Ute ute huwa ni mchanganyiko wa majimaji ambao hutoka ukeni au kwenye uume. Watu wanaweza kuona ute au majimaji kabla, au baada ya tendo la ndoa au wakati wa kufanya tendo la ndoa.
Ute unaoonekana ukeni au kwenye uume, huwa hauna kiwango maalum. Kwa mwanaume, uume wenye afya hutoa ute ute kabla au baada ya kufika kileleni. Mambo fulani yanaweza kusababisha kiwango na muonekano wa ute ute au majimaji. Muendelezo wa kutoka kwa ute ukeni kwa mfano, mabadiriko ya asili katika vipindi vya mzunguko wa hedhi.
NUKUU: Hata hivyo baadhi ya mabadiriko kwenye uteute kunaweza kuonyesha matatizo ya kiafya.
Makala hii itaonyesha visababishi hakika vya kutokwa na ute au majimaji baada ya kumaliza kufanya tendo la ndoa.
Je, Uteute Ukeni Baada Ya Tendo La Ndoa Unakuwaje?
Uteute unaotoka ukeni pindi uke ukiwa na afya nzuri huwa ni msafi au mweupe ambao huwa ni uteute wa shingo ya kizazi, au uteute wa ukeni. Baadhi ya mabadiriko katika kiwango au muonekano wa ute wa ukeni yanaweza kuonekana kiasili, wakati mengine yanaweza kuonyesha matatizo ya kiafya.
Sehemu hii inaelezea baadhi ya visababishi vya kawaida vya ute ute unaotoka ukeni baada ya kufanya tendo la ndoa.
- Hamu Au Hisia
Hamu ya tendo la ndoa huamsha muongezeko wa damu kwenye sehemu ya uke. Mishipa ya damu hupanuka ili kupokea damu. Kwa wanawake, hali hii husababisha kuvimba kwenye mashavu, kisimi pamoja na tishu zinazotanda ukeni. Pia tezi kwenye uke huzarisha uteute wenye muonekano kama majimaji unaokuwa msafi ambao husaidia kulainisha uke wakati wa tendo la ndoa.
Uwepo wa ute wa hisia yanaweza kuufanya ute wa ukeni uweze kuonekana zaidi. Ute ute unaweza kuwa mzito na ukawa na muonekano kama maziwa ya mtindi.

Aina hii ya uteute ukeni huwa ya kawaida na huwa haionyeshi dalili za matatizo. Hata hivyo, kama ute ni mzito na utakuwa na harufu mbaya, basi yanaweza kuonyesha tatizo la afya.
- Mwanamke Kufika Kileleni
Mwanamke anaweza kufika kileleni wakati wa tendo la ndoa. Hii huwa ni hali ya kutoa majimaji kupitia njia ya mkojo. Mwanamke yeyote anayefika kileleni inaonyesha kuwa ni mtu mwenye afya kamili katika kizazi chache.
- Mabadiriko Ya Mzunguko Wa Hedhi
Mabadiriko ya homoni ambayo yanajitokeza kwenye mzunguko wa hedhi hubadirisha kiwango na muonekano wa ute au majimaji ukeni. Mwanzoni hadi mwisho mwa mzunguko wa hedhi, uteute unaweza kuwa mzito na mweupe. Wakati yai linapopevuka, uteute unaweza kujitokeza wenye muonekano kama ute wa yai la kuku kwani huwa wenye kulendemka.
Wakati mwingine kipindi cha mzunguko wa hedhi, ute unaweza kuwa mwepesi wenye majimaji. Inapofikia hatua ya mzunguko wa hedhi kufikia mwishoni, damu ya zamani inaweza kuonekana kwenye uteute, wenye rangi ya kahawia.
NUKUU: Yote haya huwa ni mambo ya kawaida wala hayasababishi matatizo kwa muhusika.
- Bakteria Ukeni
Bakteria ukeni wanaweza kusababisha ute kutoka baada ya kufanya tendo la ndoa. Hali hii hujitokeza pale kiwango cha asidi ukeni kinapobadirika, na kuharibu afya ya uwiano wa bakteria wa asili ukeni. Unapokuwa na mpenzi mpya au wapenzi wengi, au kuwa na tabia ya kuosha uke kwa sabuni za marashi, nk, unaweza kuongeza vihatarishi katika uke wako.
Bakteria ukeni wanaweza kusababisha kutokwa na ute mweupe au wa kijivu na wenye harufu mbaya kama shombo la samaki. Inaweza kuwa rahisi kabisa kutambua ute unaotoka ukeni baada ya kumaliza kufanya tendo la ndoa.
Dalili zingine za maambukizi ya bakteria ukeni huwa kama ifuatavyo;
- Muwasho au kuhisi hali ya kuwaka moto ukeni
- Muwasho au kuhisi hali ya kuwaka moto maeneo ya mashavu ya uke
- Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa
Je, Vipimo Vinafanyikaje?
Daktari atafanya vipimo vya uke na kuchunguza sampli ya ute unaotoka ukeni kwa ajili ya ishara za bakteria wanaokua.
Je, Matibabu Yake Yanakuwaje?
Baadhi ya watu hawahitaji matibabu kwa ajili ya maambukizi ya bakteria ukeni, lakini pale mtu anapokuwa na dalili, basi zinaweza kuhitaji matibabu ya antibiotic.
Pia napenda nikukumbushe msomaji kuwa tatizo hili lisipotibiwa linaweza kusababisha kuongezeka vihatarishi kwa muhusika kama vile;
- Ukimwi
- Pangusa
- Kisonono
- Maambukizi katika via vya uzazi
- Fangasi
Uteute mweupe mzito wakati wa kufanya tendo la ndoa unaweza kuonyesha ishara za fangasi. Maambukizi ya fangasi sehemu za siri hukua kwa kasi sana katika maeneo ya mwili yaliyoathirika.
. Kwa asili, vimelea wa Fangasi huishi kinywani, kooni, ukeni, na juu ya ngozi. Karibia asilimia 75% ya wanawake hupatwa na maambukizi ya fangasi ukeni katika maisha yao. Mambo yafuatayo yanaweza kuongeza vihatarishi vya maambukizi ya fangasi, nayo ni;
- Ujauzito
- Kisukari
- Madawa ya mpango wa uzazi
- Kupungua kwa kinga ya mwili
- Matumizi ya sabuni ukeni zenye marashi makali
Maambukizi ya fangasi sehemu za siri husababisha dalili mbalimbali kama vile;
- Muwasho ndani au pembeni mwa uke
- Kuvimba kwa uke au mashavu ya uke
- Mashavu ya uke kuwa mekundu sana kwa ndani
- Kuhisi maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa
- Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa
- Kutokwa na ute mweupe kama maziwa mgando usiokuwa na harufu
- Ute Utokao Kwenye Uume Baada Ya Tendo La Ndoa
Ute unaotoka kwenye uume hufanana na majimaji yoyote mbali na mkojo unaopita kwenye mrija wa mkojo. Ute wenye afya unaotoka kwenye uume ni ule unaotoka kabla ya tendo la ndoa pale mwanaume anapokuwa ana hisia au nyege, pia ule unaotoka anapofika kileleni baada ya kumaliza kufanya tendo la ndoa. Kutokwa na uteute kwenye uume bila kuhisi hisia au nyege, yaweza kuwa ishara au dalili za matatizo ya kiafya.
- Hamu Au Hisia
Wakati wa hisia za tendo la ndoa, tezi zinazokuwa chini ya korodani, huzarisha ute mwepesi tena msafi unaojulikana kama, “ute ute unaotoka kabla ya kufanya tendo la ndoa”.
Ute huu hufanya kazi kama kilainisha cha asili kwa ajili ya kichwa cha uume wakati wa tendo la ndoa. Ute huu pia hugeuza asidi ya mrija wa mkojo wa mwanaume pamoja na uke.
Kukojoa shahawa au manii, huwa ni ute wenye rangi nyeupe au kijivu ambao una majimaji ya manii na seli za shahawa.
Kitendo cha kukojoa shahawa kwa kawaida hujitokeza wakati wa kufika kileleni.
- Kuvimba Kwa Mrija Wa Mkojo(Urethritis)
Urethritis ni kuvimba kwa mrija wa mkojo. Visababishi vyake huwa ni maambukizi ya virusi pamoja na bakiteria. Kuvimba kwa mrija wa mkojo kunaweza kusababisha kutokwa na ute kwenye uume wenye rangi nyeupe au kijivu.
Dalili zingine ni pamoja na;
- Kuhisi hali ya kuwaka moto wakati wa kukojoa
- Kukojoa mara kwa mara
- Maumivu wakati wa tendo la ndoa au wakati wa kufika kileleni
- Damu kwenye mkojo au shahawa.
- Muwasho, uvimbe au michubuko ndani ya uume pamoja na mlango wa mrija wa mkojo
Je, Vipimo Vinafanyikaje?
Daktari anapokuwa na mgonjwa, yeye huangalia uvimbe maeneo ya tumbo la chini pamoja na kwenye nyonga. Pia madaktari wanaweza kukusanya sampuli za mkojo na uteute ambao hupelekwa maabara kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Unaweza ukaona hapo juu jinsi daktari anavyoweza kukusanya mkojo kwa ajili ya kufanya uchunguzi zaidi.
- Maambukizi Ya Magonjwa Ya Zinaa
Magonjwa ya zinaa huenea kama matokeo ya kufanya tendo la ndoa bila kutumia kinga. Magonjwa ya zinaa ni kisonono pamoja na pangusa ambayo yanaweza kusababisha kutokwa na ute usio wa kawaida ukeni au kwenye uume.
- Pangusa(Chlamydia)
Pangusa ni mojawapo ya magonjwa ya zinaa ya kawaida. Watu walioathirika inaonyesha kuwa wenye umri kati ya miaka 15-24. Pangusa kwa kawaida huwa haionyeshi dalili. Kama dalili zikionekana zinaweza kuonekana kwa siku chache au wiki kadhaa baada ya mtu kuwa amepata maambukizi.

Ute unaotoka ukeni unaweza kuwa wa njano. Dalili zingine za ugonjwa wa pangusa kwa wanawake huwa kama ifuatavyo:
- Choo chenye damu, maumivu au kutokwa na uchafu
- Maumivu makali baada ya kukojoa
- Kutokwa na damu ukeni
Ute unaotoka kwenye uume unaweza kuwa wenye majimaji na kuonekana mweupe au kijivu. Dalili zingine za pangusa kwa mwanaume huwa kama ifuatavyo;
- Dalili za kuvimba kwa mrija wa mkojo
- Maumivu ya nyonga au tumbo la chini
- Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa au shindwa kukojoa
- Maumivu, au kuvimba korodani moja.
- Kisonono
Kisonono ni ugonjwa mwingine wa zinaa. Hutokana na bakteria aina ya Neisseria. Kisonono kinaweza kusababisha kutokwa na ute mweupe, wanjano au wakijani kwenye uume au kuongezeka kwa uchafu ukeni.
Dalili zingine za kisonono ni pamoja na;
- Kushindwa kukojoa au kuhisi maumivu makali wakati wa kukojoa
- Maumivu kwenye korodani
- Maambukizi katika njia ya mkojo(yaani UTI)
- Kutokwa na damu ya hedhi mara mbili kwa mwezi.
Je, Vipimo Vinafanyikaje?
Daktari anaweza kuchunguza ugonjwa wa kisonono na pangusa kwa kupima muonekano wa seli uliopatikana kwenye uchafu unaotoka ukeni au njia ya mkojo.
Je, Muda Gani Unapaswa Uonane Na Daktari?
Mgonjwa unapaswa kuonana na daktari endapo kama utaona ute wowote wenye muonekano na harufu isiyo ya kawaida. Uchafu au ute unaotoka wenye harufu mbaya ya shombo la samaki huonyesha uhitaji wa matibabu tena kwa haraka sana.
Ute wenye rangi nyeupe, kijivu, njano au kijani unaweza kuashiria maambukizi. Mwanamue anaweza kufaidika na matibabu ikiwa kama ute unaotoka kwenye uume wake utaambatana na mambo yoyote yafuatayo;
- Maumivu wakati wa kukojoa au wakati wa tendo la ndoa
- Maumivu baada ya kufika kileleni
- Ute unaotoka kwenye uume ambao huonekana nje pale unapokuwa na hisia
- Maumivu au kuvimba kwa korodani
- Maumivu maeneo ya tumbo la chini au nyonga
- Muwasho au hali ya kuwaka moto kwenye njia yamkojo, ukeni au mashavu ya uke
Nipende kuishia hapa ndugu msomaji, karibu katika kipindi cha maswali unaweza kutuma kupitia e-mail yako, au unaweza kutuma namba yako ya WHATSSAP unakaweza kuungana na group letu la mafunzo zaidi katika Jame Herbal Group.
Je, unahitaji huduma pia? Tupigie kwa namba hizi: 0752 389 252 au 0712 181 626.
Arusha-Mbauda
Karibuni sana.
Nimejifunza mengi kuhusu afya ya uzazi, makala nzuri nimependezwa nayo
Barikiwa sana dada, karibu sana
Nmejifunza mazuri kupitia makala yako ahsante,pia ngependa kujiunga na grp lako la whatsap
0753313765 whatsap no
Je ?mwanamke aliye toa mimba anaweza kushika mimba baada ya mda gani na anaona siku zake baada ya muda gani tangu kufanya abortion
Umenipa somo zuri sana,nimependa elimu yako nimejfunza mmb mengi mazuri!naomb nijiunge na group la whatsup kam lipo nahitaj elimu zaid
0757400105 join me please
Tuma namba yako tu ya wahatsap
0710702527
Nimejifunza mengi
Karibu sana
Karibu sana
Je mwanamke akiwa hajapata hedhi miez 3 halafu baadae akapata hedikwa muda wa siku 11 mfululizo Ikiwa inatoka na mwanzoni hedhi alikua akipata kwa muda wa siku nne mfululizo. Je, anaweza shika mimba siku 13 tangu hedhi itoke???
kWANZA UKIONA HUPATI HEDHI MIEZI HIYO YOTE UJUE KWAMBA UNA TATIZO KUBWA TU, NA UKIJA KUPATA HEDHI NA HUJALITIBU TATIZO HILO, NI VIGUMU KUPATA MIMBA
Ujumbe mzuri sana
Karibu sana ndugu Matofari, unaweza kutuma namba yako ya WHATSAP pia ukaungana na darasa letu