ZIJUE SABABU ZA TUMBO KUJAA GESI NA KUUMA

Gesi katika mfumo wa umeng’enyaji ni sehemu kawaida ya njia ya umeng’enyaji. Ili kuepukana na ongezeko la gesi, iwe ni kwa kujamba au kucheua, pia ni kawaida. Maumivu ya gesi yanaweza kutokea ikiwa kama gesi haiendi vizuri kwenye mfumo wako wa umeng’enyaji.

How to Get Rid of Intestinal Gas Pain: Causes, Symptoms & Treatment

NUKUU: Kuongezeka kwa gesi au maumivu ya gesi yanaweza kutokana na ulaji wa vyakula ambavyo vinaweza kuzarisha gesi tumboni. Mara nyingi, mabadiriko katika tabia za ulaji yanaweza kupunguza masumbufu ya gesi.

Matatizo mbalimbali  katika mfumo wa umeng’enyaji, kama vile kutoa choo hewa au chenye makamasi kamasi, au tumbo kuvurugika,  inaweza kusababisha dalili zingine kuongeza gesi na maumivu tumboni.

Je, Dalili Zake Zinakuwaje?

Dalili za tumbo kujaa gesi au maumivu ya gesi ni kama ifuatavyo;

  • Kujamba
  • Kucheua
  • Tumbo la chini kuunguruma, vichomi au kuuma
  • Tumbo kujaa au kuunguruma
  • Tumbo kuonekana kuwa kubwa

Belly bloat: Why your hormones might be the secret cause

NUKUU: Kujamba ni kawaida, hasa baada ya kula. Watu wengi hucheua zaidi ya mara 20 kwa siku. Kwahiyo, unapokuwa na tatizo la gesi tumboni, basi unaweza kuwa na uwezo wa kuchangamana na watu au ukawa na aibu ya kuwa karibu na wengine kwasababu ya kujambajamba au kucheua au tumbo kukaa linaunguruma mara kwa mara. Wengi huwafanya kuhisi aibu kutoka na mazingira waliyojiwekea na sifa walizo nazo.

Je, Ni Kipindi Gani Unatakiwa Kufika Hospitali?

 

Fika hospitali ikiwa kama tumbo lina gesi au maumivu ya gesi ni endelevu au makali kiasi kwamba yanakufanya usijikie amani na furaha hata katika kufanya kazi zako za kila siku nyumbani au ofisini. Gesi au maumivu ya gesi yanayoambatana na dalili zingine yanaweza kuonyesha matatizo makubwa.

Appendicitis: Early symptoms and warning signs

Fika hospitali haraka ikiwa kama utaona dalili zozote kati ya hizi zifuatazo;

 

  • Choo chenye damu
  • Mabadiriko katika choo kinachotoka mara kwa mara
  • Kupungua uzito
  • Kukosa choo au kuharisha
  • Kuhisi kichefuchefu au kutapika

Fanya juu chini uweze kupata matibabu haraka ikiwa kama;

  • Tumbo la chini litaendelea kuuma sana
  • Kifua kuuma

 

Je, Nini Husababisha Tumbo Kujaa Gesi?

 

Gesi kujaa tumboni kwanza kabisa husababishwa na kumeza hewa wakati unapokula au kunywa. Gesi nyingi hupungua pale unapojamba.

Burping and stomach pain: Possible causes and remedies

NUKUU: Gesi hujengeka kwenye utumbo mkubwa wakati bakteria wanapotengeneza wanga, fiber, na baadhi ya sukari ambavyo havimeng’enywi kwenye utumbo wako mdogo. Bakteria pia huharibu baadhi ya gesi, lakini inayobaki hutolewa nje kwa kujamba.

Je, Ni Vyakula Gani Vya Kawaida Vinavyosababisha Gesi?

 

Vyakula mbalimbali vyenye wingi wa fiber vinaweza kusababisha gesi, navyo ni;

 

  • Maharage na kunde
  • Matunda
  • Mbogamnboga
  • Vyakula vya nafaka

NUKUU: Ikiwa vyakula vyenye wingi wa fiber huongeza uzarishaji wa gesi, lakini fiber inafaa katika kuuweka mfuko wa umeng’enyaji katika utaratibu mzuri wa utendaji kazi na kurekebisha sukari kwenye damu pamoja na kiwango cha lehemu.

Je, Sababu Zingine Zinakuwaje?

Sababu zingine za lishe ambazo zinaweza kuchangia kuongezeka kwa gesi kwenye mfumo wa umeng’enyaji ni hizi zifuatazo;

  • Vinywaji vyenye wingi wa Carbon, kama vile soda na bia
  • Tabia ya ulaji kama vile, kula haraka haraka, kunywa harakaharaka, utafunaji, akuongea wakati unapotafuana ambako husababisha kuvuta hewa nyingi.

 

Mungu awabariki sana wapendwa mnaosoma makala hii, naomba nikomee hapa, tutaonana katika makala nyingine. Asanteni sana.

 

Kwa wale wanaohitaji huduma naomba mtupigie kwa namba hii: 0752 389 252 au 0712 181 626

Arusha-Mbauda

 

Pia tuna darasa letu zuri katika mtandao wa TELEGRAM, wale wanapoenda kujiunga na darasa letu unaweza kutuma namba yako ya WHATSSAP tukakutumia link.

 

Karibuni sana!

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *