ZIJUE SABABU ZINAZOMFANYA MWANAUME KUPUNGUKIWA NGUVU ZA KIUME. JE, NINI MADHARA YAKE?

Upungufu wa nguvu za kiume ni kutokuwa na uwezo wa kudindisha au kusimamisha uume kwa ajili ya kufanya tendo la ndoa. Uume unapokuwa unadindisha vizuri halafu siku zingine unaishiwa nguvu, hilo linaweza lisiwe tatizo sana. Lakini kama upungufu wa nguvu za kiume utakuwa tatizo endelevu, hata hivyo unaweza kusababisha msongo wa mawazo, na inaweza kuathiri ujasiri wako na kuchangia matatizo katika mahusiano ya ndoa katika familia yako.

NUKUU: Matatizo yanayojitokeza kwenye nguvu za kiume yanaweza pia kuwa ishara za tatizo la msingi la afya yako ambalo linahitaji matibabu pamoja na sababu hatarishi ya ugonjwa wa moyo.

Kama una tatizo la la kupungukiwa nguvu za kiume, nakushauri ufike hospitali ukapate ushauri kwa daktari hata kama unaaibika. Wakati mwingine kutibu tatizo la msingi inatosha  kurejesha uwezo wa uume kudindisha. Hivyo basi, matibabu kwa njia ya mimea ya asili inatosha kabisa kuondoa tatizo hili.

Je, Dalili Zake Zinakuwaje?

Dalili za upungufu wa nguvu za kiume zinaweza kuendeleza mambo mengine mabaya kama haya yafuatayo;

  • Kupata shida ya kutokudindisha
  • Tatizo la kutokusimamisha
  • Kupungua kwa hamu au hisia ya tendo la ndoa

Je, Unapaswa Umuone Daktari Kipindi Gani?

Kufika hospitalini na kuonana na daktari ni jambo zuri sana unapoanza pale unapokuwa na matatizo ya kukosa nguvu za kiume. Muone daktari wako ikiwa kama:

  • Una matatizo ya nguvu za kiume au matatizo ya uzazi kama vile kufika kileleni mapema au kuchelewa kufika kileleni.
  • Una ugonjwa wa kisukari, moyo au tatizo jingine linalopelekea kukosa nguvu za kiume.

Je, Visababishi Vyake Vinakuwaje?

Hisia za tendo la ndoa kwa mwanaume ni mchakato tatanishi ambao hujumuisha ubongo, homoni au vichochezi, hisia, neva za fahamu, misuli pamoja na mishipa ya damu. Hali ya uume kushindwa kusimama inaweza kutokana na viungo hivyo vya mwili nilivyovitaja. Vile vile, msongo wa mawazo pamoja na afya ya ubongo inaweza kusababisha au kuharibu uume na kushindwa kusimama.

NUKUU: Wakati mwingine mchanganyiko wa matatizo ya mwili na ubongo husababisha kupungua kwa nguvu za kiume. Kwa mfano, tatizo kubwa la mwili ambalo hupunguza hamu ya tendo la ndoa linaweza kusababisha wasiwasi katika kutengeneza uwezo wa uume kusimama. Wasiwasi au mashaka yanapojitokeza yanaweza kupelekea kuishiwa kabisa nguvu za kiume.

Je, Ni Sababu Zipi Za Mwili Zinazopelekea Uume Kuishiwa Nguvu?

Katika hali nyingi, uume kuishiwa nguvu husababishwa na jambo la mwili. Visababishi vya kawaida ni pamoja na;

  1. Umri

Umri unapokuwa mkubwa nao pia ni chanzo cha mwanaume kupungukiwa nguvu za kiume. Kwa watu wenye umri mkubwa miili yao huzeeka. Inamaanisha kwamba utendaji kazi katika sehemu za miili yao hasa utendaji kazi wa mfumo wa uzazi pia hupungukiwa.

 

 

NUKUU: Kiwango cha vichocheo vya mwanaume(homoni), nacho hushuka kiwango chake na hivyo kusababisha hamu ya tendo la ndoa na uume kusimama kushindwa kufanya kazi kama inavyostahili.

  1. Matatizo Ya Ubongo

 

Ubongo hufanya kazi vizuri sana katika kusafirisha ishara za hisia au nyege na hivyo kuufanya uume kusimama. Kwahiyo, matatizo ya ubongo ni mojawapo ya vyanzo vya uume kushindwa kusimama. Hali yoyote ya ubongo kama vile msongo wa mawazo, matatizo ya kikazi au nyumbani kwenye familia ambayo hupelekea mwanaume kuwa na mashaka au wasiwasi kwa muda mrefu, yaweza kuwa kizuizi cha uume kuweza kusimama.

Mbali na hivyo, kutokuwa na ujasiri au kuhisi mashaka kabla na wakati wa tendo la ndoa kunaweza kusababisha uume kushindwa kusimama.

  1. Magonjwa

 

Wanaume wenye baadhi ya magonjwa kama vile magonjwa ya moyo, kisukari na magonjwa fulani ya meno yanayoathiri mishipa ya damu pamoja na neva za fahamu, wanaweza kupatwa na tatizo la kuishiwa nguvu za uume.

NUKUU: Kulingana na utafiti wa kisayansi, ugonjwa wa shinikizo la juu la damu unaweza kuwa chanzo kikubwa cha mwanaume kupungukiwa nguvu za kiume. Uume unahitaji kupata damu nyingi ya kutosha ili uweze kusimama. Hata hivyo, mishipa inayosambaza damu kwenye uume wa mwanaume mwenye ugonjwa wa shinikizo la juu la damu(High Blood Pressure) itaharibiwa na hivyo, damu isiyotosha kwenye uume husababisha uume kushindwa kudindisha.

  1. Utumiaji Wa Madawa Fulani

 

Unapokuwa na baadhi ya magonjwa, utumiaji wa madawa fulani hulazimu kabisa. Hata hivyo, mara nyingi husababisha madhara kwa muhusika. Kwa mfano, kutumia baadhi ya madawa kama vile madawa ya ugonjwa wa moyo, vidonge kwa ajili ya kuzuia ugonjwa wa kifafa, nk. Hupelekea kuwepo madhara yasiyotarajiwa yanayomfanya mwanaume kushindwa kufanya tendo la ndoa vizuri.

NUKUU: Madawa haya yanaweza kubadirisha baadhi ya kemikali kwenye mfumo wa damu, na hivyo humfanya mwanaume kushindwa kuwa na hisia au hamu ya tendo la ndoa.

  1. Maisha Yasiyokuwa Yenye Afya

 

Maisha yasiyo yenye afya mara nyingi husababisha magonjwa mengi kama vile kisukari, shinikizo la juu la damu, magonjwa ya moyo, nk. Hata pia husababisha baadhi ya matatizo katika mfumo wa uzazi kama vile uume kushindwa kudindisha. Unapaswa ufahamu kwamba, ulaji wa vyakula vibaya visivyokuwa na afya bora kama vile vyakula vyenye mafuta mengi au vya kuungwa sana, nyama nyekundu, ugali wa sembe, mikate, chapati, maandazi, chips, nk, vinaweza kuathiri viungo vya mwili hasa mfumo wa uzazi wa mwanaume.

NUKUU: Wanaume wanaopenda pombe sana, sigara, sio kwamba miili yao tu huharibika bali pia uwezo wao wa ubongo hupoteza nguvu. Pombe naomba msipende kuitumia sana ikiwezekana achana na pombe.

Je, Madhara Yake Yanakuwaje?

Madhara yatokanayo na upungufu wa nguvu za kiume huwa ni nyingi kidogo nazo huwa ni pamoja na:

  • Kutomridhisha mwanamke wakati wa tendo la ndoa
  • Msongo wa mawazo au wasiwasi
  • Kuwa na aibu
  • Matatizo ya mahusiano
  • Kutokumpatia mimba au ujauzito mke wako
  • Heshima ya ndani ya nyumba kutoweka na ndoa kuvunjika
  • Mwanaume mzembe kufanya mazoezi huufanya mwili wake mara nyingi kuwa kwenye uchovu. Hali hii inaweza kuathiri uume kuchelewa kudindisha au hata kupelekea kupungua kwa hamu ya tendo la ndoa.

 

Je, Unahitaji Kuondoa Tatizo Hili?

 

James Herbal Clinic tuna dawa nzuri kabisa za asili zenye uwezo mkubwa wa kuondoa vyanzo vya tatizo hili. Unahitaji kuwasiliana nasi, tupigie kwa namba hizi: 0752 389 252 au 0712 181 626-Arusha Mbauda.

NENO LA FARAJA:  Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu. Wafilipi 4:13.

 

Pia unahitaji kujiunga na darasa letu au Group letu katika mtandao wa WHATSSAP au TELEGRAM, basi unaweza kutuma namba yako tukaweza kukuunganisha na Group letu.

Karibuni sana!

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *