ZIJUE SABABU, DALILI, NA MADHARA YA KUVIMBA KWA UKE

Kuvimba kwa uke kunaweza kuashiriwa na kutokwa na uchafu, au kuwa na  muwasho na maumivu ukeni. Kwa kawaida Chanzo huwa ni badiriko kwenye uwiano wa bakteria ukeni au maambukizi. Viwango vya homoni ya estrogen vinapopungua baada ya kukoma hedhi pamoja na maradhi mengine ya ngozi pia yanaweza kusababisha uke kuvimba.

Aina kuu za uke kuvimba huwa kama hivi ifuatavyo:

  • Bakteria Ukeni: Hali hii hutokana na kuongezeka kwa bakteria wa asili wanaokuwa ukeni mwako, ambayo huvuruga uwiano wa asili.
  • Maambukizi Ya Fangasi Ukeni; Hali hii kwa kawaida husababishwa na fangasi wa asili wanaoitwa Candida albicans.
  • Malengelenge: Hali hii husababishwa na vimelea na mara nyingi huambukizwa kwa magonjwa ya zinaa.

Matibabu yake hutegemeana na aina ya uvimbe wa uke ulionao, lakini JAMES HERBAL CLINIC tunazo dawa za asili zenye uwezo wa kuondoa vyanzo vyote.

Je, Dalili Zake Zinakuwaje?

Dalili za uke kuvimba huwa sio nyingi mno, lakini zinapojitokeza humfanya muhusika kusumbuka sana, nazo huwa kama hivi ifuatavyo:

  • Kubadirika kwa rangi au harufu au kiwango cha uchafu unaotoka ukeni
  • Uke kuwasha sana
  • Kuhisi maumivu wakati wa tendo la ndoa
  • Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa
  • Kutokwa na matone ya damu nyepesi ukeni

Kama unatokwa na uchafu ukeni, muonekano wa uchafu lazima uonyeshe aina ya uvimbe ukeni ulionao. Kwa mfano:

  • Bakteria Ukeni: Lazima uendelee kutokwa na uchafu wenye rangi ya kijivu, harufu mbaya. Harufu, mara nyingi inayokuwa kama shombo la samaki lazima idhihirike zaidi baada ya kumaliza kushiriki tendo la ndoa.
  • Maambukizi Ya Fangasi Ukeni: Dalili kuu huwa ni muwasho, lakini lazima utokwe na uchafu mweupe mzito unaofanana na maziwa mgando.
  • Malengelenge: Maambukizi ambayo kitaalamu yanaitwa, “trichomoniasis” yanaweza kusababisha kutokwa na uchafu ukeni wenye rangi ya kijani kuelekea njano, wakati mwingine unakuwa na uchafu wenye povu.

Je, Lini Unapaswa Kuonana Na Daktari?

Fika hospitalini uonane na daktari muhusika unapokuwa na masumbufu ukeni mwako, hasa endapo kama:

  • Unatokwa na uchafu mbaya au unahisi muwasho
  • Hujawahi kuwa na maambukizi ukeni. Lakini kuonana na daktari wako kutakusaidia kutambua dalili za maambukizi
  • Uliwahi kuwa na maambukizi kabla
  • Ulikuwa na wapenzi wengi baada ya kuwa na mpenzi mpya.
  • Uliwahi kuwa na magonjwa ya zinaa, baadhi ambayo yana dalili zinazofanana na maambukizi ya fangasi au bakteria ukeni.
  • Una hisi homa au baridi au maumivu ya nyonga.

Je, Vyanzo Vyake Ni Nini?

Chanzo hutegemeana na aina gani ya uvimbe ukeni uliyonayo:

  1. Bakteria Ukeni

Aina ya kawaida ya uke kuvimba hutokana na badiriko la bakteria wanaoonekana ukeni mwako, wanaovuruga uwiano. Kinachosababisha uwiano kutokuwa sawa, hakifahamiki. Inawezekana kuwa na bakteria ukeni bila kuona dalili zozote.

Aina hii ya uke kuvimba inaonekana kuwepo lakini haisababishwi na ngono, hasa ikiwa kama ukiwa na wapenzi wengi au mpenzi mpya uliyempata, lakini pia hutokea kwa wanawake wasiopenda ngono sana.

  1. Maambukizi Ya Fangasi Ukeni

Hali hii hutokea pale kunapokuwa na muongezeko wa utando wa vimelea wa fangasi, mara nyingi Candida albicans, ukeni mwako. Candida albicans pia husababisha maambukizi katika maeneo mengine yenye unyevunyevu mwilini mwako, kama vile kinywani mwako, kwapani na kwenye makucha vidoleni.

  1. Malengelenge

Ugonjwa huu wa zinaa wa kawaida sana nao husababishwa na kimelea mmoja asiyeonekana kwa macho anayeitwa, “trichomoniasis vaginalis.” Kimelea huyu husambaa wakati unapofanya tendo la ndoa na mtu mwingine mwenye maambukizi hayo.

Kwa wanaume, kimelea mara nyingi huathiri njia ya mkojo, lakini mara nyingi haisababishi dalili. Kwa wanawake, maambukizi ya malengelenge kwa kawaida huathiri uke, na lazima yasababishe dalili. Pia huongeza vihatarishi vya mwanamke kupata maambukizi mengine ya magonjwa ya zinaa.

  1. Kuvimba Kwa Uke Pasipokuwa Na Maambukizi

Tabia ya kupurizia marashi ukeni, kuosha uke kwa sabuni zenye manukato makali, kunaweza kusababisha aleji au miwasho kwenye mashavu ya uke. Vitu vya kigeni, kama vile pedi inapokaa muda mrefu ukeni, inaweza kuharibu tishu ya uke.

  1. Uke Kuwa Mkavu

Kupungua kwa viwango vya homoni ya estrogen baada ya kukoma hedhi au kuondolewa kwa vifuko vyako vya mayai kwa njia ya upasuaji, kunaweza kusababisha ukuta wa uke kwa ndani kuwa mwembamba, wakati mwingine hutokea hali ya uke kuwasha sana, kuhisi kama moto fulani ukeni na kuwa mkavu mno.

Je, Vihatarishi Vyake Ni Nini?

Mambo ambayo huongeza vihatarishi vinavyoendeleza uke kuvimba ni pamoja na haya yafuatayo:

  • Mabadiriko ya homoni kama vile unapokuwa mjamzito
  • Madawa ya uzazi wa mpango
  • Kuwa na maambukizi ya magonjwa ya zinaa
  • Kutumia marashi ukeni
  • Kuwa na ugonjwa wa kisukari usiodhibitiwa
  • Kutumia sabuni za marashi ukeni
  • Kuvaa nguo za ndani zenye kubana sana
  • Kuweka vitanzi ili kuzuia ujauzito, nk

Je, Madhara Yake Yanakuwaje?

Wanawake wenye maambukizi ya trichomiasis au bakteria ukeni wapo kwenye hatari kubwa  ya kupata maambukizi ya magonjwa ya zinaa kwasababu ya uvimbe uliosababishwa na magonjwa haya.

Ndugu msomaji makala yetu inaishia hapa, nakukaribisha kwa maswali na maoni yako, karibu sana!

Pia unaweza ukatuma namba yako ya WHATSAP ili tuweze kukuunganisha na darasa letu endelevu la afya.

Je, Unahitaji Huduma?

Wasiliana nasi kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626,

Arusha-Mbauada

Karibu sana!

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *