JE, UNAJUA VYANZO, DALILI NA MADHARA YA UVIMBE SEHEMU YA VIFUKO VYA MAYAI(OVARIAN CYSTS)?

 

Uvimbe kwenye mayai ya mwanamke (ovary), hutokana na mkusanyiko wa majimaji yanayozungukwa na kuta nyembamba ndani ya mayai ya mwanamke. Uvimbe huu ambao hupatikana ndani ya mayai ya mwanamke ndio unaojulikana kama ovarian cyst. Uvimbe huu hutokea kwa wanawake wa umri wowote ule na mara nyingi huonekana kwa wanawake waliofikia kikomo cha umri wa kupata ujauzito. Lakini kwanza hebu tuelezee juu ya mayai ya mwanamke.

 

Kwa kawaida mwanamke anakuwa na mayai mawili katika mwili wake. Yai moja upande wa kulia na yai jingine upande wa kushoto kwake. Mayai haya hupatikana pembezoni mwa mfuko wa uzazi (uterus).

Tukiangalia tunaona kuwa wanawake wengi wamekuwa wakisumbuliwa na tatizo hili mara kwa mara. Hata hivyo aina ya uvimbe huu hasa ule ambao tayari umeshapasuka unaweza kusababisha dalili mbaya zaidi. Napenda kuwashauri wapendwa kinamama, ili kuidhibiti afya yako, yafaa ukawa unapata vipimo kila mara na kutambua dalili ambazo zinaweza kuonyesha ishara ya tatizo hili.

Dalili Zake

 

Mara nyingi vivimbe katika vifuko vya mayai(Ovarian Cysts), huwa havionyeshi dalili na hivyo huweza kutoweka bila kutumia matibabu. Lakini uvimbe huu unakuwa mkubwa zaidi, huonyesha dalili zifuatazo:

  • Maumivu kwenye nyonga hasa maeneo ulipo uvimbe sehemu za tumbo la chini
  • Tumbo kujaa au kuwa zito
  • Tumbo kuunguruma
  • Maumivu na kuhisi homa au kutapika

Uonapo dalili kama hizo, ikiwapo kupumua kwa haraka, kichwa kuuma, ngozi kuwa na jasho la kunatanata au mwili kuchoka, basi wahi haraka hospitali ukamuone daktari ili upate vipimo.

Visababishi Vyake

 

Mayai haya ya mwanamke huanza kuzalisha mayai ya uzazi yanayojulikana kama ovam, na mayai hayo ya uzazi hukuwa ndani ya mayai ya mwanamke (ovary) kwa kuchochewa na baadhi ya homoni. Katikati ya mwezi, siku ya kumi na nne, masaa 24-36 baada ya kiwango cha kichocheo kuwa juu, mayai ya uzazi hutolewa katika kila ovari na hii ndio hujulikana kama ovulation au kufikia kilele upevukaji wa mayai. Mayai haya ya uzazi huishi kwa masaa machache hadi masaa 24 ikiwa hayatorutubishwa na mbegu kutoka kwa mwanamume. Mabaki ya mfuko wa mayai ya uzazi yanayojulikana kama follicle ndani ya ovari, hugeuka na kuwa kovu katika sehemu lilipotoka yai(corpus luteum) ambayo huhusika na utoaji wa kichocheo au homoni aina ya progesterone kwa wingi. Homoni hii ya progesterone ndio inayosababisha mfuko wa uzazi kujiandaa kwa kujikita yai (implantation) lililorutubishwa kwa mbegu ya kiume ndani ya mfuko wa uzazi kwa kuongeza unene kwenye kuta zake. Yai hili husafiri hadi kwenye mfuko wa uzazi ambako hukua na kuwa mtoto. Kama upachikwaji wa yai liliorutubishwa hautafanyika, basi ndani ya wiki mbili, kovu katika sehemu lilipotoka yai (corpus luteum) huanza kusinyaa na kupotea na kusababisha kushuka kwa kiwango cha homoni aina ya progesterone na estrogen. Kushuka kwa viwango vya vichocheo hivi ndio husababisha mfuko wa uzazi kuanza kutoa mabaki ya kuta zake pamoja na yai la uzazi na hii ndiyo pale mwanamke anapotoka damu ukeni inayojulikana kama hedhi. Unaweza ukajiuliza, ni kwa nini nimeanza na maelezo haya, lakini jibu ni kutaka kuonyesha umuhimu wa mayai ya uzazi kwa mwanamke pamoja na kazi yake.

 

VIHATARISHI

Vihatarishi vya vivimbe katika vifuko vya mayai hutokana na mambo yafuatayo:

  • Matatizo Ya Homoni: Hali hii hutokana na matumizi ya vidonge vinavyotumiwa kwa ajili ya kupevusha mayai.
  • Ujauzito: Wakati mwingine uvimbe unaojitokeza huweza kukaa kwa kipindi cha ujauzito
  • Endometriosis: Hii huwa ni hali inayosababisha seli za ukuta wa tumbo la kizazi kuota nje ya kifuko chako cha kizazi. Baadhi ya tishu zinaweza kushikamana na vifuko vyako vya mayai na kutengeneza uvimbe.
  • Madhara mabaya katika nyonga: Ikiwa kama maambukizi ya bakteria kama vile UTI, fangasi, pangusa(Chlamydia) au kisonono, wakisambaa na kufika maeneo ya vifuko vya mayai(ovaries), wanaweza kusababisha uvimbe.

 

MADHARA YAKE

 

Madhara yanayojitokeza baada ya tatizo hili kukosa matibabu ni kama ifuatavyo:

  • Kujisokota Kwa Kijifuko Cha Yai(Ovarian Torsion): Uvimbe wa kifuko cha yai unapokuwa mkubwa unaweza kusababisha kifuko kuondoka, na kuongeza maumivu yatokanayo na kujisokota kwa kifuko chako cha yai. Dalili zinazoanza kujitokeza huwa ni maumivu makali ya nyonga, kichefuchefu au kutapika. Kujisokota kwa kifuko cha yai kunaweza pia kupunguza au kusimamisha damu kububujika kuelekea kwenye vifuko vya mayai.
  • Kupasuka: Uvimbe unaopasuka unaweza kusababisha maumivu makali na damu kuvuja ndani ya tumbo. Kadiri uvimbe unavyozidi kuwa mkubwa, ndivyo kunazidi kuwepo na hatari ya kupasuka kwa uvimbe. Kazi ngumu ikiwamo na tendo la ndoa pia vyaweza kuongeza madhara kwa muhusika.

MATIBABU

James Herbal Clinic tuna dawa nzuri za asili zenye uwezo wa kuondoa tatizo hili. Unahitaji huduma, tafadhari tupigie: 0752389252 au 0712181626