • Mkojo mweusi au kinyesi chenye rangi ya kijivu kwa mbali

Kama ugonjwa wa homa ya manjano haukusababsihwa na maambukizi, unaweza ukawa na dalili kama vile uzito wa mwili kupungua au muwasho wa Ngozi. Kama homa ya manjano inasababishwa na saratani ya mrija wa kongosho, basi dalili ya kawaida huwa ni maumivu ya tumbo la chini. Wakati mwingine, unaweza kupatwa na homa ya manjano kutokana na ugonjwa w aini ikiwa kama una:

  • Uvimbe w aini
  • Ugonjwa wa Ngozi
  • Ugonjwa sugu wa hepatitis A, B, au C
  • Uvimbe wa maungio ya mifupa(polyarthralgias)

Je, Ugonjwa Wa Homa Ya Manjano Unapimwaje?

Unapofika hospitali, madaktari hupima homa ya manjano kwa kuchunguza dalili za ugonjwa w aini kama vile:

  • Michubuko ya Ngozi
  • Mkusanyiko wa mishipa midogo yad amu karibu na uso wa Ngozi
  • Viganja na ncha za vidole kuwa na rangi nyekundu

Vipimo vya mkojo ambavyo huwa chanya kutokana na bilirubin kuonyesha kwamba mgonjwa ana homa ya manjano. Utafiti wa kipimo cha mkojo unapaswa kuthibitishwa kwa kipimo cha damu. Kipimo cha damu kitaambatana na kipimo kamili cha dam una viwango kamili vya bilirubin.

Daktari wako pia atafanya kipimo ili kubaini ukubwa na ugumu wa ini lako. Dakatari anaweza kutumia kipimo cha ultrasonography na kompyuta ya tomographic(CT) scanning Pamoja na biopsy kwa ajili y aini(yaani anachukua sampuli ya ini) kwa ajili ya uthibitisho Zaidi.

Ndugu msomaji napenda kuishia hapa katika makala hii nikaribishe kipindi cha maswali na maoni yako, karibu sana.

Pia unaweza kutuma namba yako ya WHATsAP utaunganishwa na darasa letu ili upate masomo mbalimbali ya magonjwa.

Je, Unahitaji Huduma?

 

Basi unaweza kuwasiliana nasi kupitia namba hizi; 0752389252 au 0712181626,

Arusha-Mbauda,

Karibuni sana!

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *