Je, Unaweza Ukapimwaje?
Ikiwa kama ulikuwa huwezi kupata ujauzito kwa muda mrefu, basi nakushauri utafute msaada kwa daktari katika hospitali za wilaya au mkoa ili kutathimini hali yako ya ugumba. Baada ya vipimo, basi unaweza ukafika James Herbal Clinic kwa ajili yatiba za asili.
Vipimo vinavyotumika ili kutambua hali ya ugumba kwa mwanamke huwa kama ifuatavyo:
- Kipimo Cha Kuonyesha Kuwa Yai Limepevuka(Ovuluation testing)
Kipimo hiki unaweza ukawa nacho nyumbani kwa ajili ya kupima ute ute unatoka ukeni kabla yai halijapevuka. Kipimo cha damu kwa ajili ya homoni ya projesterone, homoni ambayo hutengenezwa baada ya yai kupevuka, lakini pia inaweza kuonyesha kwamba yai linapevuka. Viwango vingine vya homoni kama vile prolactin pia vinaweza kuchunguzwa.

Unaweza ukakiona hapo kipimo hicho kinavyokuwa.
- Kipimo Aina Ya Hysterosalpingography
Hiki ni kipimo aina ya X-ray ambacho huingizwa kwenye mfuko wa kizazi wa mwanamke(uterus) ili kupima na maradhi yanayokuwa kwenye mfuko wa kizazi(uterine cavity). Kipimo hiki pia huingizwa na kupuliza maji yenye dawa ambayo hupita ndani ya mfuko wa kizazi mpaka kwenye mirija ya uzazi. Ikiwa kama kuna matatizo yoyote, basi utahitaji uchunguzi wa kina zaidi.

NUKUU: Katika wanawake wachache inaonyesha kipimo hiki kinaweza kikaonyesha majibu mazuri ya kuwa wana uwezo wa kupata ujauzito, hasa pale inapokutwa njia ya miriya ya uzazi iko wazi.
- Kipimo Cha Kubaini Ubora Na Kiwango Cha Mayai(Ovarian reserve testing)
Kwa kawaida kipimo hiki husaidia kubaini wingi na kiwango cha mayai yanayopatikana kwa ajili ya kupevushwa. Wanawake wenye upungufu wa mayai hasa wale wenye umri mkubwa zaidi ya miaka 35, wanaweza wakapimwa kupitia kipimo hiki.

Hiki ni kipimo ambapo wanaweza kuchukua damu tu na wakachunguza ili kuweza kubaini.
Unaweza ukaona hapo juu jinsi inavyokuwa katika kipimo hicho.
- Vipimo Vingine Vya Homoni
Vipi vipimo vingine vya homoni vinavyohusika kuangalia kiwango cha homoni za kupevusha mayai pamoja na homoni za pituitary na thyroid ambazo huongoza utaratibu wa mfumo wa uzazi.
![]()
NUKUU: Unapokuwa na tatizo la kupata ujauzito, tafadhali hakikisha unafanya vipimo katika maeneo hayo ili kuhakiki tatizo lako liko wapi.
- Kipimo Cha Kuzamisha(Imaging Test)
Kipimo cha ultrasound kinachopima nyonga(pelvic ultrasound) huchunguza magonjwa ya mirija ya uzazi au tumbo la uzazi(uterine). Wakati mwingine kipimo aina ya hysterosonograph hutumika kuangalia maelezo ndani ya tumbo la uzazi(uterus) ambayo hayawezi kuonekana kwa kipimo cha kawaida cha ultrasound.
Nawashauri sana kina mama wote wenye matatizo ya kutopata ujauzito kuwa, hebu jaribu kuvishika vipimo hivi ninavyokuelekeza hapa na uviweke kichwani ili unapoenda kwa daktari hospitalini aweze kukuhudumia vizuri kulingana na vipimo na tatizo ulilonalo.
/MRI-test-569c3e173df78cafda99a64e.jpg)
NUKUU: Kulingana na dalili ulizo nazo, daktari wako anaweza akaamuru kutumia kipimo aina ya Hysteroscopy ili kuangalia magonjwa yaliyomo kwenye mirija ya uzazi au tumbo la uzazi(uterus).
- Kipimo Cha Laparoscopy
Huu upasuaji mdogo wa kushitukiza huhusika kutengeneza kuchana kichale kidogo tu chini ya kitovu na kuingiza kifaa chembamba chenye uwezo wa kutazama na kuchunguza mirija yako ya uzazi, vifuko vya mayai pamoja na mfuko wa kizazi.

NUKUU: Kipimo cha laparoscopy kinaweza kubaini ukuta laini wa mfuko wa kizazi kama umevimba, majeraha, hali ya kuziba kwa mirija pamoja na matatizo kwenye vifuko vya mayai na kwenye kizazi pia.
Nipende kuishia hapa mpendwa msomaji, nikaribishe kipindi cha maswali na maoni yako kupitia tovuti yetu, karibu sana. Kumbuka pia tuna darasa letu katika mtandao wa telegram, hivyo unaweza ukatuma namba yako ya whatssap ili upate link ya kuweza kuungana nasi katika kujifunza mambo ya afya bure.
Je, unahitaji huduma? Tupigie kwa namba zetu hizi: 0752389252 au 0712181626,
Arusha Mbauda.
Wote mnakaribishwa.