JE, MFUMO WA UZAZI WA MWANAUME UNAKUWAJE?

Wanadamu hufanya tendo la ndoa, hivyo mwanaume na mwanamke huhitaji kuzaana ili kuongezeka, kama ilivyoandikwa nendeni mkazaane. Kila mwanadamu mwenye viungo kamili vya uzazi anao uwezo wa kuumba kiumbe kingine.

Picha inayohusiana

Tendo la ndoa linaweza kusababisha kutengeneza kiumbe kingine pale tu unapokutana na viungo vya uzazi vya mwanamke. Kwa upande wa wanaume viungo vya uzazi vya nje huwa kama ifuatavyo:

 

 

  • Uume: Hiki ni kiungo chenye mrija na msuli ambao hujaa damu pale unapohisi nyege au hamu, na hivyo kulifanya tendo la ndoa lifanyike

 

 

  • Korodani: Viungo hivi viwili vyenye umbo kama la yai, ndivyo huzarisha seli za mbegu za mwanaume na testosterone.

 

  • Pumbu: Mfuko huu ambao huning’inia chini ya uume na ndio hubeba korodani.

Wakati wanaume wote wanapozaliwa huku wakiwa na viungo vyao kamili vya uzazi, bado huwa hawawezi kufanya tendo la ndoa kikamilifu mpaka pale wanapofikia umri wa kubalehe. Umri huu wa kubalehe kwa wanaume huwa ni kuanzia miaka 12. Wakati wa kipindi hiki, mabadiriko ya homoni humuathiri kijana wa kiume katika tezi zake za uzazi ambazo kitaalamu tunaita, “gonads”, na hivyo hutengeneza mabadiriko ya kudumu na kumfanya kuwa mwanaume.

 

Hatua hii ina matokeo mengi kama vile, kukua kwa umbo lake, misuli kuongezeka, na nywele kuota maeneo ya chini sehemu za uzazi wake. Pamoja na kutoa mbegu, lakini kubalehe yaweza kuwa ndio ishara au dalili za kuonyesha muda ambao kijana amefikia kipindi cha kuweza kumzarisha mwanamke na kuitwa baba.

Korodani za mwanaume  huzarisha mbegu ambazo humwagwa wakati wa tendo la ndoa au pale anapofika kwenye mshindo. Hii ndio tunaita kufika kileleni. Mbegu hutoka kwenye uume zikiwa na mchanganyiko wa vitu vilivyoumbwa kwa ajili ya kurutubisha na kusafirisha seli kwenye mfumo wa uzazi wa mwanamke ili kuumba kiumbe kipya.

Picha inayohusiana

NUKUU: Kumbuka kuwa, huwa kuna takribani ya seli za mbegu milioni 750 zinazokuwa kwenye mshindo mmoja, lakini huwa ni mbegu moja tu ndio inayorutubisha yai la mwanamke.

 

Korodani nazo huzarisha homoni ya testosterone, ambayo hunyonywa moja kwa moja na kuingia kwenye mfumo wa damu. Pamoja na kurekebisha uzarishaji wa mbegu na kutengeneza hisia za mapenzi, lakini bado homoni hii pia hutengeneza sura ya kawaida ambayo kimwili hutofautisha mwanaume na mwanamke, kwa mfano; ndevu, sauti nzito, misuli mikubwa, na mabega mapana.

Mwanaume anapofikisha umri mkubwa, kazi ya tendo la ndoa hupungua. Hivyo basi, matatizo yanayompata katika kizazi chake huwa kama haya yafuatayo;

 

  • Kupungukiwa nguvu za kiume
  • Tasa
  • Mbegu kuwa chache
  • Homoni ya testosterone kupungua
  • Kufika kileleni mapeni

 

Je, Mbegu Za Mwanaume Zinazarishwaje?

 

 

Mfumo wa uzazi hasa umeundwa kwa ajili ya kuzarisha na kutoa mbegu, kuzihifadhi na kuzisafirisha., Mfumo wa viungo vya uzazi vya mwanaume vimo katika eneo la nyonga kwa ndani na nje pia, kama ilivyo jinsia ya kike. Viungo hivi ni kama ifuatavyo:

 

 

  • Korodani

 

  • Mrija wa kutolea mbegu

 

  • Tezi ya prostate pamoja na mrija wa shahawa

 

  • Uume

 

Je, Mbegu Hizi Zinatokea Wapi?

 

Uzarishaji wa mbegu hutokea kwenye korodani. Mwanaume hutoa mamilioni ya seli za mbegu kila siku pale anapofikia umri wa kubalehe.

 

Je, Mbegu Za Mwanume Zinatengenezwaje?

 

 

Kuna mfumo wa mirija midogomidogo kwenye korodani. Mirija hii, inaitwa seminiferous tubeles, huhifadhi kiini cha seli ambacho huchochea homoni hasa ya testosterone, homoni ya jinsia ya kiume ambayo huvifanya viini vya seli hizo zibadirike na kuwa shahawa. Viini vya seli hugawanyika na kubadirika hata kufanana na viluwiluwi huku vikiwa na kichwa na mkia mfupi.

Tokeo la picha la image of seminiferous tubules

NUKUU: Mikia ndio husukuma mbegu iingie kwenye mrija nyuma ya korodani unaoitwa, “epididymis”. Kwa muda wa wiki 5 hivi, mbegu husafiri kupitia mrija huu  na ili kukamirisha ukuaji. Ikiwa kama zikishindwa kupitia kwenye mrija wa epididymis, basi shahawa huelekea kwenye mrija mwingine ujulikanao kama, vas deferens

NUKUU: Mwanaume anaposisimuka mwili na kuwa na hamu ya kufanya tendo la ndoa, basi shahawa huchanganyikana na uteute wa manii, majimaji meupe mepesi ambayo hutengenezwa na seminal vesicles pamoja na tezi ya prostate ili kufanya kuwa manii. Kama ilivyo matokeo ya nyege au hamu ya kufanya tendo la ndoa, basi manii ambazo huwa zimebeba mbegu milioni 500, hutolewa nje ya uume pale unapofika kileleni kupitia mrija wa mkojo.

 

 

Je, Inachukua Muda Gani Kuzarisha Mbegu Zingine Mpya?

 

 

Utaraibu wa kuanzia pale kwenye kiini cha seli mpaka kuwa seli za mbegu zilizokomaa zikiwa tayari kwa ajili ya kurutubisha yai la mwanamke huchukua muda wa miezi 2.5.

 

Je, unahitaji pia kujiunga na darasa la mafunzo ya afya kila siku katika JAMES HERBAL GROUP? Sasa unaweza ukatuma namba yako ya WHATSSAP na tukakuunganisha na mafunzo ya afya bure.

 

Je, Unahitaji huduma juu ya matatizo ya uzazi kwa mwanaume au mwanamke? Tupigie kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626.

Tunapatikana Arusha Mbauda pia Njombe Makambako.

 

Karibuni sana.

 

One thought on “JE, MFUMO WA UZAZI WA MWANAUME UNAKUWAJE?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *