JE, UNAJUA SABABU ZINAZOPELEKEA WANAWAKE WENGI KUTOKUSHIKA MIMBA?

 

 

Mwanamke kutokushika mimba kumegawanyika katika makundi makuu mawili.

Kwanza ni hali inayoitwa “Primary infertility” ambapo mwanamke hana historia ya kupata ujauzito. Pili, kuna hali inayoitwa Sekondari infertility, hapa mwanamke anayo historia kama aliwahi kupata ujauzito haijalishi kama alizaa au alitoa ama iliharibika.

Matatizo ya kutoshika mimba kitaalamu tunaita ‘infertility’ ama ugumba.

Kutoshika mimba kwa mwanamke husababishwa na mambo mengi ingawa tutakuja kuona vyanzo vikuu, nayo ni haya:

  • Maambukizi katika viungo vya uzazi
  • Hali duni ya lishe
  • Magonjwa sugu ambayo huathiri hali ya ugumba wa mwanamke.

 

Chanzo Chake

 

Chanzo cha matatizo haya vinahusisha aina zote mbili za ugumba yaani, Primary na Sekondari. Kwanza kabisa ni chanzo kinachohusu upevushaji wa mayai(Ovulatory). Tatizo hili huathiri wanawake kwa kiasi kikubwa ambapo mwanamke anapata siku zake kama kawaida lakini hapevushi mayai. Hii husababishwa na matatizo katika mfumo wa homoni mwilini, tatizo linaweza kutokea lenyewe ktokana na mabadiriko ya mwilini au mabadiriko  yanayohusiana na matumizi ya dawa za homoni kutumika kiholela au matumizi ya baadhi ya vyakula au vipodozi.

 

Dalili za upevushaji mayai zipo nyingi, lakini kubwa ni kwa mwanamke kupata ute wa uzazi ambapo uko wa aina tatu. Pia upevushaji tunaweza kuuona kwa kutumia vifaa maalum ambavyo unatumia mwenyewe nyumbani kwa kupima mkojo siku unazohisi unaweza kupata mimba.

Tatizo linguine la chanzo cha ugumba ni kwenye mirija, mirija inaweza kuziba, kutanuka au kuweka usaha au maji. Maambukizi katika mirija au upasuaji wa mimba nje ya kizazi au kufunga kizazi. Utoaji wa mimba, maambukizi ya mara kwa mara ukeni husababisha athari katika kizazi na mirija ya mayai. Matatizo ya mirija husababisha ugumba kwa kiasi kikubwa ambacho ni kati ya silimia 15 hadi 40 kwa wanawake ambacho ni kiwango kikubwa kuliko matatizo mengine.

Mwanmke pia anaweza kuwa na kasoro  katika tabaka la ndani la kizazi ambapo linatoka kwa nje badala ya kuwa ndani. Hali hii kitaalam inaitwa ‘Endometriosis, ’ nitakujakulielezea baadaye katika makala nyingine. Sio tatizo linalojitokeza kwa ukubwa sana lakini linaathiri baadhi ya wanawake. Mwanamke mwenye tatizo hili hulalamika maumivu chini ya tumbo na huwa makali wakati wa hedhi na kusababisha damu ya hedhi kutoka kidogokidogo, na mwanamke hupoteza uwezo wa kushika mimba.

Matatizo ya mwanaume kushindwa kufanya tendo la ndoa, anamaliza lakini manii hazitoki, pia husababisha ugumba kwa mwanaume ambapo humuathiri mwanamke. Mwanaume pia anaweza kufanya tendo la ndoa vizuri, anatoa manii lakini mbegu hakuna, hili pia ni tatizo kubwa.

Mwanaume anaweza kupata tatizo la uzazi hata kama anayo historia ya kumpa mwanamke mimba au kuwa na watoto, kwahiyo ni vyema naye kufanyiwa uchunguzi endapo wanatafuta mtoto au ujauzito kwa mwaka mmoja bila ya mafanikio.

Ugumba pia unaweza kutokea na baada ya uchunguzi wa kina inaonekana mume wala mke hana tatizo, hali hii kitaalamu inaitwa ‘Unexplained infertility’

UCHUNGUZI

 

Matatizo ya ugumba yanazidi kuwa makubwa sana, nayo yanazidi kuumiza watu wanaotafuta ujauzito. Tunaziona sababu kuu za ugumba lakini pia mapungufu ya lishe mwilini nayo ni mojawapo ya visababishi.

Napenda kuwashauri tu wapendwa wasomaji wenye matatizo haya kuwa ni vyema kabisa kufanya uchunguzi kwa madaktari wa magonjwa ya kina mama na matatizo ya uzazi katika hospitali za mikoa au Wilaya. Yafaa sana kupata vipimo vya damu ili kuangalia homoni, pia vipimo vya Ultrasound ili kuangali mirija ya uzazi.

Ikiwa wewe umeshawahi kupata vipimo na kupewa majibu, basi unaweza kupata tiba za asili kutoka James Herbal Clinic. Kwa mawasiliano tupigie: 0752389252 au 07121818626

Karibu sana.