ZIJUE DALILI 5 ZA UGONJWA WA MAAMBUKIZI KATIKA VIA VYA UZAZI(PID).

Dalili za ugonjwa PID huwa ni rahisi mno kuzigundua ikiwa kama ukijua namna ya kuzichunguza. Unapaswa kuzuia madhara ya ugonjwa wa PID na hali ya kutokupata ujauzito kwa kupata ushauri kwa daktari wako haraka iwezekanavyo mara unapougundua dalili za ugonjwa wa PID.

Ugonjwa wa PID ni msemo uliotumika kuelezea maambukizi ya viungo vyako vya uzazi yaliyosababishwa na bakteria. PID ni maambukizi ya kawaida kabisa, ambayo yanawapata watu wengi mno kila mwaka katika nyakati hizi.

Pelvic inflammatory disease: Symptoms, treatment, causes, and more

NUKUU: Kama ugonjwa huu usipotibiwa, basi unaweza kusababisha madhara makubwa kabisa katika kizazi chako, kwakweli ni chanzo tatizo la ugumba wenye kudumu daima. Ugonjwa wa PID unaweza kuwa ni matokeo ya idadi ya maambukizi ya magonjwa ya zinaa, kwahiyo hakikisha unatafuta tiba haraka mara unapoona dalili hizi zifuatazo:

1. Maumivu Ya Tumbo La Chini Au Kwenye Nyonga

Wakati viungo vyako vya uzazi vinapopata bakteria wa maambukizi ya ugonjwa wa zinaa, basi vivimbe hutokea ambao unaweza kusababisha maumivu makali sana. Baadhi ya maumivu ya tumbo la chini huwa ni ya kawaida wakati wa mzunguko wako wa hedhi, lakini maumivu yaliyosababishwa na ugonjwa wa PID huwa ni makali san ana huonekana kuliko maumivu ya kawaida ya tumbo la hedhi.

Kama ukihisi maumivu makali au maumivu yenye kupenya kwenye tumbo lako la hedhi au kwenye nyonga, basi wasiliana na daktarin wako haraka mno, hasa unapokuwa haupo kwenye kipindi cha hedhi,

2. Uchafu Utokao Ukeni Na Ukiwa Na Harufu Mbaya

Kiwango kidogo cha utoko mweupe huwa ni wa kawaida kabisa unapotoka ukeni, lakini kama ukiona kiwango kikubwa cha uchafu huku ukiambatana na harufu isiyo ya kawaida, inaweza kuwa ni dalili za ugonjwa wa PID. Unaweza usione maumivu ya nyonga yanayoambatana ikiwa kama maambukizi hayajafika kwenye mfuko wa uzazi kupitia mlango wako wa kizazi.

Unaziona dalili za maambukizi kwenye via vya uzazi kabla hayajafika kwenye viungo vya uzazi(yaani kwenye mlango wa uzazi, mfuko wa uzazi, mirija ya mayai na vifuko vya mayai), basi ni vyema kuzuia kabisa tatizo la ugumba. Kama ukiona uchafu mwingi ukikutoka ukeni ukiambatana na harufu mbaya, fika hospitali haraka sana.

3. Kuhisi Maumivu Makali Wakati Unapokojoa

Maumivu wakati unapokojoa mara nyingi huwa ni dalili za maambukizi kwenye kibofu cha mkojo. Kama yasipotibiwa, basi maambukizi ya kibofu yanaweza kuwa mabaya na baadaye kuingia kwenye mji wa mimba na kwenye vifuko vya mayai, na kusababisha PID. Kama ukihisi maumivu unapokuwa ukikojoa, daktarin wako atakufanyia kipimo cha mkojo ili kuona maambukizi hayo. Hakikisha unawasiliana na daktarin wako ikiwa kama unahisi maumivu makali wakati unapokojoa. Maumivu makali unapokojoa ni dalili za ugonjwa wa PID, na yanahitaji kutibiwa kwa kutumia antibiotic za asili zenye nguvu kabisa.

4. Homa

Homa inayopanda san ani ishara ya kwamba mwili wako unapambana na maambukizi. Kama homa yako ikiwa ya siku nyingi, basi fika hospitali muone daktarin aweze kuona dalili. Homa kali mara nyingi huwa haionyeshi PID. Hata hivyo, kama homa yako ikiambatana na maumivu ya nyonga au kutokwa na uchafu ukeni, basi ni ishara kubwa kwamba una dalili za maambukizi katika via vya uzazi, yaani ugonjwa wa PID.

5. Maumivu Wakati Wa Kujamiiana

Kama ukipatwa na maumivu wakati wa kujamiiana, hasa kama ikiwa ni hali inayojirudia mara kwa mara, inaweza kuwa ni ishara ya PID. Inawekana pia ukawa na maambukizi ya fangasi au kwenye kibofu cha mkojo, au kwamba eneo limeathiriwa na tendo la ngono kila siku. Maambukizi yanaweza kusababisha ugonjwa wa PID ikiwa hayatatibiwa haraka.

Pain During Sex: Causes and How It Impacts Fertility

NUKUU: Kama ukiugundua ugonjwa wa PID mapema, unaweza ukatibiwa kwa gharama kidogo tu za dawa. Usiruhusu dalili zako zikaachwa kufanyiwa uchunguzi la sivyo maambukizi hayo yanaweza kusababisha madhara makubwa mno huko baadaye. Kama ukiona dalili zozote za ugonjwa wa PID,basi fika hospitali ukapate vipimo halafu anza matibabu haraka.

Nipende kuishia hapa mpendwa msomaji, nikaribishe kipindi cha maswali na maoni yako, karibu sana!

Pia unaweza ukatuma namba yako ya WHATsAP tuweze kukuunganisha na darasa letu utaweza kupata huduma endelevu ya matatizo ya afya na pia utapata ushauari.

Je, Unahitaji Huduma?

Ukiwa kama unahitaji huduma ya matibabu, basi wasiliana nasi kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626.

Arusha-Mbauda

Karibuni sana!

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *