JE, UNAJUA CHANZO NA DALILI ZA MIMBA KUTUNGA NJE YA KIZAZI (ECTOPIC PREGNANCY)?

Katika wajawazito 100, mmoja anaweza kuwa na tatizo la kupata mimba nje ya kizazi. Hali hii humaanisha kwamba, yai lililorutubishwa tayari limeshachomekwa  katika tishu nje ya mfuko wa kizazi(uterus) badala ya ukuta wa mfuko wa kizazi(uterus). Yai hili huendelea kukua ndani ya kiini tete(embryo) ambapo limeshapachikwa. Mara nyingi mimba zinazotunga nje ya kizazi huwa haziwezi kukua mpaka mwisho wa ujauzito, na hivyo huweza kuleta hatari kwa afya ya mama hasa pale inapopasuka na kuvujisha damu tumboni mwa mama.
Je, Mimba Za Nje ya Kizazi Zinatokeaje?
Kwa kawaida mbegu ya kiume na yai la kike hukutana katika mirija ya uzazi (Fallopian tubes) na mimba hutungwa. Kiinitete husafri polepole kwenda kwenye mji wa uzazi ambako hujipandikiza kwenye ukuta wa uzazi na mimba huanza kukua. Katika ugonjwa huu wa mimba kuwa nje ya kizazi (ectopic pregnancy) mbegu ya kiume na yai huungana kutengeneza kiinitete. Badala ya kupandikizwa kwenye tumbo la uzazi, kiinitete huenda kujipandikiza sehemu nyingine tofauti na mji wa uzazi. Kinaweza kujipandikiza kwenye mirija ya uzazi, ovari, kwenye shingo ya uzazi na ndani ya tumbo (abdominal cavity). Mimba nyingi za nje ya kizazi hujipandikiza kwenye mirija ya uzazi ambapo huwa na hatari ya kupasuka kadri mimba inavyokua.
Mara chache sana mimba zinazotunga nje ya kizazi huweza kukua mpaka mwisho, nyingi huishia kupasuka na kuondolewa kwa upasuaji.
Je, Nini Husababisha Mimba Kutunga Nje ya Kizazi?
Zifuatazo ni baadhi ya sababu zinazochangia kutokea kwa mimba za nje ya kizazi.
·        Umri wa zaidi ya miaka 40 kwa mwanamke
·        Matumizi ya vijiti vya mji wa uzazi (intrauterine devices)
 
·        Kutoa mimba zaidi ya 3
 
·        Upasuaji wa mirija ya maji ya uzazi
 
·        Ugonjwa wa PID
Dalili Zake
Kufuatia wiki kadhaa baada ya kukosa siku zako za hedhi, hutokea dalili zifuatazo:
·        Kuchelewa kuingia katika hedhi au kupata maumivu ya tumbo chini ya kitovu au kiuno, ambayo yanaweza kuwa upande mmoja. Maumivu yanaweza kuja na kuacha, kuwa makali sana kiasi cha kushindwa kuvumilia.
·        Kutokwa damu ukeni, mara nyingi ikitoka kidogo kidogo. Inaweza kuwa nyepesi au nzito nyeusi.
Wakati mwingine unaweza usipate dalili zozote, tatizo likagunduliwa wakati wa kipimo cha ultrasound. Kuna baadhi ya watu wanaweza wasipate dalili zozote na mimba kukua nje ya kizazi mpaka wakati wa kujifungua kukaribia.

 

MATIBABU YAKE

James Herbal Clinic tunazo dawa nzuri za asiri zenye uwezo mkubwa wa kuondoa visababishi vya tatizo hili. Kwa mawasiliano tupigie: 0752389252 au 0712181626

Karibuni sana