Mirija ya uzazi ni ya muhimu sana katika kufanya kazi za mfumo wa uzazi wa mwanamke. Kumbuka wanawake wana mirija miwili ya uzazi, na kila mmoja umeungana na mfuko wa mayai(ovary) kila sehemu ya mfumo wa uzazi(uterus).
Kila mwezi yai lililopevuka hutolewa kwenye mfuko wa mayai kwa njia inayofahamika kama upevushaji. Yai husafiri ndani ya mrija mmoja ambao huungana na mbegu za mwanaume ili kufanya urutubishaji. Kiinitete kinapotokea baadaye huanza kusafiri kupitia mrija mpaka kwenye mfuko wa uzazi ili kujipachika kwa ajili ya ujauzito.
NUKUU: Pale mrija mmoja au yote miwili inapoziba, inaweza kusababisha ugumba huenda kwa kuzuia yai lisirutubishwe, au kuzuia kiinitete kilichotokea kisiweze kusafiri mpaka kufika kwenye mfuko wa uzazi(uterus). Mirija iliyoziba inaweza pia ikawa na madhara kama vile mimba kutunga nje ya uzazi.
Wanawake wengi hushindwa kufahamu kuwa wana tatizo la mirija ya uzazi kuziba mpaka pale wanapoona ugumu wa kushindwa kupata ujauzito, mpaka tu kutakapotokea dalili chache sana zitakazoashiria kuwa mirija ya uzazi imeziba. Na moja ya visababishi vya kuziba kwa irija ya uzazi kwanza huwa ni maambukizi ya ugonjwa wa pangusa, na asilimia 85% ya wanawake waliowahi kuwa na maambukizi haya hawakugundua kuwa wana maambukizi hayo.
NUKUU: Mimba inayotunga nje ya tumbo la uzazi hutokea pale kiinitete kinapojipachika katika eneo lisilo sahihi, na mara nyingi kiinitete hujipandikiza ndani ya mirija ya uzazi. Mimba zinazokuwa nje ya tumbo la uzazi zinaweza kuwa matokeo ya mirija ya uzazi kuziba au idadi ya vihatarishi vingi ikiwa pamoja na:
- Kuwepo kwa michubuko kwenye tishu za mirija ya uzazi
- Umri wa mwanamke kuwa mkubwa(miaka 35).
- Mimba kutunga nje ya tumbo la uzazi
- Maambukizi ya magonjwa ya zinaa yasiyotibiwa
- Maambukizi katika via vya uzazi
- Vivimbe kwenye utando wa ukuta wa mfuko wa uzazi
Maambukizi Katika Via Vya Uzazi(Pelvic Inflammatory Disease au PID).
Maambukizi ya kisonono au pangusa yanapokaa muda mrefu bila kutibiwa yanaweza kusababisha maambukizi katika via vya uzazi au PID kwa wanawake. Asilimia 5% ya dalili za maambukizi ya ugonjwa wa pangusa, huwa ziko juu sana hata kuliko kisonono.
Maambukizi mengine kama vile bakteria ukeni wanaweza pia kusababisha PID, lakini hii huwa ni ya kawaida sana. Maambukizi haya yanaweza kutokea kwenye michubuko ya mirija ya uzazi, na kujenga hali ya kuziba na kuzuia kabisa uwezo wa mwanamke kuwa mjamzito. Uharibifu wa mirija inayohusiana na maambukizi mara nyingi huwa mbaya zaidi kuliko vyanzo vingine kwasababu huharibu manyoya madogomadogo ambayo husukuma shahawa au mbegu na mayai pamoja.
Hii ndio maana mrija unaweza kuwa wazi lakini sio muda wote unafanya kazi. Hii ni kwasababu hata kama mrija uko wazi, pasipo manyoya hayo(cilia), mbegu na mayai huwa na muda mgumu wa kuweza kupatana. Na kama vikipatana, kiinitete kitakachotokea hakiwezi kufika kwenye mji wa mimba, inaweza ikatokea kwenye mrija wa uzazi.
NUKUU: Vihatarishi vya maambukizi katika via vya uzazi au PID vinaweza kupunguzwa kupitia vipimo vya kila mara, kupima magonjwa ya zinaa na kutumia kinga unapokuwa katika mahusiano na mtu usiye mfahamu vizuri. Maambukizi ya magonjwa ya zinaa yanaweza kuwa vigumu kuyafahamu kwasababu watu wengi huwa hawana dalili, na ndio maana kufanya vipimo kwa ajili ya magonjwa ya zinaa ni muhimu sana. Dalili za maambukizi katika via vya uzazi au PID zinaweza kuwa pamoja na;
- Kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi
- Kuhiusi maumivu makali wakati wa hedhi
- Maumivu ya tumbo la chini
- Kuhisi uchovu
- Kuhisi homa au baridi
- Kutokwa na uchafu ukeni wenye harufu mbaya
- Kuhisi maumivu makali wakati wa tendo la ndoa
NUKUU: PID inaweza kuongeza vihatarishi vya mimba kutunga nje ya uzazi. Kuonekana kwa maambukizi ya zinaa kama kisonono na pangusa kunaweza pia kuendeleza maumivu sugu na ugumba(kushindwa kupata ujauzito)kama matokeo ya PID.
Tishu Zenye Muonekano Wa Tishu Ya Ndani Ya Tumbo La Uzazi Kuota Nje Ya Tumbo La Uzazi(Endometriosis).
Endometriosis ni ugonjwa ambapo tishu zenye muonekano na wa tishu zinazoota ndani ya tumbo la uzazi wakati wa mzunguko wa hedhi ya mwanamke, huota nje ya tumbo la uzazi, mara nyingi juu au ndani ya viungo vingine vya uzazi. Unaweza kuwa ugonjwa wenye maumivu makali sana na ni moja ya visababishi vitatu vya ugumba kwa wanawake. Endometriosis inaweza kuwa ngumu kuichunguza na kuielewa kwasababu dalili zake zinafanana na magonjwa mengi ya uzazi. Dalili za endometriosis huwa kama hivi:
- Maumivu ya nyonga
- Maumivu wakati wa tendo la ndoa
- Maumivu wakati wa kukojoa
- Maumivu wakati wa kujisaidia haja kubwa
- Maumivu makali ya tumbo la chini
- Maumivu ya kiuno
- Kutokwa na damu nyingi sana wakati wa hedhi au damu kidogokidogo kabla ya kipindi cha hedhi kufika.
NUKUU: Endometriosis inaweza kusababisha matatizo kwenye mirija ya uzazi kwa njia mbili: tishu zilizokaa vibaya zinaweza kuziba mirija ya uzazi, au tishu zilizorundikana, upasuaji unapofanyika ili kuondoa tishu hizo kunaweza kusababisha michubuko kwenye mirija ya uzazi. Endometriosis inaweza kusababisha pia uharibifu kwenye vifuko vya mayai kutokana na madhara ya uvimbe, pamoja na uvimbe kwenye vifuko vya mayai pale unapojaribiwa kuondolewa mrundikano wa tishu, ambazo hutokea pindi tishu za endometrial zinapojinasa ndani ya vifuko vya mayai.
Nipende kumshukuru Mungu katika makala hii, naomba niishie hapa tutaonana katika vipindi vingine. Nikaribishe kipindi cha maswali na maoni kwa wale wote wanaosoma makala hii.
Je, Unahitaji Huduma? Wasiliana nasi katika namba hizi: 0752389252/0712181626.
Napenda kukumbusha kwamba, James Herbal Clinic tuna darasa letu la maswalia ya afya kupitia group la WHATSSP. Hivyo unaweza kutuma namba yako ya WHATSAP ukaunganishwa na group letu.
Karibuni sana!