YAJUE MADHARA YA MAAMBUKIZI YA MAGONJWA KATIKA VIA VYA UZAZI(PELVIC INFLAMMATORY DISEASES) AU PID.

Madhara kutokana na maambukizi ya PID ambayo hayajatibiwa yanaweza kuchukua miaka mingi kuendelea. Matokeo ya tatizo hili yanaweza kuwa yenye maumivu makali. Yanaweza pia kusababisha uharibifu wa kudumu katika viungo vya uzazi. Madhara yanaweza kusababisha hali ya ugumba. Mwanamke anapokaa muda mrefu na ugonjwa bila kutibiwa, ndipo nafasi kubwa ya matatizo ya ugonjwa huu hutokea kwa baadaye.

 

 

  1. Majipu

 

 

Mfumo kinga wa mwili hutengeneza usaha katika eneo la tishu iliyoambukizwa kwenye mirija ya uzazi au vifuko vya mayai. Hali hii inaitwa jipu. Jipu linaonekana kutungika muda mfupi baada ya maambukizi ya PID kuanza. Linaweza kuwa lenye maumivu sana, na linaweza likachukua miezi kadhaa ili liweze kupona lenyewe. Endapo kama halitatibiwa, basi linaweza kusababisha uharibifu wa kudumu na maumivu kwa ujumla.

Tokeo la picha la image of abscess surounding ovary

 

 

 

  1. Makovu Na Muunganiko

 

Maambukizi husababisha mirija na vifuko vya mayai kuvimba. Kama tishu iliyovimba hupona taratibu, basi ndipo kovu hujengeka. Mirija ya uzazi, vifuko vya mayai, mfuko wa uzazi, au viungo vingine vinaweza kuunganika pamoja kwa muunganiko wa tishu za makovu. NUKUU: Hali hii huitwa mshikamano. Kovu na mshikamano vinaweza kuwa vyenye maumivu makali na vinaweza kuvifanya viungo vya uzazi visiweze kufanya kazi vizuri.

Tokeo la picha la image of ovary and fallopian tubes stuck together

 

 

 

  1. Mirija Ya Uzazi Kuziba

 

 

 

 

Mirija ya uzazi inaweza kuziba kutokana na jipu, makovu kwenye tishu, au muunganiko wa tishu zenye makovu. Hali ya kuziba kwa mirija ya uzazi huzifanya mbegu za mwanaume kushindwa kulifikia yai ili kulirutbisha. Nyuzinyuzi zinazokuwa kwenye mirija ya uzazi pia huharibika. NUKUU: Nyuzinyuzi zilizoharibika haziwezi kusaidia mbegu na yai kuweza kusafiri kwenye mirija ya uzazi. Matatizo yote haya mawili hufanya kuwa vigumu sana mwanamke kupata ujauzito.

 

Picha inayohusiana

 

 

  1. Mimba Kutunga Nje Ya Uzazi

 

 

Mimba kutunga nje ya kizazi hutokea wakati uharibifu wa mrija wa uzazi unapolizuia yai lililorutubishwa lisiweze kusafiri kwenye mrija mpaka kwenye mfuko wa uzazi(uterus). Badala yake, kiinitete huanza kukua ndani ya mrija wa uzazi. Kumbuka mrija wa uzazi hauwezi kutanuka kama unavyokuwa mfuko wa uzazi. Wakati kiinitete kinapofikia ukubwa Fulani, basi mrija unaweza kupasuka. Hali hii inaweza kuwa ya kutisha kwa mama na ni hatari pia kwa kiumbe kinachokuwa tumboni.

Tokeo la picha la image of embryo trapped

 

 

  1. Kama Maambukizi Yakisambaa

 

 

 

Maambukizi ya PID yanaweza kusambaa katika maeneo mengine ya mwili. Bakteria wanaweza kutoka kwenye mirija ya uzazi na kuambukiza tumbo la chakula. Hali hii huitwa, “Peritonitis”. Karibu na viungo kama vile utumbo mpana pamoja na kibofu cha mkojo, vinaweza kushikamana pamoja kwa makovu ya tishu. Hali hii inaweza kusababisha maumivu na hivyo kuvifanya viungo visiweze kufanya kazi kwa usahihi.

Tokeo la picha la image of peritonitis

 

NUKUU: Ni mara chache sana maambukizi ya PID yanaweza pia kuingia kwenye mfumo wa damu. Maambukizi ya haya ya damu yanaweza kuwa mabaya na tena hatari.

 

 

Je, Unahitaji Kuondoa Tatizo La PID?

 

 Tupigie kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626

 

 

Arusha-Mbauda

 

 

Karibuni sana

 

4 thoughts on “YAJUE MADHARA YA MAAMBUKIZI YA MAGONJWA KATIKA VIA VYA UZAZI(PELVIC INFLAMMATORY DISEASES) AU PID.

  1. Doctor pole Sana na majukumu,pia tunakuombea sana Mungu ili azidi kukuinua na kukupatia maarifa ya kila siku,
    Pis zingatia kurudisha maadili kwenye Ofisi yako,yah gro lako ambalo ndo ofisi yako,jaribu kuikataa miza na kejeli,jaribu kujenga member kwenye msingi wa kiimani zaidi,zuia na kataa kwa mtu yeyeote anaetaka kutengeneza chuki,au chachu,kutokana na mtazamo wake mwenyewe,

    Mila jioni weka Neno la Mungu,weka vifungu vya biblia kujenga na kuimiza watu upendo,heshima,kuombeana,kutojiona yeye bora kulikoni wengine,Tafuta kuwaweka watu pamoja kusiwe na watu bora kuliko wengine,
    Jen ga msingi mwema wa kuwa na maono makubwa zaidi

    MUNGU AKUINUE AKUTUNZE AKUWEKE JUU ZAIDI,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *