MADHARA YA MAMBUKZII YA UGONJWA WA PID

Ugonjwa wa maambukizi katika via vya uzazi(PID) ni maambukizi ya mirija ya mayai(fallopian tubes), vifuko vya mayai(ovaries), mfuko wa kizazi(uterus) pamoja na shingo ya kizazi(cervix). Ugonjwa huu usipotibiwa unaweza kusababisha makovu ama tishu kuoteana ikiwa na mkusanyiko wa ute mchafu kama vile usaha kwenye mirija ya mayai, na hivyo kuharibu viungo vyako vya uzazi.

Miongoni mwa wanawake 8 wenye ugonjwa wa maambukizi katika via vya uzazi(PID),  mmoja anaweza kupata tatizo la kutoshika ujauzito au kuwa mgumba daima.

830+ Pelvic Inflammatory Disease Stock Photos, Pictures & Royalty-Free  Images - iStock | Pelvis, Irritable bowel syndrome, Endometriosis

NUKUU: Ugonjwa huu kama ilivyo kawaida hutokana na maambukizi katika via vya uzazi. Hali hii hujitokeza pindi bakteria wanapoingia kupitia uke au shingo ya kizazi na kuenea mpaka kwenye mfuko wa kizazi(uterus), mirija ya mayi, au vifuko vya mayai(ovaries).  Bakteria hawa hutokana na magonjwa ya zinaa kama vile pangusa(Chlamydia), kisonono(gonorrhea), nk. Bakteria wa magonjwa ya zinaa humpata muhusika ikiwa kama atafanya tendo la ndoa bila kutumia kinga.

Ni mara chache sana ugonjwa wa PID unaweza kumpata mwanamke baada ya kujifungua mtoto, mimba kuharibika, kutoa mimba, ama kuingiziwa chombo kama vile kipimo ukeni.

Mwanamke yuko katika hatari ya kupatwa na ugonjwa huu ikiwa kama

  • Ana ugonjwa wa maambukizi lakini hajazingatia kuutibu
  • Anapoanza tendo la ndoa chini ya umri wa miaka 18
  • Ana wapenzi zaidi ya mmoja
  • Ana mpenzi mwenye zaidi ya mpenzi mmoja
  • Ana mpenzi aliyewahi kupatwa na maambukizi ya PID hapo mwanzo

Katika makala yetu ya mwanzo tuliona dalili za PID anazozipata mwanamke huwa kama ifuatavyo:

  • Maumivu ya nyonga, tumbo la chini au kiuno
  • Maumivu wakati wa tendo la ndoa
  • Kutokwa na uchafu mwingi ukeni tena wenye harufu mbaya
  • Maumivu au kushindwa kukojoa
  • Mzunguko wa hedhi wa kubadirikabadirika
  • Maumivu ya tumbo wakati wa hedhi ambayo huwa makali kuliko kawaida
  • Kuhisi homa au baridi
  • Kuhisi kichefuchefu au kutapika
  • Mwili kuchoka

Je, Nini Madhara Ya PID Isipotibiwa Mapema?

Ikiwa kama ugonjwa huu hautatibiwa, basi unaweza kusababisha vidonda ama makovu kwenye viungo vyako vya uzazi ambayo yanaweza kusababisha:

  • Maumivu makali ya nyonga
  • Kutunga mimba nje ya kizazi
  • Ugumba
  • Usaha kwenye mirija au vifuko vya mayai

NUKUU: Madhara ya maambukizi haya yanaweza pia kuenea mpaka kwenye mzunguko wa damu au katika sehemu zingine za mwili wako. Yafaa sana kumuona daktari mapema ikiwa kama unahisi una tatizo hili la PID. Dawa zetu aina ya MULTICURE POWDER, na FRESH HERB zitakusaidia sana katika kuondoa tatizo hili na kuzuia kabisa madhara katika mfumo wako wa uzazi.

Je, Unawezaje Kujikinga Na Ugonjwa Wa PID?

Unaweza kujikinga na ugonjwa huu kwa kufanya tendo la ndoa kwa kutumia kinga na kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu. .

Je, Unawezaje Kupata Vipimo?

  1. Kupiga bomba: Usipende kupiga bomba, kwani kwa kutumia njia hii unaweza kusababisha kuharibu uwiano wa bakteria katika uke wako.
  2. Kupima magonjwa ya zinaa: Unapopima magonjwa ya zinaa na kuanza kuyatibu mapema, kunaweza kukusaidia usipatwe na matatizo ya PID.
  3. Kuwa msafi: Unapokuwa ukitawaza au kusafisha uke wako, hakikisha unafuta uke wako kutoka mbele kwenda nyuma baada ya kujisaidia haja kubwa ili kuzuia kuenea kwa bakteria walioko sehemu ya njia ya haja kubwa wasiingie katika eneo la uke.

NUKUU: Madaktari hupima ugonjwa wa maambukizi katika via vya uzazi(PID), kwa kuangalia dalili zilizopo, kama vile kupima mkojo, uchafu unaotoka ukeni, kupiga picha kwenye nyonga, nk.

Wakati wa kupiga picha kwenye nyonga, daktari wako ataanza kwanza kuchunguza nyonga zako kwa kuangalia dalili au ishara za PID. Daktari wako hatimaye anaweza kutumia pamba ili kuchukua kielelezo kutoka kwenye uke wako ama shingo ya kizazi chako. Kielelezo hicho kitapimwa ndani ya maabara ili kubaini vimelea waliosababisha maambukizi hayo.

Ili kuhakikisha kipimo au kubaini maambukizi haya yameenea kwa ukubwa gani, basi daktari wako anapaswa apendekeze vipimo vingine tena kama vile:

  • Vipimo vya damu na mkojo: Vipimo hivi vitapima kiwango cha chembe zako nyeupe za damu, ambavyo vitaonyesha maambukizi, na kutia alama inayoonyesha uvimbe. Daktari wako pia sharti apendekeze vipimo vya HIV pamoja na maambukizi ya magonjwa ya zinaa, ambayo wakati mwingine huchangamana na PID.
  • Vipimo vya Ultrasound: Kipimo hiki hutumia sauti ya mawimbi ili kutengeneza umbo la viungo vyako vya uzazi.
  • Laparoscopy: Wakati unapofanyika utaratibu huu, daktari wako huingiza chombo chembamba chenye incha kali kwenye tumbo lako la chini ili kuangalia viungo vya nyonga yako.

Je, Matibabu Yake Yanafanyikaje?

Matibabu ya maambukizi katika via vya uzazi(PID) yanatakiwa yafanyike kama ifuatavyo:

  1. Matibabu Kwa Mwenzi Wako:

Ili kuzuia ugonjwa usiendelee, yafaa pia mwenzi wako apate vipimo na aanze tiba. Wapenzi wenye maambukizi haya wakati mwingine wanaweza wasionyeshe dalili zao.

  1. Kujizuia Kwa Muda:

Jizue kufanya tendo la ndoa mpaka pale matibabu ya PID yatakapokamilika, vipimo vitakapodhihirisha kuwa maambukizi yametoweka kabisa kwa wapenzi wote wawili, ikiwa kama ni mume na mke au mtu na mpenzi wake. James & Ferdinand Herbal Clinic tunapenda sana kuwashauri ndugu wapendwa kwasababu tatizo hili linazidi kukithiri katika familia kutokana na kutozingatia masharti ya matibabu.

NUKUU: Wanawake wengi wenye ugonjwa huu wanahitaji matibabu ya nje. Ili kuondoa na kuzuia madhara ya uvimbe ndani ya kizazi, mgonjwa unapaswa kutumia dawa za asili zenye uwezo mkubwa wa kuondoa matatizo hayo.

Hivyo naomba niihsie hapa, nikaribishe kipindi cha maswali na maoni yako. Pia unaweza kutuma namba yako ya WHATSAP ili uweze kuungana na kundi letu au GROUP letu la kujifunza mambo ya afya kwa muda endelevu.

Je, Unahitaji Huduma? Basi, wasiliana nasi kwa namba hizi: 0752389252/0712181626,

Arusha-Mbauda,

Karibuni sana!

2 thoughts on “MADHARA YA MAMBUKZII YA UGONJWA WA PID

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *