JE, NINI MAANA YA UPEVUSHAJI?

Upevushaji ni pale yai linapotolewa kwa ajili ya kurutubishwa. Kufahamu muda wako wa yai kupevuka ni njia mojwapo itakayo kusaidia kupata ujauzito kwa urahisi.
Yapo mabadiriko ya kimwili ambayo mwili wako huyapata kabla yai halijapevuka ili kwamba uweze kutambua vizuri kuwa ni wakati gani mwanaume unaweza kukutana na mke au mwenza wako ili kurutubisha yai. Upevushaji ni msemo uliotumiwa kuelezea njia ya yai linapokuwa likitoka kwenye mfuko wa yai. Yai lazima lirutubishwe ndani ya masaa 24 baada ya kuwa limepevuka.

Ovulation, Eggs, Sperm and Timing

Hapo chini kuna baadhi ya ufafanuzi muhimu utakaokufanya kuwa na vitu sahihi vifuatavyo:
1.     Yai zuri
2.     Kifuko cha yai kizuri
3.     Upevushaji mzuri
4.     Homoni ya estrogen katika kiwango kizuri
5.     Urutubishaji mzuri

 

NUKUU: Kabla ya upevushaji homoni ya estrogen huongezeka na joto hushuka.
Mayai yako yanapokomaa kwenye kifuko cha yai, huzarisha homoni ya estrogen kwa wingi zaidi.

 

Human egg | Muco cervical, Gravidez ectópica, Ervas

Zipo ishara 4 muhimu zinazoonyesha viwango vya juu vya homoni ya estrogen, navyo ni:

 

1.     Joto La Mwili:

 

 

Joto la mwili huwa ni dogo sana kwa siku kwa maana huwa ni baada ya masaa 3 yanayofuata baada ya kusinzia. Weka kipima joto chako kitandani kisha pima joto lako kabla hujaamka. Homoni ya estrogen hushusha joto la mwili. Kupanda kwa joto ya angalau 2/10 inaweza kuonyesha kuwa upevushaji wa yai tayari umeshatokea.

woman measuring basal body temperature
Joto la mwili linaweza kutumiwa kukadiria upevushaji ndani ya siku tatu. Joto la mwili linaposhuka, unaweza ukaweka kipimo chako cha ujauizto na ukaona chanya kuwa yai limeshapevuka.   

 

  1. Uteute Wa Shingo Ya Kizazi

 

Uteute wa shingo ya kizazi ni eneo muhimu sana la kuonyesha siku za hatari za mwanamke. Ute ni ule unaolinda mbegu za mwanaume zisiharibiwe na asidi inayokuwa ukeni. Ute wa shingo ya kizazi unaokuwa kama ute wa yai la kuku, ni ute mzuri unaoashiria mwanamke kupata ujauzito.

All About Cervical Mucus and Getting Pregnant – BabyHopes

Ute hubadirika katika kipindi chote cha mzunguko wa hedhi. Kwa muda  wa siku kadhaa katika kipindi cha upevushaji, aina ya ute wa siku za hatari huzarishwa; huwa una majimaji mengi, una asidi au hali kidogo ya uchachu.

 

 

  1. Nafasi Ya Shingo Ya Kizazi

 

Baada ya hedhi na moja kwa moja chini ya ushawishi wa homoni ya estrogen, shingo ya kizazi hupitia mabadiriko mbalimbali katika msimamo na muundo. Katika mzunguko wote wa hedhi,shingo ya kizazi hubaki kuwa ngumu kama ncha ya pua, na hushushwa chini na kufungwa. Hata hivyo, mwanamke anapokaribia kupevusha yai lake, shingo ya kizazi huwa laini kama mashavu ya uke, nayo hupanda juu na kufunguka kwasababu ya viwango vingi vya homoni ya estrogen wakati wa upevushaji wa yai.

 

Functions of the Cervix in Reproductive Health

Mabadiriko haya, huambatana na uzarishaji wa ute wa siku za hatari ambao husaidia kudumu na kusafiri kwa mbegu za mwanaume.

 

 

  1. Luteinizing Hormone

 

 

Hii huwa ni homoni inayozarishwa kwenye tezi ya pituitary. Kazi yake huwa ni kupasua kijiyai na kukiondoa nje baada ya kuiva au kukomaa pamoja na maendeleo ya corpus luteum. Corpus Luteum huwa ni  bonge la tishu za njano zinazokuwa zimeundwa na gamba lililopasuka ndani ya kifuko cha yai ambalo tayari limetoa yai lake. Kama yai limesharutubishwa, basi tishu hii hutengeneza homoni ya progesterone, inayohitajika kwa ajili ya kutengeneza ujauzito.  Ni muundo wa muda wa endocrine kwa wanawake unaohusika kwenye uzarishaji wa viwango vikubwa vya homoni ya progesterone ambayo ni homoni ya steroid tayari kwa ukuzaji wa  ngozi laini ya ukuta wa tumbo la uzazi(endometrium) ambayo itapokea yai lililorutubishwa na kutoa msaada na ulinzi.

Surrogacy Tips: How Do I Know When My Surrogate Is Ready For Egg ...

Homoni ya Luteinizing hujitokeza kabla na hulifanya yai likomae na kupevuka. Je, unaona hii ndio inaweza kuwa kiashiria kamili cha kukuonyesha kuwa ni lini unaweza kujaribu kushika ujauzito? Kama hali hii inatokea, basi upevushaji

unaelekea kuonekana hivyo, mayai yanakuja! Ni muda wa kuweka mbegu!

 

Jinsi Gani Unaweza Kutambua Yai Kama Limeshakomaa?

 

 

 

 

Kukomaa kwa yai au kupevuka mara nyingi hutokea baada ya masaa 24-36 baada ya upasuaji ya homoni ya Luteinizing. Ili kuwa mjamzito, basi tendo la ndoa linapendekezwa kufanyika ndani ya siku 2 baada ya upasuaji ya homoni ya luteinizing.

 

What is a Zona Pellucida? (with picture)

NUKUU: Katika mamilioni ya mbegu za mwanaume zilizomwagwa baada ya kufika kileleni, ni mbegu moja tu inayoruhusiwa kupenya na kutoboa membreni ya nje ya yai. Membreni huwa inakaa mahali pake wakati yai likisafiri kwenye mrija wa yai. Mbegu ya mwanaume lazima ipenyeze kwenye membreni hii nyembamba ili kuweza kulirutubisha yai. Kama urutubishaji utafanyika, basi membreni ya nje hutoweka, ili kuruhusu yai liweze kujipachika kwenye ukuta wa tumbo la uzazi.

Nipende kuishia hapa wapendwa, niwakaribishe wenye maswali wote karibuni sana.

 

Je, unahitaji huduma? Kwa mawasiliano tupigie kwa namba hii: 0752389252 au 0712181626

 

Arusha-Mbauda

 

Karibuni sana

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *