Tatizo hili huwakumba wengi katika jamii yetu lakini kwa bahati mbaya watu wengi huchukulia ni jambo la kawaida kitu ambacho baadaye hupelekea watu wengi kuingia kwenye matatizo makubwa ya ki afya hasa kwenye mfumo wa uzazi na wa chakula.

NUKUU: Yapo yale ya chini ya kitovu katikati, kushoto na kulia. Kwa wanawake Maumivu ya kushoto na kulia yapo ya aina mbili. Kuna yale ambayo yanakuwa upande mmoja lakini husambaa kwa urefu wa sentimita mpaka nne na inaweza ikawa upande mmoja au pande zote mbili lakini yapo mengine chini ya kitovu ambayo yanaweza yakawa upande mmoja au pande zote mbili bila kusambaa kwa marefu.
Kuna Maumivu mengine chini ya kitovu huwapata wanawake wakati wanaposhiriki tendo la ndoa kwa ndani ya uke au chini ya kitovu. Pia yapo ambayo huwapata wanawake wakati wameinama , wakati wa kunyanyua vitu vizito, wakati wa kucheka au kukimbia na wakati mwingine wakiwa wamelala kifudifudi.
Je, Maumivu Chini Ya Kitovu Yanaashiria Nini Kwa Wanawake?
Kwa kawaida Maumivu chini ya kitovu huwa yanaashiria mambo yafuatayo:
- Mirija Ya Uzazi Kujaa Maji Machafu
Maji haya huwa machafu tena mazito ambayo huzuia yai kutembea kwenye mirija ya uzazi. Mwanamke ambaye amewahi kuambiwa na daktari kwamba anatakiwa asafishwe kizazi chake au mirija ya uzazi na wakati huohuo anasikia maumivu chini ya kitovu na kulia au upande mmoja kuna uwezekano akawa na tatizo la mirija ya uzazi kuziba kutokana na kujaa maji machafu.
Unaweza ukaona mfano hapo juu.
- Kutokukomaa Kwa Mayai Ya Uzazi.
Hali hii husababisha vifuko vya mayai ya uzazi kuvimba(ovaritis) na kumletea mwanamke maumivu chini ya kitovu mithili ya kichomi. Mwanamke ambaye ana maumivu chini ya kitovu na wakati huo huo ana matatizo ya hedhi, mfano; hedhi kukoma au kutokuwa na mpangilio maalum, kuna uwezekano mkubwa akawa na tatizo la vifuko vyake vya mayai ya uzazi kutokomaza mayai na hivyo mayai kutotoka kwenye vifuko hivyo na kusababisha kuvimba na hatimaye kumsababishia mwanamke maumivu makali mithili ya kichomi.
- Maambukizi Katika Via Vya Uzazi
Hali ya kuvimba kwa kuta za mji wa mimba na kuta za mirija ya uzazi inaweza kutokana na maambuki ya magonjwa hasa ya zinaa(Pelvic Inflammatory Disease au PID).

NUKUU:Mwanamke anayesikia Maumivu chini ya kitovu katikati na pembeni kwa wakati mmoja na wakati huo huo akawa anatokwa na uchafu mzito mithili ya maziwa mtindi, kuna uwezekano akawa na PID hasa kama amewahi kukumbwa na tatizo la kuharibika kwa mimba kabla haijafikia miezi mitano.
- Afya Mbaya Ya Kibofu Cha Mkojo
Hali hii mara nyingi huwa inaambatana na matatizo ya maambukizi kwenye mfumo mzima wa mkojo(UTI). Mumivu chini ya kitovu yanayohusisha afya mbovu ya kibovu cha mkojo huambatana na magonjwa kutoa haja ndogo sana ila mara kwa mara.
Je, Maumivu Chini Ya Kitovu Kwa Wanaume Huashiria Nini?
Maumivu chini ya kitovu kwa wanaume huashiria pia tatizo la tezi dumu yaani kuvimba kwa tezi dume (Prostatitis). Maumivu haya hujikita kwenye shina la uume na huashiria tatizo hili hasa kama mwanaume anakwenda haja ndogo mara kwa mara nyakati za usiku na umri ukiwa unaelekea miaka 50 au zaidi. Dalili nyingine ambazo ni kutoa haja ndogo ambayo ina kiasi kidogo sana tofauti na kawaida ikiambatana na maumivu makali ya kiuno na mgongo, kuvimba kwa korodani, haja ndogo inayoambatana na usaha na damu, maumivu ya uume wakati wa kufika kileleni, na damu kwenye manii(semen).

NUKUU: Kwa wanaume maumivu haya pia huashiria tatizo la ngiri(hernia). Mwanaume anaposikia Maumivu haya ya chini ya kitovu yakiambatana na maumivu ya korodani, korodani moja kupungua na nyingine kukua zaidi au zote mbili kukua au kupotea, ni dalili ya ugonjwa huu ambao huharibu ubora wa uzarishwaji wa mbegu za kiume ambazo zaweza kuzarishwa chache au ambazo hazina kasi ya kutosha kusafiri kwenye via vya uzazi vya mwanamke na hivyo mwanaume kupoteza uwezo wake wa kutungungisha mimba.
Maumivu chini ya kitovu kwa wanaume kama ilivyo kwa wanawake huashiria matatizo ya maambukizi katika mfumo wa haja ndogo yaani(Urinary Tract Infection au UTI) ambapo dalili zake ni kama zile za mwanamke hapo juu.
Jame & Ferdinand Herbal Clinic tunatibu magonjwa hayo yote kwa njia ya tiba za asili kabisa.
Je, unahitaji huduma? Unaweza kutupigia simu kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626.
Arusha-Mbauda
Karibuni sana.
Mm nilikuw period siku ya kwanza zilitok Ila sio nying siku ya pil zilitok kidog na jion nikasex na kakojoa ndan na nikaw natokwa na uchaf wa rang ya maziw Ila saiv nasumbuliw na tumbo chin ya kitov nashindwa hat kutembea vizur je ntakuw na mimba au
Nahitaji kueleweshwa sababu ya mwanamke kukojoa mkojo afu mwisho damu ikiambatana na maumivu ya chivi ya kitovu akibanwa na mkojo
Je, unaweza kutuma namba yako ya whatsap
Jaman nahitaj kujua dawa maana shida zote hapo mm ninazo namehangaika sana bila mafanikio namba yangu ya WhatsApp 0623343779
Nauliza kwa mwanamme akipata maumivu chini ya kitovu ni Dalili za nini
0679530114
Naomba kuuliza shida inayompata Mama mjamzito kuwa na maumivu makali chini ya kitovu tatizo ni nini n’a nini madhara yake
Je, aliwahi kupima maambukzii ya PID?
Mke wangu anasumbuliwa na maumivu chini ya kitovu yanasamba mpak huku pembeni halafu anatoka uchafu Kam wanjano tatizo ni nini?
Mm napata chini ya kitovu katikati Kama kichomi Yani yakinikamata ata kunyanyuka siwezi
Pole sana
Karubu sana
Habar
Eti naomba kuuliza hivi ukiwa siku za hatar alafu tumbo likawa linauma upande wa kulia chini hapa shida ni nn itakua manake nimejichunguza Leo ndo nimegundua nikiwa siku hizi ndo naumwa Sana upande huu na nahisi kichefu chefu pia
Habar
Eti naomba kuuliza hivi ukiwa siku za hatar alafu tumbo likawa linauma upande wa kulia chini hapa shida ni nn itakua manake nimejichunguza Leo ndo nimegundua nikiwa siku hizi ndo naumwa Sana upande huu na nahisi kichefu chefu pia
Maumivu chini ya Kitovu na chuchu kuvuta na kuwasha sijui shida nini msaada jaman
Pole dada je umewahi kufanya vipimo?
Je hayo maumivu yanaweza kupelekea
Mwanamke kutopata hedhi yake
Akikutana na mume wake siku ambzo sio hatari baada ya siku3 anapata hayo maumivu na haoni hedhi yake je nn chanzo na tiba dr
Je, amewahi kwenda kufanya vipimo katika tumbo lake la uzazi?
Jmn mie pia nasumbuliwa na Hilo tumbo Ila nikiwaambia nyumban wanasema nikapime uti Yan linanisumbuwa Sana
Je, umewahi kupima vipimo ukapata jibu sahihi?
Doktor mwanamke wang mara ya mwisho ku sex nae alivoend chooni kujisafish akatoa vitu vyeupe tofaut na sperms iyo itakua shida n nn
Hayo huwa ni maambukizi ya fangasi mwambie akapime tu
Hi mm natatiz la mkoj mara kwa mara na maumivu chin ya kitovu je? Tatizo au inaendana namaradhi ya zinaa
Pole sana, hizo ni dalili za UTI. Je, umewahi kufanya vipimo?