Mirija ya uzazi ni mirija inayokuwa kwenye mfumo wa uzazi wa mwanamke inayokuwa sehemu zote mbili za tumbo la uzazi. Hali yoyote ya kuziba kwenye mirija inaweza kuzuia yai kurutubishwa na mbegu za mwanaume.
NUKUU: Hali ya mirija ya uzazi kuziba husababisha ugumba kwa asilimia 25% hadi 30%. Hii huambatanisha mirija yote inapoziba moja kwa moja, yaani kuziba kwa mrija mmoja au majeraha au mikwaruzo kwenye mirija au mirija kusinyaa na kuwa myembamba. Hali hii ya kuziba inaweza kutibiwa kwa kutumia upasuaji au dawa za asili.
Je, Nini Umuhimu Wa Mirija Ya Uzazi Katika Urutubishaji Wa Mayai?
Kwakuwa urutubishaji hufanyika ndani ya mirija ya uzazi, hivyo hali yoyote ya uharibifu, au kuziba kwa mrija kunaweza kuzuia muingiliano wa yai na mbegu za mwanaume na kupelekea ugumba kwa mwanamke.
Hivyo basi, kuziba kwa mrija wa uzazi kunaweza kuruhusu kuingia kwa mbegu za mwanaume, lakini njia inaweza kuwa ni ndogo sana kiasi kwamba yai lililorutubishwa hushindwa kuingia kwenye mji wa mimba au tumbo la uzazi, na hivyo kusababisha mimba kutunga nje ya uzazi.
NUKUU: Kwahiyo basi, yai lililorutubishwa linaweza kujishikamanisha mahali popote nje ya tumbo la uzazi. Matokeo yake yatakuwa ni kutokwa na damu maeneo ya tumbo la chini. Tatizo la mimba kutunga nje ya uzazi linaweza kutatuliwa kwa njia ya madawa au upasuaji.
Kizuizi kwenye mrija wa uzazi kinaweza kutokea katika sehemu mbalimbali, ikiwa pamoja na:
- Karibu na tumbo la uzazi(Proximal end)
- Kwenye kifuko cha yai(Distal end)
- Mrija wote kuwa katika hali mbaya
Sababu zifuatazo zinaweza kusababisha kuziba au kuchubuka kwa mirija ya uzazi, na kupelekea hali ya ugumba kwa mwanamke:
- Kuvimba kwa mrija wa uzazi
- Mimba ya awali kutunga nje ya uzazi
- Mrija kufunga
- Kufanyiwa upasuaji
- Kuwa na vivimbe vidogo vidogo
- Uvimbe kwenye tumbo la uzazi(Fibroid)
NUKUU: Zaidi tena, kuziba kwa mrija wa uzazi kunaweza kuwa ni matokeo ya mkusanyiko wa majimaji kutoka kwenye mirija au majeraha au mikwaruzo.
Je, Dalili Zake Zinakuwaje?
Kwa kawaida, kuziba kwa mirija ya uzazi huwa hakuonyeshi dalili zozote. Hali mara nyingi huendelea kuwepo bila kufanyiwa matibabu mpaka pale mgonjwa atakapoanza kupatwa matatizo ya uzazi, kama vile;
- Kushindwa kubeba ujauzito
- Maumivu makali sehemu za nyonga hasa wakati wa hedhi
- Kuhisi maumivu makali wakati wa tendo la ndoa
- Mimba kutunga nje ya kizazi
- Maambukizi katika via vya uzazi kama vile PID
NUKUU: Hata hivyo, dalili hizi mara nyingi huwa hazionyeshi kuziba kwa mirija na zinapaswa kufanyiwa vipimo au uchunguzi kupitia daktari mtaalam kwa ajili ya vipimo sahihi.
Je, Unahitaji Kuondoa Tatizo La Mirija Kuziba?
James Herbal Clinic Tuna dawa nzuri kabisa zenye uwezo mkubwa wa kuondoa vyanzo vya kuziba kwa mirija ya uzazi pamoja na kutokubeba ujauzito, nazo ni MULTICURE POWDER, VITAMAKA na CARD HERB.
Kwa mawasiliano naomba utupigie kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626-Mbauda Pepsi.
Pia kama unahitaji kujiunga katika MAJUKWAA(GROUP) yetu katika mtandao wa TELEGRAM au WHATSAP, basi unaweza kutuma namba zako au ukajiunga kupitia link yetu hii: t.me/jamesherbalclinic.
Tunawakaribisha sana katika James Herbal Clinic, Karibuni sana.