JE, NINI HUSABABISHA MWANAMKE KUPATA HEDHI YA SIKU 2 TU KISHA INAKATA? JE, NINI DALILI ZAKE?

Kipindi cha mzungo wa hedhi hutofautiana kutoka kwa mwanamke mmoja kwenda kwa mwingine. Hata kwa mwanamke mmoja mzunguko wa hedhi unaweza ukawa sawa lakini baadaye ukawa tofauti. Mzunguko wa kawaida wa hedhi huwa ni kuanzia siku 28-35 na hujitokeza ovyo ovyo majuma mawili baada ya yai kupevuka. Kila mwanamke mwenye afya nzuri anaweza akaingia hedhini mara 11-13 kila mwaka.

What Your Period Says About Health Explained

Kipindi cha kutokwa na uteute ukeni kila mwezi kinaweza kudumu kwa muda wa siku 2-5 kwa mwanamke mwenye hali ya kawaida. Kutokwa na ute ukeni kwa muda wa siku 2 sio jambo la kutisha sana. Lakini kama ukiwa kwenye kipindi au umri wa kuzaa na unajaribu kupata ujauzito, basi hiki kipindi cha siku 2 kinaweza kukutia wasiwasi. Kumbuka kuwa huwezi kuwa mjamzito mara unapotokwa na damu ukeni. Yai linaporutubishwa hupachikwa ukutani mwa mfuko wa uzazi. Utaratibu huu unaweza kusababisha kutokwa na damu kwa muda wa siku 1 au 2. Ikiwa uliwahi kufanya tendo la ndoa bila kutumia kinga hivi karibuni na kama umekuwa ukitokwa na matone ya damu yenye rangi ya kahawia, basi ni ishara tosha ya kukufanya ufike hospitali umuone daktari.

SPOTTING - YouTube

Kutokwa na damu ya hedhi kwa muda wa siku 2 yaweza kuwa ishara ya ujauzito lakini sio hakika sana. Matone ya damu kutoka ukeni hukoma ghafla baada ya siku 2 ikiwa kama yai limerutubishwa. Lakini zipo dalili zingine kama vile uchovu mabadiriko ya homoni yanayosababisha kutiwa na wasiwasi au hisia za kusikitisha pamoja na kukojoa mara kwa mara. Matiti yako yanaweza kuwa magumu na chuchu zinaweza kuuma na zenye rangi nyeusi. Kuhisi kichefuchefu na kutapika huwa ni ishara zingine zinazoonyesha ujauzito kwa wanawake wengi. Kizunguzungu, kichwa kuuma pamoja na uchovu huwa ni ishara za kawaida wakati wa ujauzito. Kutamani vyakula fulani ni ishara pia za kawaida miongoni mwa wanawake wajawazito.

No elevated risk of coronavirus in pregnancy, experts say | World ...

NUKUU: Sio lazima kwamba kila mjamzito anaweza akapata dalili nilizozitaja hapo juu. Baadhi yao wanaweza wasipate dalili zozote kati ya hizo nilizozisema lakini bado wanakuwa ni wajawazito tu. Inapendeza ukajipima mwenyewe au ukaenda hospitali ukamuona daktari ili kuhakikisha endapo kama ni dalili za ujauzito au la.

Visababishi Vikuu Vya Kutokwa Na Damu Ya Hedhi Kwa Muda Wa Siku 2 Tu.

 

 

  1. Homoni Ya Estrogen

 

 

Homoni ya estrogen huwajibika sana katika kumfanya mwanamke kuwa mjamzito au kupata kipindi cha hedhi. Kiwango cha homoni ya estrogen kinaweza kuwa juu katika umri wa kubalehe na pale unapofikia umri mkubwa na inaweza kinaweza kikashuka polepole kadri mwanamke anapofikia umri wa miaka 40-45 na anapokoma hedhi kabisa. Matone ya damu ukeni yanaweza yakajitokeza kwasababu ya kubadirika kwa viwango vya homoni ya estrogen.

7 Conditions That Can Cause Sporadic Spotting Between PeriodsNUKUU: Kindi cha hedhi kinaweza kikawa cha kubadirika badirika kwasababu ya kubadirika kwa viwango vya homoni ya estrogen. Badiriko lolote katika homoni ya estrogen linaweza kusababisha kipindi kifupi cha hedhi au kirefu kutegemeana na hali yenyewe.

