Nchini Marekani, takribani mtu mmoja kati ya watu watatu anaishi na shinikizo la damu yaani presha ya kupanda, ndiyo sababu mada ya mapendekezo ya chakula kwa shinikizo la damu inazidi kuwa maarufu zaidi siku hizi tulizo nazo.
Kwa kawaida kutotumia mboga na matunda ya kutosha kunaweza kusababisha kuwepo kwa sodiamu nyingi na kupungukiwa madini ya potasiamu, ambayo inaweza kuchangia kupandisha presha juu au shinikizo la damu kuwa kubwa.
Vyakula Vya Kuepuka Unapokuwa Na Shinikizo la Damu
Kwa hivyo unapokuwa na shinikizo la damu, unapendekezwa kuwa na lishe isiyo na sodiamu na mafuta, na uepuke vyakula hivi:
- Vyakula Vya Nyama Nyekundu (Kitimoto, Ng’ombe, Mbuzi, nk)
Watu wengi wanaogopa kuvila. Lakini kwa nini watu wengi huogopa kula? Kwa kuwa ina sodiamu nyingi, vipande vitatu vya nyama vina takribani mg 270 ya sodiamu na gramu 4.5 za mafuta, kwa hivyo ni busara kuviepuka.
- Maziwa Fresh Au Mgando
Unapojaribu kujenga misuli, maziwa yote ni chaguo lako bora, hutoa mafuta zaidi kuliko unavyohitaji, kikombe kimoja cha maziwa kina gramu 8 za mafuta. Ikiwa kama unaishi na tatizo presha ya kupanda (shinikizo la damu), jaribu kutumia asilimia 2% ya maziwa, au ikiwezekana achana nayo tu kabisa, kwani mafuta yaliyomo kwenye maziwa yote ni mabaya kwako na yanaweza kusababisha ugonjwa wa moyo. Ni hatari kwako!
- Donati/Vitumbua
Watu wanapenda donati na vitumbua, kwa ladha yake tamu, lakini sio vizuri kwa afya yako. Donati moja inaweza kutoa zaidi ya kalori 300 na gramu 12 za mafuta, kwa kuwa zimekaangwa, ambapo inamaanisha kuwa unaweza kupata mafuta mengi yaliyoshehena, ambayo yanaweza kuongeza hatari ya ugonjwa wa moyo katika mwili wako.
- Tambi
Tambi ni chakula maarufu miongoni mwa wanafunzi walioko vyuo vikuu ulimwenguni kote, kwa kuwa ni za bei nafuu na zinafaa sana. Walakini, sio chaguo la chakula chenye afya kwani hakina virutubishi na kina vitu vingi visivyofaa kwa afya yako. Paketi moja ya tambi ina gramu 1731 za sodiamu, zaidi ya asilimia 70% ya mahitaji ya kila siku yaliyopendekezwa! Kwahiyo haifai kabisa. Ili kuepukana na wingi wa sodium, ni bora kuacha kabisa kutumia chakula cha tambi.
- Pombe (Bia, nk)
Kunywa pombe kunaweza kuongeza shinikizo la damu kwa viwango visivyofaa, na pombe inaweza kuharibu kuta za mishipa ya damu. Kwa watu wenye shinikizo la damu, epuka unywaji wa pombe kabisa pombe kabisa.
NUKUU
Ikiwa una shinikizo la damu, ni vyema sana kujizuia kula vyakula vilivyo hapo juu na kuzingatia vyakula vyenye kiwango kidogo cha sodium kunaweza kusaidia afya ya mwili wako. Baadhi ya vyakula vizuri ni ndizi kwani zina kiwango kikubwa cha madini ya potasiamu, vitoweo visivyo na chumvi, viazi vitamu, samaki wabichi, mboga za majani kama vile mchicha kwani una madini ya chuma mengi.
Mungu akubariki sana msomaji naomba nikupatie wakati wa maswali na maoni yako.
Kama unahitaji huduma au msaada, tupigie: 0768 559 670/0712 181 626,
Arusha-Mbauda,
Karibu sana!