Ni salama kabisa kwa mwanamke kuendelea kufanya tendo la ndoa wakati wa ujauzito wake endapo tu kama daktari au mkunga wake atakuwa amemwambia mambo mengine kama ushauri. Kusema kweli, tendo la ndoa kwa mwanamke linaweza kuongezeka katika hatua Fulani za ujauzito, na tendo la ndoa linaweza kuwa na baadhi ya faida.

NUKUU: Tumbo linapoanza kuwa kubwa, mwanamke anaweza kugundua kuwa maeneo Fulani yanaweza kuwa salama. Kuongea waziwazi juu ya tendo la ndoa kunaweza kusaidia wazazi wote wawili kufurahia tendo la ndoa kupitia ujauzito.
Lakini pia tunajadiliana vizuri tu kama mume na mke kuwa jinsi gani tunaweza kubadiri style zetu za kufanya tendo la ndoa pale mimba inapofikisha miezi tisa.
Je, Kunakuwa Na Usalama Kweli Ufanyapo Tendo La Ndoa?
Tendo la ndoa halitamdhuru mtoto katika hatua yoyote ya ujauzito. Kumbuka kuwa mimba hutunzwa na misuli migumu ya tumbo la uzazi, majimaji ya tumboni, pamoja na uteute ambao huendelea kutoka kwenye shingo ya uzazi. Baadhi ya watu huamini kuwa kitendo cha kufanya tendo la ndoa na kufika kileleni kunaweza kuharibu mtoto tumboni, au kufanya mimba iporomoke au kumfanya mwanamke azae kabla ya muda wake. Hata hivyo kwa mwanamke mwenye mwili wenye afya hali hii haiwezi kutokea.
Je, Tendo La Ndoa Linaweza Kumfanya Mjamzito Kujifungua Mapema?
Tendo la ndoa wakati wa ujauzito huwa halina mpaka. Hata hivyo ikiwa kama daktari atatoa ushauri au tahadhari, anaweza akapendekeza kwamba mjamzito asifanye tendo la ndoa wakati wa ujauzito wake au pale mimba inapofikia muda wa kujifungua.

NUKUU: Inawezekana kwamba kile kitendo cha mwanaume kufika kileleni kunaweza kusababisha hitilafu kama vile tumbo kuuma kama uchungu vile ikiwa kama mimba ina miezi tisa au mwanamke kakaribia kujifungua. Hata hivyo hitilifu hii haiwezi kuonyesha kuwa mwanamke anaweza akajifungua.
Je, Mitindo Au Style Gani Nzuri Za Kufanya Tendo La Ndoa?
Wakati mimba inapofikisha miezi 8-9, wanandoa wanapaswa wachague tyle au mitindo ya kufanya tendo la ndoa ambazo haziwezi kuleta madhara kwenye tumbo la mjamzito. Kama mwanamke akilala chali, basi uzito wa mtoto lazima ukandamize viungo vya ndani vya uzazi vya mwanamke au mishipa mikubwa ya damu inayokuwa kwenye kizazi.