 

 

  1. Matumizi Ya Madawa Ya Mpango Wa Uzazi

 

 

 

Wanawake wengi wanaopata kipindi kifupi cha hedhi yaani kutokwa na damu ya hedhi kwa muda wa siku 2 tu wanaweza kuwa waliwahi kutumia baadhi ya aina ya madawa ya uzazi wa mpango. Inaweza ikawa vidonge vya kumeza au vijiti au sindano.

Herpes Medical Treatment Guide - Herpes101.net - The Ultimate ...NUKUU: Sindano za uzazi wa mpango zinaweza kuathiri uzarishaji wa homoni ya estrogen. Wanawake wanaotumia njia ya kupandikiza vijiti ili kuzuia ujauzito mara nyingi hutokwa na matone ya damu kuliko wengine.

 

  1. Msongo Wa Mawazo

 

 

 

Wanawake wanakumbana na matukio mabaya ya ghafla wanaweza kupata  matone ya damu kwa muda wa siku 2 hata kabla kipindi cha hedhi hakijawadia. Ugomvi wa mara kwa mara  au unyanyasaji unaweza kusababisha kutokwa na vitu ukeni ghafla.

Why do women suffer more stress? | Sha Wellness

NUKUU: Kama kuna kiwango kikubwa cha msongo wa mawazo inaweza kusababisha  uchafu ukeni au maambukizi katika njia ya mkojo.

  1. Kupungua Uzito Au Kukonda

 

 

 

Kupungua uzito ghafla kunaweza kubadirisha mzunguko wa hedhi pamoja na viwango vya homoni ya estrogen ambavyo vinaweza kusababisha hedhi kurukaruka.

How to lose weight fast: 9 scientific ways to drop fat

NUKUU: Vilevile kama unaongezeka uzito haraka inaweza kusababisha kutokwa na damu damu ukeni kwa muda wa siku 2 au vipindi vya hedhi kuchelewa. Kumbuka mwili wako hupokea badiriko lolote katika uyeyushaji wa mafuta.

 

  1. Anemia

 

Kama viwango vya madini ya chuma kwenye damu yako yakipungua, basi inaweza kusababisha kutokwa na damu ya hedhi kwa muda wa siku 2 au hata 1. Kwa namna hiyo kunaweza kukawa na dalili zingine kama vile uchovu pamoja na kuishiwa nguvu kabisa.

 

  1. Ugonjwa Sugu

 

 

 

Wanawake wenye kisukari pamoja na matatizo sugu kama vile ugonjwa wa ini au TB wanaweza kupatwa na hali ya kutokwa na damu ya hedhi kwa muda wa siku 2 tu kabla mzunguko wa hedhi haujawadia. Tatizo lolote jipya katika mfumo wako linaweza kusababisha vipindi vya hedhi kubadirika au kuruka.

5 Tips for Managing Diabetes at Work - Parents Magazine AfricaNUKUU: Kama kuna badiriko lolote katika vipindi vya kawaida na kama hakuna dalili yoyote, basi unaweza ukaonana na daktari. Inafaa kupata kipimo cha ujauzito kuliko kuwa na hali ya hofu. Ni kawaida kabisa kuwa na wasiwasi endapo kama jambo litakuwa limeenda kinyume na utaratibu. Hata kama utaona hali ya kutokwa damu nyepesi ukeni na ikadumu kwa muda wa siku moja tu, bado unaweza kwenda kumuona daktari ili aweze kuchngananua mambo yanayokusumbua.

 

NUKUU: Baada ya vipimo ikiwa kama umepata majibu na kujua chanzo cha tatizo lako, basi unaweza kutupigia simu kwa namba zetu hizi: 0752389252 au 0712181626

 

Au unaweza ukatuma namba yako ya Whatssap ili uweze kupata link ya kuweza kuingia katika darasa letu zuri la masomo ya afya.

 

Arusha-Mbauda

 

 

Karibuni sana

3 thoughts on “JE, NINI HUSABABISHA MWANAMKE KUPATA HEDHI YA SIKU 2 TU KISHA INAKATA? JE, NINI DALILI ZAKE?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *