Maumivu makali wakati wa tendo la ndoa yanaweza kutokea kwa sababu mbalimbali kutokana na viungo vya mwili au kuwa na hofu Fulani. Watu wengi wamekuwa wakipatwa na maumivu makali wakati Fulani katika maisha yao, pale wanapoanza kujamiiana.
Kuhisi maumivu makali wakati wa kujamiiana kitaalam tunaita “dyspareunia”. Ni maumivu ya muda mrefu au ya mara kwa mara sehemu za siri ambayo hutokea kabla, wakati au baada ya kujamiiana. Hakikisha unafika kituo cha afya haraka unapohisi maumivu makali wakati wa kushiriki tendo la ndoa. Kumbuka tendop la ndoa ni furaha sio kero wala huzuni.
Je, Dalili Zake Zinakuwaje?
Ikiwa kama unahisi maumivu makali wakati unaposhiriki tendo la ndoa, basi lazima uhisi:
- Maumivu pale tu uume unapoingia
- Maumivu kila unapoingiza kitu chochote, ikiwa pamoja na pedi
- Maumivu makali wakati mwanaume anaposukuma uume ndani
- Maumivu kama moto vile au ya kuchoma
- Maumivu ya muda mrefu baada ya kushiriki tendo la ndoa
Ikiwa una maumivu ya mara kwa mara wakati wa kushiriki tendo la ndoa, basi fika kituo cha afya ongea na mtaalamu wako wa afya. Kutibu tatizo kunaweza kusaidia maisha yako pamoja na kizazi chako, ukaribu wako na mweza wako pamoja sura yako binafsi.
Je, Vyanzo Vyake Ni Nini?
Sababu za kimwili za kujamiiana huku ukihisi maumivu makali, hutofautiana, kulingana na kama maumivu hutokea wakati uume unapoingia au unaposukumwa kuzama ndani kwa kina. Sababu za kihisia kama vile msongo wa mawazo zinaweza kuhusishwa na aina nyingi za maumivu makali wakati wa tendo la ndoa.
Maumivu Wakati Uume Unapoingia
Maumivu wakati uume unapopenya yanaweza kuambatana na mambo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na:
- Kutokuwa Na Ute Wa Kutosha: Hii mara nyingi hutokana na kutokuwa na hisia nyingi za kutosha, au msisimko, au kutokuandaliwa vyema, au kutokuwa na mahaba hata kidogo. Kupungua kwa viwango vya homoni estrojeni baada ya kukoma hedhi au kuzaa au wakati wa kunyonyesha, pia kunaweza kuwa sababu. Madawa fulani yanaweza kuathiri hamu ya tendo la ndoa au msisimko. Hali hii inaweza kupunguza ute utelezi, uke kuwa mkavu na kufanya kuhisi maumivu makali wakati wa tendo la ndoa. Madawa hayo ni pamoja na madawa kwa ajili yaa msongo wa mawazo, dawa za shinikizo la damu(presha ya kupanda), madawa ya uzazi wa mpango, nk.
- Uvimbe, Maambukizi Au Matatizo Ya Ngozi: Maambukizi katika eneo la uzazi au njia ya mkojo yanaweza kusababisha kuhisi maumivu makali wakati unaposhiriki tendo la ndoa. Maambukizi katika via vya uzazi (PID) yanaweza kumfanya mwanamke kuhisi maumivu makali wakati wa kushiri tendo la ndoa
NUKUU: Fungua hapa ili ujue zaidi: Haya Ndio Madhara Ya Maambukizi Ya PID
Misuli hii ya uke isiyo tanuka inaweza kufanya uume kushindwa kupenya na kuingia ukeni, na hivyo kuhisi maumivu makali.
- Tatizo Lililopo Tangu Kuzaliwa Kwako: Kutokuwa na uke uliokamilika, au kuwa na utando unaoziba mwanya wa uke, unaoitwa “imperforate hymen”, kunaweza kusababisha kujamiiana huku ukihisi maumivu makali.
Maumivu Kwenye Kina Cha Ndani.
Maumivu kwenye kina cha ndani kwa kawaida hutokea pale uume unapozama kwa ndani Zaidi. Hali inaweza kuwa mbaya Zaidi katika maeneo Fulani. Vyanzo ni pamoja na:
Mambo Ya Muhemko
Hisia zina ambatana sana na ngono, kwa hivyo zinaweza kuchukua jukumu katika maumivu ya ngono. Sababu za kihisia ni pamoja na:
- Masuala Ya Kisaikolojia: Wasiwasi, msongo wa mawazo, kuhusiana na muonekano wa kimwili, hofu ya kuwa karibu na urafiki au matatizo ya mahusiano yanaweza kuchangia kuwa na kiwango cha chini cha msisimko na kusababisha usumbufu au maumivu.
- Msongo Wa Mawazo: Misuli yako ya kwenye nyonga hunekana kukaza kutokana na maisha ya msongo wa mawazo. Hii inaweza kuchangia maumivu wakati wa kujamiiana.
Inaweza kuwa vigumu kusema kuwa muhemko unahusiana na maumivu makali wakati wa kujamiiana. Maumivu ya awali yanaweza kusababisha hofu ya maumivu ya mara kwa mara, na kuifanya kuwa vigumu kupumzika, hali ambayo inaweza kusababisha maumivu zaidi. Unaweza kuanza kuepuka kufanya ngono ikiwa kama unahisi maumivu.
Je, Suluhisho Lake Ni Nini?
James Herbal Clinic tunazo dawa nzuri zenye uwezo mkubwa wa kuondoa vyanzo vya maumivu makali wakati wa tendo la ndoa.
Mpendwa msomaji makala yetu inaishia hapa, naomba nikaribishe kipindi chako cha maswali na maoni yako. Pia unaweza kutuma namba yako ya WhatsAp ili uweze kujiunga na Group letu la mafunzo ya kila siku juu ya afya.
Je, Unahitaji huduma? Wasiliana nasi Kwa namba hizi: 0768 559 670 au 0712181626,
Arusha-Mbauda.
Karibu sana.