NUKUU: Mwanamke mjamzito lazima ajisikie raha katika style anayoweza kuichagua ili kuweza kusaidia uume usiingie ndani sana na usiingie kwa nguvu kubwa mno. Ni taratibu tu kama vile hutaki.
Nikufundishe leo kuwa style nzuri kwa mjamzito inaweza kuwa kulala ki ubavu, kukaa mwishoni mwa kitanda au mwanamke kuwa juu ya mwanaume.
Je, Ni Kipindi Gani Cha Kuacha Kufanya Tendo La Ndoa?
Mkunga au daktari anaweza kumshauri mwanamke kujihadhali na tendo la ndoa wakati wa ujzuito wake ikiwa kama ana mambo yafuatayo:
- Mimba ya mapacha
- Kondo ikiwa halijafunika vizuri
- Shingo ya kizazi kutokuwa na uwezo ambapo hufunguka kwa muda
- Kupungukiwa na damu
- Majimaji kuvuja
- Tatizo kwenye shingo ya kizazi hali ambayo inaweza kusababisha mimba kutoka au kujifungua mapema kabla ya muda
Madhara Ya Ujauzito Katika Kuvuta Hisia Za Tendo La Ndoa
Ujauzito huathiri hisia za mapenzi za watu katika njia mbalimbali nazo huwa kama ifuatavyo:
- Nguvu za homoni na muongezeko wa mtiririko wa damu katika eneo la uke kunaweza kuongeza hisia au nyege kwa mama mjamzito hasa pale mimba inapofikia muda wa miezi 4-6.
- Wanawake wengine wanaweza kupatwa na hali ya kupungua kwa hisia ya tendo la ndoa kutokana na mabadiriko ya homoni, kujisikia vibaya mwilini, kupungua kwa kiwango cha nishati, au maumivu ya mwili.
- Ujauzito pia unaweza kuathiri hisia za mapenzi kwa mwenzi wa mjamzito. Utakuta wakati mwingine mwanamke anapopata ujauzito, mwanaume anakosa hisia au hamu ya kufanya naye tendo la ndoa. Lakini utakuta wanaume wengine wanakuwa na mvuto au hamu kubwa sana ya kufanya tendo la ndoa na wake zao pale wanapoona umbo la mama mjamzito limebadirika kama vile matiti kuongezeka na kuwa makubwa au matakao kuwa makubwa au uso kuwa mzuri, mikono kuwa laini, na joto kuongezeka. Hivyo wanaume hao hupatwa na mvuto mkubwa mno.
Je, Nini Faida Ya Kufanya Tendo La Ndoa Wakati Wa Ujauzito?
Tendo la ndoa wakati wa ujauzito linaweza kuwa na baadhi ya faida kwa mjamzito pamoja na mwenzi wake. Faida hizi huwa kama ifuatavyo:
- Mwanamke kufika kileleni au kukojoa haraka tena zaidi ya mara 1
- Joto ukeni kuongezeka na kumfanya mwanaume kujisikia raha
- Kuwafanya mke na mume kuwa pamoja muda wote
- Kinga ya mwili kuongezeka
- Furaha na upendo kuongezeka tena pale wanapofika kileleni pamoja
Je, Tendo La Ndoa Linatakiwa Lifanyike Muda Gani Baada Ya Kujifungua?
Wanawake wote waliojifungua wanahitaji muda wa kupona maeneo ya viungo vya uzazi baada ya kujifungua. Wanapaswa wapate muda wa kutosha ili mwili upone, shingo au mlango wa kizazi ufunge, damu inayotokatoka ikome, na ikiwezekana uke uweze kupona kabisa. Najua midume mingine huwa inalazimisha tendo la ndoa hata kama mama hajapona bado.
:max_bytes(150000):strip_icc()/126292540-56a771cb5f9b58b7d0ea8ed9.jpg)
NUKUU: Wanawake wanaweza kurudia hali ya kufanya tendo la ndoa endapo kama watajisikia kuwa wapo tayari kufanya hivyo. Nipende kusema tu kuwa mwanamke anapaswa apewe muda hata wa miezi kama 5-6 ndio afanye tendo la ndoa mara anapomaliza kujifungua
Je, Ni Lini Unapaswa Kumuona Daktari?
Ikiwa mwanamke mjamzito ataona maumivu yoyote yasiyo ya kawaida au kutokwa na damu wakati wa ujauzito, basi anatakiwa akimbie hospitali haraka bila kuchelewa.

Umuonapo daktari wako kwa muda mzuri, bila shaka unaweza ukaokoa maisha ya kiumbe kilichomo tumboni mwako.
Je, Unahitahi huduma kutoka James & Ferdinand Herbal Clinic? Tupigie kwa namba zifuatazo:
Arusha-Mbauda: 0752389252 au 0712181626
Njombe-Makambako: 0744531152 au 0716158086
Karibuni sana.
Nimeipenda Sana makala yako shukurani kwa kunielimisha
Ahsante mungu awabariki
Amina
Asante nimefurahia Sana n nime enjoy a lot
Barikiwa Jane
Asante wafundisha vizuri
Barikiwa dada Zuhura
Kazi nzuri
Amina
Duúuu apo kwenye miezi 5 had 6 apo weeee apana em pafanyie utafit vzr ndo uje utufundishe apa maana
Umeona nini dada
Amina
Umeelezea poa nmeelewa
Nmeipenda xana hii Makala ila hapo kwenye miez 5..hadi 6..hapana jamaniii parefu xana ebu tazameni vzurii
Barikiwa sana kaka, karibu sana
Safi Sana .
Asante nimejifuza mengi sana