Ni kawaida kushangaa huenda rangi au muonekano wa uchafu unaotoka ukeni ni wa kawaida au unahitaji kuchunguzwa. Uchafu unaotoka ukeni unaweza kuwa ni rangi nyingi, na ishara mbalimbali za afya ya mwili wako.

Je, Uchafu Unaotoka Ukeni Ni Nini?
Uchafu unaotoka ukeni ni majimaji yaliyotengenezwa kutokana na tezi ndogo ndani ya uke pamoja na mlango au shingo ya kizazi. Ute huu huvuja ukeni kila siku ili kuondoa seli zilizochakaa pamoja na vitu vilivyoharibika, ili kuutunza uke pamoja na njia ya uzazi uwe safi na wenye afya.
Kiwango cha uchafu unaotoka ukeni kinaweza kutofautiana kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine. Rangi, muonekano pamoja na kiwango kinaweza pia kubadirika siku baada ya siku, kutegemeana na mahali mtu alivyo kwenye mzunguko wake wa hedhi:
- Siku Ya 1-5
Mwanzoni mwa mzunguko wa hedhi, uchafu unaotoka ukeni kwa kawaida huwa ni mwekundu au wenye damu, kadiri mwili unapojibandua kwenye mfuko wa uzazi.
- Siku Ya 6-14
Ikifuatana na kipindi cha hedhi, mwanamke anaweza kuona uchafu kidogo ukeni kuliko kawaida. Yai linapoanza kukua na kukomaa, uteute wa mlango wa uzazi utakuwa wa kijivu, mweupe au wanjano. Unaweza kuwa wenye kunata au kuvutika.
- Siku Ya 14-25
Siku chache kabla ya yai kupevuka, uteute utakuwa mwepesi na wenye kuteleza, kama ute wa yai la kuku. Baada ya yai kupevuka, uteute huo utabadirika na kuwa mzito, mweupe au wa njano, na wenye kunata.
- Siku Ya 25-28
Ute wa shingo ya kizazi utakuwa mwepesi, na mwanamke atauona kidogo, kabla hajapata hedhi nyingine.
- Ranga Nyekundu
Rangi nyekundu ya hedhi inaweza kutofautiana kutoka rangi yenye kung’aa na kuwa nyekundu inayoelekea kuwa nyeusi. Uchafu unaotoka ukeni wenye rangi nyekundu kwa kawaida ni matokeo ya kuingia hedhini.

NUKUU: Kipindi cha hedhi hutokea, katikati au kila baada ya siku 28, ingawa kiwango cha kawaida huwa ni siku 21 na 35. Kwa kawaida hedhi hukaa kwa muda wa siku 3-5.
Mwanamke yeyote anayepata hedhi mara mbili kwa mwezi anapaswa kufika hospitali kuonana na daktari. Ingawa kuna vivimbe vingi vinavyomfanya mwanamke kutokwa na damu, lakini wakati mwingine huashiria kuwa ana ugonjwa.
Yeyote aliyefikia ukomo wa hedhi na hajaona hedhi karibia mwaka mmoja, na endapo akiona damu inamtoka ukeni, basi anapaswa afike hospitali bila kuchelewa. Wakati mwingine inaweza kuwa ni ishara ya matatizo ya saratani ya tumbo la uzazi.
- Rangi Nyeupe
Uchafu wenye rangi nyeupe unaweza kutoka ukiwa kama maziwa mgando au mwepesi wenye rangi ya njano. Kama mwanamke hana dalili zingine, basi uchafu wenye rangi nyeupe unaweza kuwa ishara ya ute wenye unaoweza kulanisha uke.

NUKUU: Hata hivyo, kama uchafu unaotoka ukeni ukiwa na rangi nyeupe na una muonekano kama maziwa mgando au umeambatana na harufu mbaya, basi unaweza kuashiria maambukizi. Kwahiyo unapaswa kuonana na daktari.
Uchafu mzito, wenye kunata, wenye rangi nyeupe, tena wenye harufu kali, mara nyingi huambatana na maambukizi ya fangasi, ambao unaweza kusababisha muwasho ukeni.
- Uchafu Wenye Rangi Ya Njano Au Kijani
Kama uchafu unaotoka ukeni ukiwa na rangi ya njano kwa mbali, unaweza usionyeshe kuwa ni tatizo. Hii inaweza hasa kuonekana kama rangi itakuwa na mabadiriko kutokana na chakula au madawa ya tiba mbadala unayotumia.

- Damu Yenye Rangi Ya Pink
Uchafu unaotoka ukeni ukiwa na rangi ya pink, inaweza kuwa yenye kung’aa au pink sana. Kwa kawaida huwa ni uchafu wenye damu kwa mbali. Uchafu wenye rangi ya pink kwa kawaida hutokea na matone matone kabla hedhi haijaanza kutoka. Hata hivyo, inaweza pia kuwa ishara ya damu kutoka wakati wa ujauzito.
Baadhi ya watu hutokewa na matone ya damu baada ya yai kupevuka, hali ambayo inaweza kusababisha kutokwa na uchafu wenye rangi ya pink.

NUKUU: Uchafu unaweza kuwa na rangi ya pink baada ya kufanya tendo la ndoa kama tendo la ndoa limesababisha michubuko au miwasho ukeni au kwenye shingo ya kizazi.
- Ute Msafi
Uchafu wa kawaida ukeni huwa ni msafi au mweupe. Unaweza kuwa wenye kuteleza au wenye muonekano kama ute wa yai la kuku.
Mwanamke anaweza kutokwa na ute msafi, wenye kuvutika kabla yai halijapevuka, au wakati mwanamke anapata hisia, na wakati wa ujauzito.
- Uchafu Wenye Rangi Ya Ukijivu
Uchafu wenye rangi ya ukijivu unaotoka ukeni huwa sio salama, na unaweza kuwa ni dalili ya maambukizi ya bakteria wa kawaida ukeni. Mambukizi haya husababisha dalili kama hizi zifuatazo:
- Muwasho ukeni
- Kutokwa na uchafu wenye harufu mbaya
- Mashafu ya ndani ya uke kuwa mekundu
- Njia ya uke kuwa nyekundu.
Yeyote anayetokwa na uchafu wenye rangi ya kijivu anapaswa kupata vipimo haraka hospitalini ili kuanza tiba.
Je, Unaweza Kufika Hospitali Kipindi Gani?
Fika hospitali uonane na daktari ikiwa kama uchafu unaotoka ukeni utakuwa na harufu mbaya na rangi mbaya. Mgonjwa pia anapaswa apate tiba ikiwa kama anaona dalili ukeni kama hizi:
- Muwasho ukeni
- Kuhisi maumivu wakati wa tendo la ndoa
- Kupata hedhi mara 2 kwa mwezi
- Kutokwa na uchafu wenye rangi ya njano au kijani
- Kutokwa uchafu ukeni wenye harufu mbaya
- Kuhisi hali ya kuwaka moto wakati unapokojoa

Daktari atakufanyia vipimo vya ultrasound, nk. Anaweza pia kuchukua sampuli ya uchafu ukeni kwa ajili ya kufanya kipimo.
Nipende kuishia hapa katika makala hii wapendwa, nikaribishe kipindi cha maswali, na tutaonana kipindi kijacho.
Pia unaweza kutuma namba yako ya whatsap ukaweza kuunganishwa kwenye Group letu ili upate huduma na uendelee na elimu ya afya.
Unahitaji huduma, basi wasiliana nasi kupitia namba hizi: 0752389252 au 0712181626.
Arusha-Mbauda.
Karibuni sana!