YAJUE MADHARA YA MAAMBUKIZI YA PID YANAPOKAA MUDA MREFU BILA KUTIBIWA.

Maambukizi katika via vya uzazi(PID) wakati mwingine yanaweza kusababisha matatizo ya muda mrefu, hasa ikiwa kama ugonjwa huo haujatibiwa haraka kwa madawa ya kuua bakteria hao.

NUKUU: Lakini wanawake wengi wenye maambukizi katika via vya uzazi au PID wanaokamilisha dozi zao za ugonjwa wa PID huwa hawana matatizo ya muda mrefu kwasababu walikamilisha dozi zao kwa uhakika.

Je, Maambukizi Haya Yanapojirudia Yanakuwaje?

Baadhi ya wanawake hupatwa na maambukizi ya PID ya kujirudia rudia. Hali inaweza ikarudi ikiwa kama maambukizi ya awali hayakutibiwa vizuri. Hii mara nyingi ni kwasababu dozi au dawa walizotumia hazikuwa na uwezo au dozi hazikukamilika au kwasababu mwenza mwingine hakupata vipimo na kuanza matibabu.

Kama maambukizi ya PID yakiharibu tumbo la uzazi au mirija ya uzazi, basi inaweza kuwa rahisi sana bakteria kuambukiza maeneo haya baadaye, na kukufanya tatizo hili likurudie tena.

NUKUU: Maambukizi ya PID ya kujirudia rudia huambatana na muongezeko wa hatari wa hali ya ugumba au kutokupata ujauzito kabisa. Naomba wagonjwa wa PID wanaosoma makala hii muwe makini sana sana pale unapopimwa na tayari ukagundulika na PID. Usifanye uzembe hata kidogo katika kuanza matibabu.

Je, PID inaweza Kusababisha Majipu Au Uvimbe?

PID wakati mwingine inaweza kusababisha mkusanyiko wa majimaji yenye maambukizi yanayoitwa majipu au uvimbe ambao mara nyingi hujitokeza kwenye mirija ya uzazi pamoja na vifuo vya mayai.

Majimaji kwenye uvimbe au majipu yanaweza kutibiwa kwa madawa yenye antibiotic, lakini wakati mwingine upasuaji unaweza kuhitajika ili kunyonya majimaji hayo.

NUKUU: Majimaji yanaweza pia wakati mwingine kunyonywa kwa kutumia sindano ambayo huingizwa kwa kutumia Ultrasound scan. Lakini pia kumbuka kwamba, kwa kutumia njia hiyo, bado suluhisho halijapatikana maana majimaji yanaweza kunyonywa na kuondolewa na baadaye yatakusanyikana tena na kurudia hali ile ile ya mwanzo na hali ikaendelea kukusumbua.

Je, Maumivu Ya Nyonga Ya Muda Mrefu Yanakuwaje?

Baadhi ya wanawake wenye maambukizi katika via vya uzazi au PID hupata maumivu makali ya muda mrefu kwenye nyonga zao na tumbo la chini, ambayo yanaweza kuwa vigumu kuishi nayo na yanaweza kupelekea kuwapo kwa matatizo mengine zaidi kama vile msongo wa mawazo na kutokupata usingizi. Kama ukiendelea kupata maumivu makali kwenye nyonga, unaweza kupewa vidonge vya kuondoa maumivu ili kutowesha dalili hizo za maumivu.

Je, Vipimo Vinaweza Kuhitajika Ili Kujua Chanzo Cha Tatizo?

Vidonge vya kupunguza maumivu haviwezi kuondoa maumivu hayo, bali itakupasa ufike kliniki ili uweze kupata vipimo.

Je, PID Inaweza Kusababisha Mimba Ikatungwa Nje Ya Kizazi?

Mimba kutungwa nje ya uzazi ni pale yai lililorutubishwa linapojipachika lenyewe nje ya tumbo la uzazi, hasa kwenye mirija ya uzazi. Kama maambukizi katika via vya uzazi au PID yakiathiri mirija ya uzazi, basi yanaweza kutia vidonda kwenye kuta za mirija, na kulifanya yai lishindwe kupita na kuingia kwenye mji wa mimba.

NUKUU: Kama yai lililorutubishwa litajipachika kwenye mrija wa uzazi na kuanza kukua ndani ya mrija, basi linaweza kusababisha mrija upasuke, hali ambayo wakati mwingine inaweza kusababisha kutokwa na damu nyingi sana.

Kama ukipimwa na kukutwa kuwa una ujauzito nje ya tumbo la uzazi, unaweza ukapewa matibabu ili kulizuia yai lisiendelee kukua au unaweza kufanyiwa upasuaji ili kuliondoa kabisa.

Je, Hali Ya Ugumba Au Kutokushika Ujauzito Inakujaje?

Kadiri vihatarishi vinapozidi kuwa vingi na kusababisha mimba kutunga nje ya tumbo la uzazi, michubuko au majipu kwenye mirija ya uzazi, ndivyo humfanya mwanamke kushindwa kupata ujauzito ikiwa kama mayai hayataweza kupita kwa urahisi na kuingia kwenye tumbo la uzazi.

NUKUU: Inakadiriwa kwamba katika wanawake 10 wenye maambukizi katika via vya uzazi au PID, basi 1 anaweza kashindwa kupata ujauzito kama matokeo ya ugonjwa huo, pia na hata kwa wanawake wanaochelewa kupata matibabu mapema au wanaokuwa na maambukizi yenye kujirudiarudia mara kwa mara.

 

Je, Unahitaji Huduma Ili Kuondoa Tatizo Hili?

James Herbal Clinic tuna dawa nzuri kabisa zenye uwezo wa kuondoa chanzo cha maambukizi na madhara yake. Kwa mawasiliano naomba utupigie kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626, Arusha Mbauda.

 

Pia unaweza ukatuma namba yako ya WHATSAP au TELEGRAM kwa msaada zaidi wa elimu yetu ya afya na ukaunganishwa na JUKWAA(GROUP) letu la WHATSSAP au TELEGRAM ili upate kujifunza zaidi. Kama una APP ya telegram unaweza kubonyeza link hii t.me/jamesherbalclinic ukaweza kujiunga na darasa letu. Au kama una APP ya whatsap unaweza pia kubonyeza link hii https://chat.whatsapp.com/G0KeUI836orFZSgYcWGcE7

Karibuni sana!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *