JE, UNAWEZAJE KUJIEPUSHA NA MAAMBUKIZI YA MAGONJWA KATIKA VIA VYA UZAZI(PELVIC INFLAMMATORY DISEASES) AU PID?

Inaonyesha kuwa yaweza ikawa ni vigumu sana kwa baadhi ya watu kuweza kujilinda ili kujiepusha na maambukizi ya magonjwa katika via vya uzazi au PID(Pelvic Inflammatory Diseases). Wakati mwingine bakteria wanaokuwa kwenye uke wanaweza kusafiri kupanda juu kwenye viungo vyako vya uzazi na kusababisha tatizo la PID. Lakini unao uwezo wa kuipunguza hatari au janga hili kwa kutotumia madawa au sabuni zenye marashi makali kwa ajili ya kuoshea sehemu hizo za uke. Unaweza pia ukajiepusha na magonjwa ya zinaa kwa kutofanya tendo la ndoa kinyume na maumbile. Napenda nikushauri mambo haya, unapokuwa unafanya tendo la ndoa ili kujihadhari sana na magonjwa ya zinaa kwa kufuata hatua hizi zifuatazo:

 

  1. Tumia Kondom

 

 

Kondom ni njia moja nzuri sana ya kuzuia magonjwa ya zinaa unapofanya tendo la ndoa. Kwasababu sio kwamba mwanaume anapofika kileleni na kumwaga mbegu zake ndipo ataweza kukuambukiza magonjwa! Inafaa sana unapokuwa makini kujiandaa kuvaa kondom kabla uume haujagusa uke wako.

 

  1. Kufanya Vipimo

 

 

Fanya vipimo mara kwa mara wewe pamoja na mpenzi wako ili kuhakiki magonjwa ya zinaa. Hakikisha kila mmoja anampa mwenzake taarifa za vipimo kabla hamjakutana kimwili.

 

 

  1. Jifunze Kuwa Mwaminifu Kwa Mwenzi Wako

 

 

Inaonyesha kwamba baadhi ya wanaume wanashindwa kuwa waaminifu kwa wenzi wao. Tabia hii utakuja kuigundua pale dada anapomwambia mwenzi wake kuwa twende tukapime. Baadhi ya vijana wa kiume wanaposikia habari ya kupima huanza kuleta maneno mengi ili kumchenga mwenzi wake. Lakini kumbuka kwamba, kuwa na mpenzi mmoja na kuwa mwaminifu kwa mwenzako ni  jambo zuri mno kwani itakusaidia kujiepusha na magonjwa ya maambukizi au zinaa.

 

  1. Kuwa Na Mpenzi Mmoja

 

 

Maambukizi ya magonjwa ya zinaa mara nyingi husababishwa na tabia ya mwanaume au mwanamke pale anapokuwa na wapenzi wengi. Napenda nikushauri ndugu mpendwa unayesoma makala hii kuwa ni vyema ukajifunza kuwa na mpenzi mmoja tu. Mpende mpenzi wako na umtimizie mahitaji yake. Epuka tamaa maana inaua.

 

  1. Kupiga Bomba Au Kuosha Sehemu Za Uke Kwa Sabuni Za Marashi

 

 

Hali ya kupiga bomba au kuosha sehemu za uke kwa kutumia sabuni zenye marashi makali husababisha kuondoa bakteria wa kawaida wanaokuwa ndani ya uke ambao hufanya kazi ya kuulinda uke ili usipatwe na maambukizi. Tabia au mazoea ya kupiga bomba pia yanaweza kukuhatarisha ukapatwa na vimelea wa PID wakapita na kuanza kusafiri katika maeneo, kama vile mfuko wa uzazi, vifuko vya mayai, pamoja na mirija ya uzazi.

 

Je, unahitaji huduma? Karibu katika James Herbal Clinic, Arusha-Mbauda.

 

Kwa mawasiliano tupigie: 0752 389 252 au 0712 181 626.

 

Karibuni sana.