Chakula kutokusagwa au mchafuko wa tumbo ni msemo wa kawaida ambao huelezea masumbufu ndani ya tumbo lako la juu. Chakula kutokusagwa sio ugonjwa, bali kuna baadhi ya dalili unaweza kuzipata, ikiwa pamoja na maumivu ya tumbo na kujisikia tumbo kujaa gesi muda mfupi tu unapoanza kula. Ingawa hali ya tumbo kujaa gesi huwa ni ya kawaida, lakini kila mtu anaweza kupatwa na hali ya kukosa choo katika njia tofauti. Dalili za kukosa choo unaweza kuzihisi mara kwa mara au kila siku.
NUKUU: Hali ya tumbo kujaa gesi inaweza kuwa dalili ya ugonjwa wa kutokusagwa kwa chakula tumboni. Sio kwamba hali ya tumbo kujaa gesi inaweza kusababishwa na ugonjwa, huenda inaweza kusababishwa na mabadiriko ya mitindo ya maisha na madawa.
Je, Dalili Zake Zinakuwaje?
Watu wenye tatizo la tumbo kujaa gesi kwa karne hii ni wengi sana, na dalili zake huwa kama hivi ifuatavyo;
- Tumbo kujaa haraka tu wakati unapokula hata kama ni chakula kidogo
- Kutokujisikia vizuri baada ya kumaliza kula
- Kuhisi masumbufu kwenye tumbo la chakula
- Kuhisi kama hali ya kuwaka moto maeneo ya tumbo la juu
- Tumbo kuunguruma
- Kuhisi kichefuchefu
NUKUU: Wakati mwingine watu wenye tatizo hili pia huhisi kiungulia, lakini kiungulia na tumbo kujaa gesi ni hali mbili zinazotofautiana. Kiungulia ni maumivu au kuhisi kuwaka moto maeneo ya katikati ya kifua chako ambayo yanaweza kupenya shingoni mwako au mgongoni wakati au baada ya kumaliza kula.
Je, Unapaswa Kufanya Nini Inapotokea Hali Hii?
Inapotokea hali ya kawaida tu ya tumbo kujaa gesi hupaswi kubabaika sana. Fika hospitali ikiwa kama masumbufu yanaendelea zaidi ya wiki mbili. Onana na daktari haraka kama maumivu ni makali au kama yanaambatana na:
- Mwili kupungua uzito au kutokuwa na hamu ya kula chakula
- Kurudia kutapika au kutapika damu
- Kutoa kinyesi cheusi
- Kushindwa kumeza chakula
- Mwili kuchoka au kudhoofika, hali ambayo huashiria kupungukiwa damu
Tafuta haraka tahadhari ya matibabu endapo kama utahisi hali mbaya zaidi kama hizi zifuatazo;
- Kukosa pumuzi,
- Kutokwa na jasho jingi au maumivu ya kifua yakipenya mpaka kwenye taya, shingo au mkono
- Kifua kuuma au kuwa na msongo wa mawazo.
Je, Nini Visababishi Vyake?
Hali ya tumbo kujaa gesi ina visababishi vingi. Mara nyingi, tumbo kujaa gesi linahusika na mitindo ya maisha ya wanadamu na inaweza kusababishwa na ulaji wa vyakula vibaya, vinywaji vibaya au utumiaji wa madawa mabaya. Vyanzo vya kawaida vya tumbo kujaa gesi ni pamoja na:
- Kula sana au kula kwa haraka haraka bila kutafuna
- Kula vyakula vyenye mafuta mengi au viungo vingi
- Vinywaji vyenye caffeine, pombe, chokoleti, nk
- Uvutaji sigara
- Wasi wasi
- Kutumia dawa za kupunguza maumivu kama vile, panadol, asprin, nk
Wakati mwingine hali ya tumbo kujaa gesi husababishwa na magonjwa mengine ya tumbo kama vile;
- Kuvimba kwa mfuko wa chakula(gastritis)
- Vidonda vya tumbo
- Mawe kwenye figo
- Kukosa choo
- Kuvimba kwa kongosho
- Saratani ya tumbo
- Utumbo kuziba
- Mtiririko wa damu kuwa mdogo kwenye utumbo
Je, Nini Madhara Yake?
Ingawa hali ya tumbo kujaa gesi mara nyingi haiwezi kuwa na madhara makubwa, lakini bado inaweza ikaathiri ubora wa maisha yako kwa kukufanya wewe ujisikie vibaya na kukufanya usijisikie kula. Unaweza ukashindwa kwenda kazini au shuleni kwasababu ya dalili za tatizo hili. Pale hali ya tumbo kujaa gesi inaposababishwa na maradhi mengine, basi hayo maradhi pia yanaweza kuwa na madhara yake yenyewe. Kuwa makini sana unapoanza kuona tatizo la tumbo kujaa gesi!!
Nikushukuru sana ndugu msomaji, makala yetu inaishia hapa, nikaribishe kipindi cha maswali na maoni yako.
Je, Unahitaji Huduma?
Basi wasiliana nasi kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626.
Pia unaweza ukatuma namba zako za WHATSAP ili uweze kuunganishwa na darasa letu la WHATSAP, ukaweza kuendelea kupata mafunzo juu ya afya.
Karibu sana katika kituo chetu cha afya JAMES HERBAL CLINIC,
Arusha-Mbauda.