Ini ni kiungo kikubwa kigumu kinachokuwa ndani ya mwili wako. Ini huondoa sumu kwenye damu , hutengeneza viwango safi vya sukari kwenye damu, hurekebisha damu isigande, na hufanya kazi mamia na kazi zingine muhimu kabisa. Kama ilivyo kawaida, ini lako huwa lipo ndani ya mbavu upande wa kulia maeneo ya tumbo la chini.
Je, Mambo Muhimu Ya Ini Yanakuwaje?
Zingatia sana kuyafahamu mambo haya kwani ni faida katika afya ya mwili wako, nayo yanahusu utendaji kazi wa ini kama hivi ilivyo:
- Ini huchuja damu yote mwili na huondoa chembechembe za sumu, kama vile pombe au madawa makali.
- Ini pia huzarisha nyongo, ute ambao husaidia kumeng’enya mafuta na kuondoa uchafu
- Ini lina migawanyiko minne, ambayo kila mmoja umetengenezwa na sehemu nane na migawanyiko mingine maelfu midogo midogo kabisa.
Je, Kazi Ya Ini Ni Nini?
Ini ni kiungo muhimu sana mwilini mwako ambacho hufanya kazi zaidi ya 500. Hii ni pamoja na kuondoa vitu vichafu pamoja na sumu kwenye mfumo wa damu, kurekebisha kiwango cha sukari kwenye damu, na kutengeneza virutubisho vizuri. Hapo chini kuna kazi zake muhimu kabisa, nazo ni kama hizi zifuatazo:
1.Uzarishaji Wa Albumin
Albumin ni protini ambayo huzuia uteute unaokuwa kwenye mfumo wa damu usiweze kuvuja na kuingia kwenye tishu zinazolizunguka ini. Pia hubeba homoni au vichocheo, vitamini pamoja na enzyme mwilini mwote.
2.Huzarisha Nyongo
Nyongo ni uteute ambao ni muhimu sana katika umeng’enyaji chakula na unyonyaji wa mafuta ndani ya utumbo mwembamba.
3.Huchuja Damu
Damu yote inayotoka tumboni na kwenye utumbo mukubwa na mdogo hupita kwenye ini, ambalo huondoa sumu, na vitu vingine vibaya.
4.Hurekebisha Amino Asidi
Uzarishaji wa protini hutegemeana na wingi wa amino asidi. Ini huhakikisha kuwa viwango vya amino asidi kwenye mfumo wa damu hubaki ukiwa na afya.
5.Hurekebisha Mgando Wa Damu
Kuganda kwa damu hutengenezwa kwa kutumia vitamani K, ambayo inaweza kunyonywa kwa msaada ya nyongo, ute ambao huzarishwa na ini.
6.Huzuia Maambukizi
Kama sehemu ya uchujaji, ini pia huondoa bakteria kutokwa kwenye mkondo wa damu.
7.Huhifadhi Vitamini Na Madini
Ini huhifadhi viwango muhimu vya vitamini A, D, E, K na B12, pamoja na madini ya chuma na shaba.
8.Hurekebisha Sukari Kwenye Damu
Ini huondoa kiwango kikubwa cha sukari kwenye mkondo wa damu na huihifadhi kama glycogen. Inapohitajika, basi ini huibadiri glycogen na kuwa sukari(glucose).
Je, Nini Sababu Ya Ini Kujaa Mafuta?
Ugonjwa huu wa ini kujaa mafuta huwa na muonekano wa uvimbe, ambao unaweza kuendelea kuwa na michubuko na uharibifu usio badirika. Uharibifu huu unafanana na uharibifu uliosababishwa na utumiaji mkubwa wa pombe. Hivyo basi, hali hii unaweza kuendelea kulifanya ini kuwa kubwa au kushindwa kufanya kazi.
Ugonjwa wa ini kujaa mafuta unaongezeka kuwa wa kawaida kabisa duniani leo, hasa katika nchi za ulaya. Nchi za Amerika inaonekana kuwa ndio ugonjwa sugu unaoathiri karibia asilimia 80%-100% ya watu mamilioni.
NUKUU: Ugonjwa wa ini kujaa mafuta huonekana kwa kila umri wa mtu hasa kwa watu waliofikia umri wa miaka 40-50 wanaokuwa kwenye hatari ya magonjwa ya moyo kwa sababu ya kuwa na miili minene na magonjwa ya kisukari. Hali hii pia inasababishwa na mkusanyiko wa mafuta, ambao hutokana na:
- Kutoyeyushwa kwa mafuta mwilini,
- Kutokuwa na uwezo wa kutumia vichocheo vya insulin,
- Shinikizo la juu la damu au presha ya kupanda na
- Damu kuwa nzito.
Je, Dalili Zake Zinakuwaje?
Ugonjwa wa ini kujaa mafuta kwa kawaida hausababishi dalili wa ishara. Lakini zinapoanza kuonekana dalili huwa kama ifuatavyo:
- Ini kuwa kubwa
- Mwili kuchoka
- Kuhisi maumivu juu ya tumbo upande wa kulia
Dalili au ishara zinazompata muhusika pale atatizo limeshakuwa kubwa, huwa kama ifuatavyo:
- Tumbo kuvimba
- Mishipa ya damu kutanuka hasa chini ya uso wa ngozi
- Matiti ya mwanaume kuwa makubwa
- Bandama kuvimba
- Viganja vya mikono kuwa myekundu
- Ngozi ya mwili pamoja na macho kuwa ya njano
Je, Nini Visababishi Vyake?
Ugonjwa wa ini kujaa mafuta husababishwa na mambo mengi mno ambayo wengi hushindwa kuyatambua haraka, nayo huwa kama haya yafuatayo:
- Mwili kuwa mzito(yaani mnene)
- Seli za damu kushindwa kusafirisha vichocheo vya insulin
- Kuwa na ugonjwa wa moyo kama vile presha ya kupanda
- Kiwango kikubwa cha mkusanyiko wa mafuta kwenye damu.
Tatizo hili hutokana na mkusanyiko wa mafuta kwenye ini. Kwa baadhi ya watu, mkusanyiko huu wa mafuta huonekana kama sumu kwenye seli za ini, na hivyo kusababisha ini kuvimba, hali ambayo hupelekea kujenga majeraha kwenye ini.
Je, Unawezaje Kuzuia Tatizo Hili?
Ili kuzuia vihatarishi vya ugonjwa huu unapaswa kubadirisha mitindo yako ya ulaji na unywaji kwa kufanya mambo haya yafuatayo:
- Hakikisha unachagua vyakula vizuri vya matunda, mbogamboga,na nafaka,
- Epuka vyakula vyenye mafuta mengi
- Usiruhusu hali ya unene au kitambi,
- Fanya mazoezi kila siku katika kila wiki.
Mungu akubariki sana ndugu msomaji, naomba makala yetu iishie hapa, nikaribishe kipindi cha maswali na maoni yako, karibu sana!
Unaweza pia kutuma namba yako ya WHATsAP ukaungana na darasa letu ili uweze kupata masomo mengi zaidi ya afya.
Je, Unahitaji Huduma?
Wasiliana nasi kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626,
Arusha-Mbauda,
Karibuni sana!