Fahamu Sababu 7 Zinazomfanya Mwanamke Kutokwa Na Damu Nyingi Wakati Wa Hedhi.

Kutokwa na mabonge ya damu wakati wa hedhi mara nyingi huwa ni tukio la kawaida wakati unapotokwa na damu nyingi wakati wa hedhi. Kwakweli, wanawake wengi hutokwa na damu yenye mabonge wakati Fulani katika Maisha yao, kutokwa na damu nyingi na mabonge yad amu kupita yanaweza wakati mwingine kuwa sababu inayoweza kumtia wasiwasi.

Je, mabonge makubwa ya damu wakati wa hedhi yanaweza kuwa jambo la kawaida? Je, ni dalili gani zingine unazoweza kuangalia ili kuhakikisha kuwa hali mbaya za kiafya hazitokei?

advice): A Lady At My Lodge Threw Her Menstrual Pad On Me - Nairaland / General - Nigeria

Kitaalamu neno menorrhagia linatafsiriwa kama kutokwa na damu ya hedhi ambayo inaweza kuwa nyingi ya muda mrefu kuliko kawaida. Ikiwa kama unabadili pedi yako kila baada ya masaa mawili au muda mfupi tu, au kama yanapita mabonge makubwa ya damu, unaweza kuwa una tatizo la kutokwa na damu ya hedhi muda mrefu. Hali hii huwa inaleta masumbufu na mara nyingi maumivu makali, na wanawake wengi wanakabiliwa na na dalili za kudhoofika ambazo hutokana na vipindi vya muda mrefu vya hedhi.

Zipo sababu nyingi ambazo kipindi chako cha hedhi kinakuwa ni cha muda mrefu na damu nyingi na unatokwa na mabonge yad amu yasiyo ya kawaida, na habari njema ni kwamba magonjwa na sababu nyingi kwa ajili ya dalili hizi ni ya kawaida na yanatibika kabisa.

Hapa chini kuna sababu saba kwanini unaweza kutokwa na damu ye hedhi yenye mabonge na kutokwa na damu nyingi kuliko kawaida:

1. Magonjwa Kwenye Tezi Ya Tyhroid

Thyroid ni tezi inayokuwa shingoni mwako inayohusika na uzarishaji na usambazaji wa homoni. Kama haifanyi kazi vizuri, inaweza kuharibu mzunguko wako wa hedhi. Maradhi kama vile kuzarisha homoni kidogo sana za tezi ya thyroid(hypothyroid) au kuzarisha homoni nyingi zaidi za tezi ya thyroid(hyperthyroid) kunaweza kuharibu mtiririko na mzunguko wa hedhi.

Ili kupima vizuri ugonjwa wa tezi ya thyroid, basi daktari anapaswa achunguze tezi ya thyroid ili kujua afya yako. Daktari anaweza pia kupima ili kuona viwango vya homoni na kuchunguza ikiwa kama kinga ya mwili wako iko vizuri bila kuwa na ugonjwa kwenye tezi.

2. Vivimbe Ndani Ya Ukuta Wa Mfuko Wa Uzaizi(Polyps) Na Fibroid.

Vivimbe kama polyps na fibroid vinaweza kuota ndani ya tumbo la uzazi na utando wa ukuta wake na vinaweza kusababisha damu yako ya hedhi kutoka nyingi tena kwa muda mrefu kuliko kawaida. Zipo aina nyingi za vivimbe vya fibroid, lakini uvimbe wa fibroid unaoota ndani ya mfuko wa kizazi submucosal vinaweza kusababisha kabisa kutokwa na damu nyingi ya hedhi yenye mabonge makubwa. Vivimbe vinavyoota juu ya shingo ya kizazi au ndani kwenye ukuta wa mfuko wa uzazi vinaweza kuwa visababishi vya kutokwa na damu ya hedhi yenye mabonge. Kama unatokwa na damu nyingi ya hedhi, na mabonge makubwa yad amu au kiuno kuuma, inaweza kuwa chanzo ni uvimbe kama vile fibroid.

3. Uzazi Wa Mpango

Kama umeanza hivi karibuni mtindo mpya wa uzazi wa mpango na unatokwa na damu ya hedhi yenye mabonge makubwa, basi njia yako ya uzazi wa mpango inaweza kuchangia tatizo hilo. Baadhi ya njia za uzazi wa mpango, kama vile vijiti au vitanzi, vinaweza kusababisha kutokwa na damu nyingi kwa muda mrefu kuliko kawaida Pamoja na mabonge ya damu kwa baadhi ya wanawake. Kama una vitanzi na unatokwa na damu nyingi yenye mabonge, basi fika hospitali onana na daktari, mwambie dalili unazozipata ili kutambua ikiwa kama njia hii ya uzazi wa mpango ni nzuri.

4. Madawa Ya Vidonge

Kama uzazi wa mpango, yapo madawa mengi ambayo yanaweza kuchangia kutokwa na damu nyingi ya hedhi yenye mabonge kwa muda mrefu. Madawa ya vidonge kwa ajili homoni(kama vile estrogen na progestins) na mengine yanaweza kuchangia kubaribu mzunguko wa hedhi na kuwa mbaya. Kama unatokwa na mabonge makubwa ya damu wakati wa hedhi, jaribu kuchukua mtiririko wa hesabu ya madawa uliyotumia na muulize daktari madhara yake ni nini.

5. Mimba Kuharibika

Katika hatua ya awali ya ujauzito, kama kuna hali ya kuharibika kwa mimba au mimba kutunga nje ya kizazi, mara nyingi inaweza kusababishwa na kutokwa na damu nyingi yenye mabonge. Kuharibika kwa mimba kipindi cha awali kunaweza kupelekea kutokwa na damu nyingi yenye mabonge makubwa.

6. Kuota Kwa Tishu Ndani Ya Ukuta Wa Tumbo La Uzazi(Endometriosis)

Endometriosis kwa kawaida ni hali ya tishu kuota ndani  ya ukuta wa mfuko wa uzazi na kuendelea nje ya ukuta wa mfuko wa uzazi. Hali hii inaweza kusababisha kutokwa na damu ya hedhi yenye mabonge makubwa, maumivu ya tumbo la chini na vichomi vikali tumboni. Inaweza kuwa tatizo lenye maumivu makali sana na vigumu kufanya vipimo, lakini matibabu mbalimbali ya asili yanaweza kuondoa tatizo hili.

7. Vivimbe Vingi Kuota Kwenye Vifuko Vya Mayai

Hali nyingine ambayo inaweza kusababisha kutokwa na damu kwa muda mrefu  yenye mabonge, hii ni kutokuwa na uwiano sawa wa vichochezi(hormone imbalance). Vifuko vingi hujengeka kwenye vifuko vya mayai, ambavyo hushindwa kuachia mayai kwa kawaida, na hivyo kupelekea vipindi vya hedhi kubadirika.

Magonjwa Mengine Sugu Ya Muda Mrefu

Kuna magonjwa mengi ya muda mrefu ambayo yanaweza kuathiri kipindi chako cha hedhi na kukufanya utokwe na damu nyingi kwa muda mrefu, baadhii ya magonjwa hayo ni kama haya:

  • Saratani ya shingo ya kizazi
  • Kuvimba kwa shingo ya kizazi
  • Magonjwa ya tezi ya thyroid
  • Maambukizi katika via vya uzazi au PID.

Ndugu msomaji naomba niishie hapa nikaribishe kipindi cha maswali na maoni yako.

Pia unaweza ukatuma namba yako ya WHATsAP tukakuunganisha na darasa letu ukazidi kupata masomo kila siku.

Je, unahitaji duma? Basi unaweza kuwasiliana nasi kupitia namba hizi: 0752389252 au 0712181626,

Arusha-Mbauda,

Karibuni sana!