ZIJUE SABABU ZINAZOPELEKEA KUVIMBA KWA TONSES(MAFINDOFINDO) NA TISHU LAINI PUANI (ADENOIDS).

Je, Tonses Na TishuLlaini(Adenoids)  Ni Nini?

Tonses(mafindofindo) na Adenoids(tishu laini)  ni moja kati ya mtandao wa viungo muhimu mwilini vinavyo husika na kinga dhidi ya maambukizi ya virusi, bakteria ambao hujitokeza ili kuingia puani au mdomoni, lakini tishu  hizi za limfu ndizo huzuia bakteria au virusi wasiweze kuingia ndani zaidi. Kwa bahati mbaya, wakati mwingine vinaweza kuathiriwa au kusababisha matatizo kutokana na kuvimba na kuwa vikubwa sana.

Tonses ni viungo  vinavyokuwa  katika koo la hewa, kimoja upande wa kulia, na kingine upande wa kushoto.  Adenoids ni tishu laini zinazokuwa juu ya koo la hewa nyuma ya pua na paa la kinywa. Huwa hazionekani unapozitazama kwa macho tu mdomoni au puani bila kutumia vifaa maalumu.

Je, Nini Kinachosababisha Kuvimba Kwa Mafindofindo(Tonsillitis)?

Mtu anaweza kupata ugonjwa wa mafindofindo kutokana na kuongezaka kwa umbile la tezi ya pua ambapo kuna uhusiano mkubwa na maambukizi ya  virusi na bakteria kooni hali ambayo hupelekea mafindofindo kuongezeka ukubwa.

Kila mtu na ukuwaji wake wa mwili, lakini wapo ambao wanapata mafindofindo kutokana na utumiaji wa vitu vifuatavyo:

  • Kunywa vinywaji vya baridi kama vile maji, soda, juisi, barafu au ice-cream,nk
  • Kuwa sehemu yenye vumbi sana muda mrefu
  • Pilipili na vitu vikali kama vile embe mbichi, limau, nk.
  • Upungufu wa seli nyeupe za damu katika mwili ambazo hizi ndio hupingana na vidudu vyote vyenye kuleta maradhi ndani ya mwili hasa vinaposhindwa kufanya kazi (lymph) zinavimba na kusababisha mafindofindo au Tonsilitis.

Je, Nini Kinachosababisha Kuvimba Kwa Tishu Laini(Adenoids)?

Tishu laini(adenoids) zinaweza kuvimba  kwa mtoto wako kutokana na sababu mbalimbali. Inaweza kuwa mtoto alipata uvimbe huo wakati anapozaliwa. Au tishu laini zinaweza pia kuvimba pale zinapojaribu kupambana na maambukizi. Zinaweza kubaki zikiwa zimevimba hata baada ya maambukizi kutoweka.

Je, Dalili Zake Zinakuwaje?

Ugonjwa wa mafindofindo(tonsillitis) kwa kawaida huwaathiri watoto wadogo wenye umri kuanza miaka 5-15 na hata watu wakubwa pia. Dalili za ugonjwa huu zinazoambatana na vidonda kooni huwa kama ifuatavyo:

  • Uvimbe wa tezi unaodhihirika  mbele ya shingo,
  • Homa kali,
  • Kichwa kuuma,
  • Mafua,
  • Utando mweupe au wa njano kwenye vivimbe hivyo
  • Harufu mbaya kinywani,
  • Kufifia au kupotea kwa sauti na mwili kuchoka,
  • Kushindwa kumeza chakula
  • Uchovu mkubwa na usingizi usioisha,
  • Koo kuuma(madonda kooni) unaweza  kudhani ni dalili za Malaria.
  • Vidonda kooni ambavyo huambatana na dalili nyingine kama vile mafua, kupiga chafya na kikohozi mara, au maumivu kwenye masikio.

Tonsils & Adenoids - Dr. Rande Lazar

NUKUU: Kama  tonses au tishu laini puani zikivimba na kuwa kubwa, basi inaweza kumfanya muhusika kushindwa kupumulia puani, au kushindwa kupata usingizi usiku anapolala. Dalili zingine za tishu laini au tonses kuvimba ni pamoja na:

  • Kupumulia mdomoni badala ya puani muda wote
  • Sauti ya puani kuziba wakati mtu anapoongea
  • Kutokwa na makamasi mepesi
  • Kupumua kwa kelele wakati wa mchana
  • Maambukizi ya kujirudiaruida masikioni
  • Kukoroma wakati wa usiku
  • Kutokutulia kitandani wakati wa kulala usiku

Uonapo dalili kama vile matatizo sikioni, puani au kooni, basi unapaswa uonane na mtaalam viungo hivyo haraka sana ili uweze kupata uchunguzi na ushauri ili upate tiba.

 

Nipende kuishia hapa ndugu msomaji katika makala yetu hii, nikaribishe kipindi cha maswali na maoni yako. Karibu sana!

Pia unaweza kutuma namba yako ya WHATSAPP ukaunganishwa na DARASA letu ili uweze kupata masomo mengine zaidi juu ya afya.

Unahitaji huduma? Wasiliana nasi kupitia namba hizi: 0752389252 au 0712181626.

 

Arusha-Mbauda Maua.

Karibuni sana!

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *