Maumivu ya kiuno ni ya kawaida. Inaweza kuanzia kuuma na kuhisi kama kitu kinapita kwa kuchoma kama kisu na kupotea. Inaweza kuwa ni dalili ya muda mfupi au inaweza kuwa endelevu.
Wanawake wote hupatwa na hali ya kutokwa na uchafu ukeni lakini kiwango na aina ya uchafu vinaweza kutofautiani. Uchafu wa kawaida mara nyingi huwa mweupe au wenye rangi ya kijivu mweupe. Unaweza kuonekana pia kama wa njano vile pale unapokaukia kwennye chupi. Unaweza kupatwa na mabadiriko kwenye uchafu unaotoka kutokana na matumizi ya dawa za uzazi wa mpango.
Hapo chini kuna visababishi 8 vya maumivu ya kiuno na kutokwa na uchafu ukeni.
1. Maambukizi Katika Njia Ya Mkojo(UTI)
Maambukizi ya UTI yanaweza kutokea katika sehemu yoyote ya njia ya mkojo. Bakteria husababisha idadi kubwa ya UTI. Fangasi au virusi wanaweza pia kusababisha maambukizi kwenye njia ya mkojo.
Dalili zake utaziona nazo huwa kama hivi ifuatavyo:
- Kuhisi hali ya kama kuwaka moto wakati unapokojoa
- Kuhisi kukojoa mara kwa mara
- Kukojoa mkojo wenye damu
- Mkojo wenye rangi ya kijivu
- Kukojoa mkojo wenye rangi kama ya koka kola
- Mkojo wenye harufu kali
- Kuhisi maumivu makali kiunoni kwa wanawake
- Kuhisi maumivu kwenye njianya haja kubwa kwa wanaume
2. Mrija Wa Mkojo Kuvimba(Urethritis)
Mrija wa mkojo unaobeba mkojo kutoka kwenye kibofu mpaka kuutoa nje, huvimba na kuleta masumbufu kwa muhusika. Shahawa nazo hupita kwenye mrija huu.
Dalili zanazojitokeza baada ya mrija kuvimba huwa kama hivi ifuatavyo:
- Kuhisi kukojoa mara kwa mara hata kama huna mkojo
- Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa
- Kuhisi maumivu makali kwenye njia ya mkojo
- Kutokwa na uchafu ukeni usio wa kawaida na unaweza pia kutoka pamoja na dalili za mkojo
3. Ugonjwa Wa PID
Ugonjwa wa PID ni maambukizi katika via vya uzazi kwa wanawake. Nyonga huwa iko ndani ya tumbo la chini na huungana na mirija ya uzazi, vifuko vya mayai, shingo ya kizazi pamoja na mfuko wa uzazi(uterus).
Baadhi ya wanawake wenye maambukizi katika via uzazi huwa hawana dalili. Lakini wanawake wanaopata dalili za PID, huonekana katika muonekano huu:
- Kuhisi maumivu kiunoni
- Kuhisi maumivu tumbo la juu
- Kuhisi homa
- Kuhisi maumivu wakati wa tendo la ndoa
- Maumivu wakati wa kukojoa
- Vipindi vya hedhi kubadirika
- Kutokwa na uchafu ukeni wenye harufu mbaya kabisa
- Mwili kuchoka
Ugonjwa wa PID unaweza kusababisha maumivu makali sana au ya kawaida tu. Hata hivyo, baadhi ya wanawake hupatwa na maumivu makali mno na dalili huwa kama hivi:
- Maumivu ya kuchoma na yanapita kwa kasi maeneo ya tumbo la chini
- Kutapika
- Kuhisi homa kali
- Kuzimia
4. Uke Kuvimba
Uke kuvimba ni hali inayotokana na maambukizi au kuvimba kwa mashavu ya kuvimba. Kama ukiendelea kuona dalili, zinaweza kuwa kama hivi ifuatavyo:
- Uke kuwasha
- Vidonda ukeni
- Mashavu ya uke kuvimba
- Badiriko katika kiwango cha uchafu unaotoka ukeni
- Badiriko kwenye muonekano wa rangi ya uchafu ukeni
- Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa
- Kuhisi maumivu wakati uume unaingia
- Uke kutokwa na matone ya damu mara kwa mara
5. Ujauzito
Ujauzito hutokea pale mbegu za mwanaume zinaporutubisha yai baada ya kuachiliwa kutoka kwenye kifuko cha yai wakati way ai kupevuka. Yai lililorutubishwa husafiri na kushuka chini kwenye mfuko wa uzazi, ambapo hujipachika. Yai linapojipachika vizuri ndipo mimba hutokea.
Unaweza kuona ishara nyingi na dalili mbalimbali kabla hujafanya kipimo cha ujauzito. Dalili zingine zinaweza kuonekana majuma yanayofuata baadaye, kadiri viwango vyako vya homoni vinavyozidi kubadirika. Dalili unaweza kuona kama hizi:
- Kichwa kugonga
- Kukosa hedhi
- Kutokwa na matone yad amu ukeni
- Uzito wa mwili kuongezeka
- Kuhisi kiungulia.
- Kukosa choo
- Kiuno kuuma
- Kupungukiwa damu
- Kukosa usingizi
- Matiti kubadirika
- Kutokwa na chunusi usoni
- Kutapika
- Kuharisha
6. Mimba Kutunga Nje Ya Kizazi
Kuhusiana na tatizo la mimba kunga nje ya kizazi, yai huwa haliwezi kujipachika kwenye mfuko wa uzazi. Badala yake, linaweza kujipachika kwenye mrija wa uzazi, sehemu ya uwazi wat umbo la chini, au kwenye shingi ya kizazi.
Hali ya kichefuchefu na matiti kuuma huwa ni dalili za mimba kutunga kwenye mrija wa mayai au mfuko wa uzazi. Dalili zifuatazo ni za kawaida sana kwa mimba inapotunga nje ya kizazi na zinaweza kushiria dalili hizi:
- Maumivu makali kupenya maeneo ya tumbo la chini, begani au shingoni
- Maumivu makali yanayojitokeza sehemu moja ya tumbo la chini
- Kutokwa na damu nyepesi ukeni
- Kuhisi kizunguzungu
- Kuhisi hali ya kichomi maeneo ya njia ya haja kubwa.
7. Saratani Ya Shingo Ya Kizazi
Saratani ya shingo ya kizazi ni aina ya saratani ambayo hutokea kwenye shingo ya kizazi. Shingo ya kizazi hushikamana na sehemu ya chini ya uke na mfuko wa uzazi.
Wanawake wengi wenye tatizo la saratani ya shingo ya kizazi huwa hawawezi kutambua kama wanao ugonjwa kwasababu mara nyingi ugonjwa huo huwa haunyeshi dalili mpaka hatua zitakazofuata baadaye. Zinapotoea dalili, huwa rahisi kuzikosea na kuzichanganya na hali ya kawaida tu kama vile damu ya hedhi na mambukizi kwenye njia ya mkojo yaani UTI.
Dalili za saratani ya shingo ya kizazi huwa kama hivi ifuatavyo;
- Kutokwa na damu isiyo ya kawaida, unapokuwa hedhini, au baada ya kumaliza kufanya tendo la ndoa, au baada ya kukoma kabisa hedhi,
- Kutokwa na uchafu ukeni ambao una harufu isiyo ya kawaida
- Kuhisi maumivu kwenye nyonga
- Kuhisi kukojoa mara kwa mara
- Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa
8. Kuuma Kwa Jointi Za Mifupa
Maumivu kwenye jointi vya mifupa yanaweza kusababishwa na maambukizi mwilini mwako. Hasa maambukizi ya magonjwa ya zinaa kwenye utumbo mdogo au mkubwa hupelekea kuwepo kwa maumivu kwenye jointi za mifupa.
Dalili zake huwa kama hizi zifuatazo:
- Kuhisi maumivu kwenye jointi za magoti, viwiko vya mkono
- Kuvimba kwa mrija wa mkojo
- Macho kuvimba au kuwasha
- Ngozi kuwasha sana, nk
Je, Unapaswa Kuonana Na Daktari Muda Gani?
Maumivu ya kiuno na kutokwa uchafu ukeni yanaweza kuashiria dalili mbaya. Kwahi unapaswa kuonana na daktari ikiwa kama una ujauzito na uchafu unaokutoka ukeni ni wenye rangi ya ukijani au njano, mzito sana, au wenye majimaji, kwasababu dalili hizi ni za maambukizi.
Unapaswa pia kufika hospitali kuonana na daktari ikiwa kama:
- Unatokwa na uchafu ukeni wenye rangi ya ukijani, njano au mweupe
- Una muwasho ukeni
- Unatokwa na uchafu mzito kama maziwa mgando
- Unatokwa na damu ukeni ambayo sio ya hedhi
- Unatokwa na uchafu ukeni wenye harufu mbaya kabisa
Ndugu msomaji makala yetu ndio imefikia mwisho, naomba nikukaribishe kwa kipindi cha maswali na maoni yako.
Pia unaweza kutuma namba yako ya WHATsAP tukakuunganisha na darasa letu ili uweze kuendelea kupata masomo ya afya kila siku.
Je, Unahitaji Huduma? Basi unaweza kuwasiliana nasi kupitia namba hizi: 0752389252 au 0712181626,
Arusha-Mbauda,
Karibuni sana!