Maambukizi katika njia ya mkojo mara nyingi huja na maswali mengi mno, yakiwemo haya; Je, unaweza kufanya tendo la ndoa huku ukiwa na maambukizi ya UTI? Na je, vipi kuhusu kufanya tendo la ndoa huku ukiwa na maambukizi ya UTI wakati unapotumia tiba?
NUKUU: Kila mmoja anaweza kukubari kwamba maambukizi katika njia ya mkojo huwa ni ya kuchukiza. Lakini pale yanapojaribu kuingiliana na mambo ya maisha ya ndoa, huwa ni kiwango kingine cha kuogofya.
Kabla Hujafahamu Kama Unaweza Kufanya Tendo La Ndoa Huku Ukiwa Na UTI, Basi Unahitaji Kuelewa Nini Maana Ya UTI.
U.T.I ni neno la kiingereza ambalo kirefu chake ni (Urinary Tract Infections), yaani maambukizi katika njia ya mkojo yajitokezayo katika sehemu yoyote ya mfumo wako wa mkojo, figo, mirija ya mkojo, kibofu cha mkojo na urethra. Maambukizi mengi hujitokeza sehemu za chini za njia ya mkojo, yaani kibofu na mrija wa mkojo.

NUKUU: UTI inaweza kuenea katika maeneo hayo niliyoyataja, ingawa yanaweza kupatwa na bakteria wengine pale wanapoingia kupitia njia ya haja kubwa na kuelekea kwenye utumbo, baadaye tena huhama kwenye utumbo na kuingia kwenye kibofu cha mkojo, hali ambayo kitaalamu huitwa, “ Cystitis” au “Urethritis”.
Je, Dalili Za UTI Zinakuwaje?
UTI mara nyingi huwa haijitokezi na dalili, bali mara nyingi zaidi huja bila dalili kama inavyoonekana. Hapa nitapenda kuelezea dalili za kawaida kabisa zinazompata muhusika, nazo ni;
- Kuhisi kukojoa mara kwa mara
- Kuhisi hali ya kuwaka moto baada ya kukojoa
- Kukojoa mara kwa mara lakini mkojo kidogo tu
- Mkojo wenye rangi ya ukungu
- Mkojo wenye harufu mbaya
- Maumivu maeneo ya nyonga, hasa maeneo ya tumbo la chini
NUKUU: Dalili hizo nilizozisema zinaweza kutofautiana kutegemeana na maeneo yaliyo athiriwa; maambukizi kwenye mirija ya mikojo yanaweza kusababisha hali ya kuwaka moto pamoja na mkojo ukiambatana na kutokwa na uchafu mbaya na mkojo mchafu au wenye rangi ya ukungu. Mojawapo wa uchufu huu unaweza kusababisha mambo haya:
- Maumivu kwenye nyonga,
- Maumivu kwenye tumbo la chini,
- Kukojoa mara kwa mara,
- Maumivu makali wakati wa kukojoa,
- Damu kwenye mkojo.
NUKUU: Na kama maambukizi yakienea kwenye figo, unaweza ukapatwa na maumivu ya mgongo au maumivu pembeni mwa mgongo wako, homa kali, kuhisi baridi, kichefuchefu pamoja na kutapika.
Je, Nini Husababisha UTI?
Nina neno moja napenda ulifahamu, nalo ni hili, “bakteria”. UTI hutokea pale bacteria wanaposafiri kuelekea katika maeneo mbalimbali ya njia ya mkojo kupitia mrija wa mkojo. Kwa bahati mbaya wanawake hupatwa na tatizo hili kwa urahisi kwakuwa sehemu yao ya uke iko karibu.

NUKUU: Hii hutokana na sababu kuu mbili: Njia ya mkojo na njia ya haja kubwa(mkundu) vipo karibu sana, na mlango wa njia ya mkojo ni mfupi ndani ya uke kuliko jinsi ilivyo kwenye uume. Unapofanya tendo la ndoa au unapokosea kufanya usafi maeneo hayo kama vile kujifuta na kitambaa kutoka nyuma kuja mbele, basi bakteria hupata njia kwa urahisi ya kuingia kwenye mfumo wa mkojo.
Kupata maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama vile mkanda wa jeshi, kisonono, pangusa, au malengelenge vinaweza pia kuruhusu bakteria kuingia kwenye njia ya mkojo na kusababisha maambukizi.
Lakini vihatarishi vingine kama vile mwanamke kukoma hedhi, pia huchangia kuongezeka kwa matatizo ya UTI kwa wanawake. Kukoma hedhi hupunguza uwezo wa homoni ya estrogen na hivyo kusababisha maambukizi ya UTI kuwa makubwa. Kuwa na matatizo ya kisukari au magonjwa mengine kunaweza pia kuchangia kudhoofika kwa mfumo kinga na kuweza kuongeza vihatarishi vya UTI.
Jambo Moja Unapaswa Ulifahamu Kabla Hatujafikia Eneo La Tendo La Ndoa: Ni Hivi, Mara Zote Unapaswa Umuone Daktari Endapo Kama Unahisi Una Tatizo La UTI
Ukumbuke kuwa, UTI haitoweki yenyewe bila kufanyiwa tiba. Kusema kweli, bakteria wanaweza kusafiri kutoka kwenye njia ya mkojo na kuingia kwenye figo, mahali ambapo inaweza kusababisha uharibifu wa kudumu.
Pale unapokuwa umemtembelea daktari mtaalamu na amethibitisha kupitia vipimo kuwa una UTI, basi taratibu za matibabu zitategemeana na na aina ya bakteria waliosababisha maambukizi na kama maambukizi yako hayana madhara au yana madhara.
Vipi Kama Umeanza Matibabu, Na Dalili Za UTI Zimeanza Kupungua, Na Unapatwa Hamu Ya Kufanya Tendo La Ndoa, Je, Unaweza Kufanya Tendo La Ndoa Huku Ukiwa Na Maambukizi Ya UTI?
Nipende kusema hivi, kama una maambukizi ya UTI na yanaendelea kutibiwa, basi huhitaji kujitenga kwamba usifanye tendo la ndoa. Bakteria tayari wameshaingia mahali ambapo hawakupaswa kuwa, na maambukizi yameshaanza. Kuna mambo machache unayopaswa kuyakumbuka.
NUKUU: Hakika dalili za UTI zinahitaji zitoweke ili kuyafanya mazingira ya uke yawe mazuri, vinginevyo tendo la ndoa linaweza kulifanya eneo la uke kuwa lenye kukera kabisa. Niseme tu kwamba unapoona dalili za UTI, hakuna haja ya kufanya tendo la ndoa. Jambo lingine unalopaswa kulishika ni hili, hata kama dalili ukiona zimetoweka, maambukizi yanaweza yasitoweke.
Dawa zinapoua bakteria hao wa UTI, pia zinapunguza uwezo wa mwenza wako kupatwa na maambukizi wakati mnapofanya tendo la ndoa. Hii ni kwasababu bakteria wa UTI wamo kwenye njia ya mkojo, sehemu ambayo imetengana kabisa na mlango wa uke. Ingawa bakteria hawa wamesafiri kutoka kwenye njia ya mkojo mpaka kwenye mirija ya figo, hivyo hawawezi kurudi nyuma kushuka mpaka eneo la uke na kumwambukiza mwenzi wako.
Na Usisahau: Kuna Mambo Unayoweza Kuyafanya Ili Kukusaidia Kujikinga Na Maambukizi Ya UTI Baadaye.
Unapokuwa umepata maambukizi ya UTI, utahitaji kujikinga na maambukizi hapo baadaye. Hapa nitakuonyesha hatua unazoweza kuchukua ili kupunguza hatari ya UTI, nazo ni kama ifuatavyo:
- Kunywa maji mengi kila siku ili upate nafasi ya kukojoa mara kwa mara
- Jitahidi kujipangusa kwa uangalifu kabisa maeneo ya uke, kuanzia mbele kurudi nyuma
- Usiweke kitu chochote chenye marashi maeneo ya uke
- Kojoa mara baada unapomaliza kufanya tendo la ndoa, pia kunywa glasi 1 ya maji ya kunywa.
Je, Unahitaji Huduma? Tupigie kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626
Arusha-Mbauda
Karibuni sana