Mtoto asiye ridhiki ni pale mtoto anapofia tumboni kabla mjamzito hajafikisha muda wa kujifungua. Sababu huwa ni nyingi zisizoelezeka katika 1/3 ya matatizo haya. Wakati mwingine hali hii inaweza kusababishwa na matatizo ya kondo au kitovu, shinikizo la juu la damu, maambukizi, au kasoro za kujifungua, au maisha duni aliyokuwa amechagua mjamzito.
NUKUU: Hali ya mtoto asiye riziki inaweza kuainishwa kwa namna kama tatu hivi, nazo huwa kama hivi ifuatavyo;
- Mtoto anapofia tumboni kati ya wiki 20 au 27
- Mtoto anapofia tumbni kati ya wiki 28 au 36
- Mtoto anapofia tumboni kati ya wiki 37 au baada ya wiki hizo
Je, Kuna Tofauti Gani Kati Ya Mtoto Kufia Tumboni Na Mimba Kuharibika?
Kama ilivyo mtoto kufia tumboni, vilevile mimba kuharibika pia ni kupotea kwa ujauzito. Hata hivyo, wakati kitendo cha mtoto kufia tumboni ni kupoteza mtoto baada ya wiki 20 za ujauzito, basi kuharibika kwa mimba hutokea kabla ya wiki hizo 20.
Je, Nini Husababisha Mtoto Kufia Tumboni?
Chanzo cha mtoto kufia tumboni sio muhimu sana kukifahamu na sio tu kwa watoa huduma, bali na hata kwa wazazi ili kuweza kuwasaida katika harakati zao wanapokuwa katika majonzi. Vyanzo hivi mara nyingi huwa havifahamiki, lakini visababishi vinaweza kuwa pamoja na mambo kama haya;
- Matatizo Kwenye Kondo Au Kitovu
Kondo ni kiungo ambacho kinafunika mfuko wa uzazi kwa ndani unapokuwa mjamzito. Hivyo basi, kiumbe kinachokuwa tumboni hupata hewa ya oksijeni, damu na virutubishi kupitia kondo na kitovu. Matatizo yoyote yanayokuwa kwenye kondo au kitovu yanaweza kukifanya kiumbe kisiendelee vizuri.
- Msukumo Mkubwa Wa Damu
Msukumo mkubwa wa damu na uvimbe mara nyingi hutokea baadaye kwenye ujauzito. Kama una tatizo hili, unaweza ukawa na hatari ya kondo kupasuka au mtoto kufia tumboni.
- Damu Kuganda
Mama mwenye tatizo la damu kuganda yuko katika hatari ya mtoto kufia tumboni.
- Matumizi Ya Madawa Pale Mama Anapokuwa Mjamzito
Magonjwa mengine yanaweza wakati mwingine kusababisha mtoto kufia tumboni. Orodha ya magonjwa haya ni pamoja na kisukari, ugonjwa wa moyo, ugonjwa wa tezi ya thyroid, au maambukizi ya bakteria au virusi.
- Uchaguzi Mitindo Ya Maisha: Kama mtindo wa maisha yako ni pamoja na ulevi pombe, matumizi ya sigara, au madawa ya kulevya, unaweza ukasababisha mtoto kufia tumboni.
- Kasoro Za Uzazi: Kasoro moja au zaidi zinaweza kuwa chanzo cha mtoto kufia tumboni. Kasoro za uzazi hutamburika kwa nadra sana bila uchunguzi wa kiumbe kinachokuwa tumboni, ikiwa pamoja na kipimo cha ndani cha mwili wa mtoto.
- Maambukizi: Maambukizi kati ya wiki 24 na 27 yanaweza kusababisha kiumbe kufia tumboni. Kwa kawaida , huwa ni maambukizi ya bakteria ambao husafiri kutoka ukeni mwako mpaka kwenye tumbo la uzazi. Bakteria wa kawaida kama vile E.coli, klebsiella, enterococcus, Haemophilus influenza, pangusa(Chlamydia) na mycoplasma.
NUKUU: Nyongeza ya matatizo ni pamoja na rubella, mafua, mkanda wa jeshi, magonjwa ya maralia, nk. Baadhi ya maambukizi hupotea bila kufahamika mpaka pale muhusika anapokuwa na madhara makubwa.
Je, Mwanamke Anakuwa Na Dalili Gani Baada Ya Mtoto Kufia Tumboni?
Kama una homa, au kutokwa damu, baridi au maumivu, hakikisha unafika hospitali haraka kwasababu hizi zinaweza kuwa dalili za maambukizi.
Je, Mwanamke Anaweza Kunyonyesha Baada Ya Mtoto Kufia Tumboni?
Baada ya kondo kutoka nje, homoni zinazozarisha maziwa zinaweza kuchochewa. Mwanamke anaweza kuanza kutokwa na maziwa kwenye matiti yake. Endapo kama huna tatizo la msukumo mkubwa wa damu, basi unaweza kutumia dawa inayoitwa dopamine agonist ambayo inaweza kukusaidia kuzuia matiti yako yasitoe maziwa. Pia unaweza kutumia njia za tiba asili ili kuzuia matiti yasitoa maziwa.
Je, Hali Ya Mtoto Kufia Tumboni Inaweza Kumfanya Mwanamke Asipate Ujauzito Tena?
Hapana, mtoto kufia tumboni haiwezi kumfanya mwanamke kushindwa kupata ujauzito tena kitendo hicho hakiashirii kuwa huenda ana tatizo tumboni mwake.
Je, Tatizo Hili Hufanyiwa Kipimo Vipi?
Kwa kawaida, utagundua kuwa mtoto wako hachezi tumboni kama inavyotakiwa kuwa. Kipimo cha ultrasound kitathibitisha endapo kama mtoto amekufa.
Je, Unawezaje Kugundua Nini Kilichosababisha Mtoto Kufia tumboni?
Ili kubaini kisababishi hicho, tabibu au muhudumu wako wa afya atafanya moja ya mambo kama haya yafuatayo:
- Kupima Damu: Kipimo cha damu kitaonyesha endapo kama una tatizo la msukumo mkubwa wa damu, kisukari au asidi nyingi kwenye damu.
- Kipimo Cha Kitovu, Membreni Na Kondo: Tishu hizi huungana na kiumbe chako tumboni. Hali yoyo mbaya inapotokea inaweza kuzia kiumbe kisipokee hewa ya oksijeni, damu na virutubishi.
- Vipimo Kwa Ajili Ya Maambukizi: Tabibu atachukua sampuli ya mkojo, damu, au seli kutoka ukeni mwako au mlango wa uzazi wako ili kupima maambukizi.
- Kipimo Cha Utendaji Kazi Wa Tezi Ya Thyroid: Kipimo hiki kitabaini ikiwa kama kuna kitu kibaya kwenye tezi yako ya thyroid.
NUKUU: Tabibu au muhudumuwako pia atakagua kumbukumbu za matibabu na mazingira yanayomzunuka mtoto aliyezariwa mfu. Kwa idhini yako, utafanyiwa kipimo(autopsy) kinachoweza kubaini chanzo cha mtoto kufia tumboni. Kipimo hiki ni cha upasuaji kinachotumiwa na daktari au tabibu mwenye ujuzi. Upasuaji hufanyika kwa umakini sana ili kuepusha uharibifu wowote, na upasuaji hurekebishwa baadaye.
Je, Nini Hutokea Baada Ya Mtoto Kufia Tumboni?
Kama mtoto wako akifa kabla hujafika katika chumba cha kujifungua(labor room), una mambo matatu ya kuchagua:
- Kutiwa uchungu ili ujifungue
- Kujifungua kwa njia ya asili
- Kufanyiwa upasuaji
Kutiwa Uchungu: Tabibu au mtoa huduma hupendekeza mjamzito kutiwa uchungu kama njia bora zaidi baada ya mtoto kufia tumboni. Njia hii inapaswa kufanya haraka zaidi endapo kama mama;
- Ana shikizo la damu la juu sana
- Ana maambukizi mabaya zaidi
- Ana maji tumboni yaliyomzunguka mtoto
- Ana tatizo lolote la kuganda kwa damu
- Ametiwa uchungu kwa kutumia dawa zinazogawanywa kwa moja ya njia tano;
- Kidonge kuingizwa ukeni
- Mafuta(gel) kupakwa ukeni
- Kuwekewa drip kwenye mishipa ya damu
- Kumeza kidonge
Kuzaa Kwa Njia Ya Asili: Kitendo cha kusubiri muda wa kujifungua uwadie kwa njia ya asili huwa ni hiari yako, lakini kadiri muda unavyozidi kwenda, mwili wa mtoto wako unaweza kuharibikia tumboni. Mtoto anaweza kuonekana tofauti kuliko unavyotarajia. Ile hali ya kuharibika kwa mwili wa mtoto inaweza kusababisha ugumu fulani wa kuweza kujua chanzo cha mauti ya mtoto.
Kuzaa Kwa Njia Ya Upasuaji: Kuzaa kwa njia ya upasuaji huwa haipendekezwi kwasababu sio njia salama kama ilivyo njia ya kawaida au ya asili au ile ya kutiwa uchungu.
Je, Nini Hutokea Baada Ya Mtoto Aliyefia Tumboni Kuzaliwa?
Mama utakuwa tiyari kubeba mtoto wako, na muhudumu wako atakuruhusu muda wote kadiri unavyohitaji kuutumia kwa mwanao. Unaweza usijisikie vizuri kwa wazo hili kwanza.
NUKUU: Unaweza kuhitaji kuomba kumbukumbu zozote na kumbukumbu za mtoto wako, kama vile blanketi, nywele za mwanao, kadi ya hospitali, nk. Unaweza kuchukua picha. Hii inaweza pia kuwa na mashaka, lakini hii inaweza kuwa mali itakayo tunzwa badaye na inaweza kukusaidia wewe wakati wa kipindi cha majonzi.
Je, Unahitaji Huduma?
Ikiwa kama uliwahi kufanyiwa vipimo na ikaonekana una visababishi vya mtoto kufia tumboni, kama vile maambukizi ya magonjwa ya zinaa, UTI, nk, basi tupigie simu kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626.
Pia unaweza kutuma namba zako za WHATSAP au TELEGRAM ili uweze kuunganishwa na jukwaa au group letu uzidi kujifunza kwa kina habari ya fya.
Karibuni sana!