Na ieleweke kuwa, uvimbe ni bonge la tishu ambalo huota ndani ya ukuta wa mfuko wa kizazi(uterus). Fibroid huwa sio kitu cha kawaida kabisa; kwani tukiangalia asilimia 50% ya wanawake hivi sasa wamekuwa wakipatwa na matatizo ya uvimbe wa fibroid.

Lakini kumbuka kwamba uvimbe aina ya fibroid mara nyingi huendelea kukua pale mwanamke anapofikia umri mkubwa wala tu katika umri wake wa kuzaa.
Je, Dalili Za Uvimbe Aina Ya Fibroid Zinakuwaje?
Kwa upande wa wanawake wengi, uvimbe aina ya fibroid inaonyesha kutosababisha matatizo yoyote ikiwa kama uvimbe utatibiwa mapema. Baadhi ya wanawake, hata hivyo hupatwa na dalili zifuatazo:
- Maumivu ya nyonga
- Kutokwa na damu ya hedhi muda mrefu
- Matatizo ya ugumba
- Mimba kuporomoka
Je, Kwanini Uvimbe Wa Fibroid Unasababisha Mimba Kutoka?
Inaonekana kwamba, uvimbe aina ya fibroid umekuwa chanzo kikubwa cha kuharibu mimba au ujauzito wa mwanamke. Madaktari wengi kwenye mahospitali makubwa wamekuwa wakiamini kwamba, matatizo yanayosababishwa na uvimbe wa fibroid kwa baadhi ya wanawake ni aina na ukubwa wa uvimbe wa fibroid na mahali au eneo uvimbe ulipo kwenye mfuko wa kizazi.
![]()
Kwa mfano, kama uvimbe wa fibroid unapokuwa karibu katikati ya mfuko wa kizazi(uterus), ambapo yai lililorutubishwa hujipachika, basi uvimbe unaweza kusababisha mimba kuporomoka. Uvimbe wa fibroid ambao huota nje ya mfuko wa kizazi na ukabadirisha umbo lake(submucous fibroids) na vivimbe vingine vinavyokuwa ndani ya mfuko wa kizazi(intracavity fibroids), mara nyingi husababisha mimba kuporomoka kuliko uvimbe unaokuwa ndani ya ukuta wa mfuko wa kizazi(intramural fibroids) au nje ya ukuta wa mfuko wa kizazi(subserosal fibroids). Uvimbe mkubwa wa fibroid huwa ni tatizo kubwa mno kuliko uvimbe mdogo.
NUKUU: Uvimbe mkubwa wa fibroid huwa una mishipa mingi ya damu, na ndio maana unaweza kufanya damu ibubujike kwa wingi kutoka kwenye mfuko wa kizazi na kusababisha mimba kuporomoka.
Je, Uvimbe Wa Fibroid Hupimwaje?
Madaktari mara nyingi hupima uvimbe wa fibroid kwa kufanya uchunguzi wa nyonga. Ikiwa kama daktari anahitaji taarifa nyingi zaidi juu ya uvimbe, hasa kwa wanawake wanaokuwa na tatizo la kuporomoka kwa mimba au ugumba, basi daktari anaweza pia kuagiza kipimo cha, “Hysterosalpingogram(HSG) au Sonohysterogram, ambacho huingizwa ukeni na kupimwa kwa njia ya Ultrasound.
Je, Uvimbe Wa Fibroid Hupimwaje?
Madaktari mara nyingi hupima uvimbe wa fibroid kwa kufanya uchunguzi wa nyonga. Ikiwa kama daktari anahitaji taarifa nyingi zaidi juu ya uvimbe, hasa kwa wanawake wanaokuwa na tatizo la kuporomoka kwa mimba au ugumba, basi daktari anaweza pia kuagiza kipimo cha, “Hysterosalpingogram(HSG) au Sonohysterogram, ambacho huingizwa ukeni na kupimwa kwa njia ya Ultrasound.
Je, unahitaji huduma? Basi tupigie kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626
Arusha Mbauda
Karibuni sana.