JE, WAJUA CHANZO, DALILI NA MADHARA YA UGONJWA WA KASWENDE?

 

Kwa kawaida ugonjwa huu huambukizwa kwa njia ya kujamiiana au kugusa majimaji yanayotoka kwenye vipele vya mgonjwa wa kaswende. Pia uchangiaji wa taulo au shuka ya mgonjwa wa kaswende unaweza kusababisha kupata ugonjwa huo. Ugonjwa huu huonekana sana kwa wanawake wenye umri wa miaka 15-24 na wenye umri wa miaka 35.

Kaswende (syphilis) ni mojawapo kati ya maradhi ya zinaa ambayo inasababishwa na bakteria inayofahamika kama Treponema pallidum.

Katika hatua za mwanzo, vipele katika sehemu za uzazi huanza kujitokeza muda mfupi baada ya maambukizi ambavyo baadaye hupotea vyenyewe.

Kama ugonjwa hautatibiwa, maambukizi huendelea kwa miaka hadi 25, yakishambulia mifupaubongo na moyo na kusababisha madhara mengine yanayotokana na matatizo katika mfumo wa fahamu kama vile homa ya uti wa mgongo na magonjwa ya moyo na kiharusi.

Kaswende wakati wa ujauzito unaweza kuwa hatari kubwa kwa kiumbe tumboni, kama vile kusababisha kutoumbika vizuri (deformity) na kifo.

Siku hizi kaswende inaweza kutibika kwa urahisi kwa kutumia tiba za asili ambazo ni NEOTONIC na Fresh Herba.

 

Dalili Zake:

 

 

Dalili na ishara za kaswende hutofautiana kulingana na hatua iliyoko kati ya hatua nne. Hatua ni ya kwanza, ya pili, ya tatu, ya nne na ya tano.

 

  1. Ugonjwa wa Kaswende ya awali(primary syphilis): Aina hii hutokea kidonda kidogo cha mviringo ambayo bakteria wameingilia na hutokea kati ya siku 10 hadi miezi mitatu(yaani kuanzia wiki 2 hadi 6) baada ya mtu kupata maambukizi ya kaswende.

Kindonda hiki kinaweza kutokea sehemu ya njia ya haja kubwa, shingo ya kizazi(cervix), mdomoni, kwenye uume, ulimi, kwenye uke, pamoja na sehemu zingine mwilini….Kwa kawaida kidonda huwa hakiambatani na maumivu na kwa kuwa kinaweza kujitokeza katika sehemu zilizojificha kama vile kwenye shingo ya kizazi, na ndio maana huwa sio rahisi mtu kutambua kuwa ana ugonjwa wa kaswende. Robo tatu ya wagonjwa wa kaswende wanaposhindwa kupatwa tiba mapema huishia kwenye kundi la kaswende ya hatua ya pili(second syphilis).

 

  1. Hatua ya pili ya kaswende(second syphilis): Hatua hii hutokea wiki 4-10 baada ya mtu kupata kaswende ya awali. Dalili ya aina hiyo ya kaswende huwa ni pamoja na uchovu, kuumwa kichwa, homa, kunyofoka nywele, vidonda vya koo, kuvimba kwa matezi mwili mzima, Maumivu ya mifupa au kupungua uzito. Kaswende ya aina hii huwa inakuwepo kwa wiki kadhaa na hupotea bila hata kupata tiba kwa mtu aliye athirika. Pia inaweza kujirudiarudia kwa katika kipindi cha mwaka mmoja na mtu huingia kwenye kundi la hatua ya ugonjwa wa kaswende iliyojificha(Latent Syphilis)
  2. Kaswende iliyojificha(Latent Syphilis): Aina hii ya kaswende hujulikana kama kaswende ambayo inaweza kuthibitika tu kwa kutumia vipimo vya maabara(serological test). Nayo imegawanyika katika makundi mawili; (1). Kaswende iliyojicha ya awali(early latent syphilis) ambayo hutokea ndani ya kipindi cha mwaka mmoja baada ya mwathirika kuona kaswende aina ya pili(secondary syphilis) kama nilivyoeleza hapo juu mwanzo. Aina hii huwa na dalili zinazojirudiarudia kama ilivyo kaswende aina ya pili…..Mgonjwa anapokuwa na kaswende aina hii huwa hapati dalili zozote na uwezo wake wa kuambukiza mtu mwingine unakuwa chini au hawezi kumwambukiza mtu mwingine ugonjwa huo.
  3. Kaswede ya baadaye(Tertiary syphilis): Asilimia ya wagonjwa wa kaswende ambao hawakupata tiba hapo awali huingia kwenye kundi hili hutokea miaka 15-30 baada ya maambukizi ya kaswende hapo awali. Aina hii inaweza kuathiri viungo vya mwili kama vile macho, ubongo, mishipa ya fahamu(neurosyphilis), viunganishi vya mifupa(jointi), uti wa mgongo, moyo, mishipa ya damu, na hivi vyote husababisha madhara makubwa kama vile, upofu wa macho, magonjwa ya moyo, magonjwa ya akili, kuwa kiziwi, kupungukiwa kumbukumbu na hatimaye kifo. Aina hii ya kaswende pia inaweza kuathiri mfumo wa usagaji chakula, mfumo wa upumuaji, na mfumo wa uzazi.
  4. Kaswende ya kuathiri(Congenital syphilis): Aina hii ya kaswende hutokea baada ya ujauzito au baada ya mtoto kuzaliwa. Robo mbili ya watoto wanaozaliwa huwa hawaonyeshi dalili zozote. Nusu ya watoto wenye maambukizi ya kaswende hufariki muda mfupi kabla ya kuzaliwa au baada ya kuzaliwa. Dalili za aina hii ya kaswede kwa mtoto mchanga zinaweza kutokea baada ya kuzaliwa au wiki 2 hadi miezi 3 baada ya kuzaliwa, nazo huwa kama ifuatavyo:
  • Kushindwa kukaa ama kupungua uzito
  • Kuhisi homa
  • Kupatwa na hasira haraka
  • Kutochongoka kwa pua au pua kuwa bapa.
  • Kupatwa na vipele mdomoni, sehemu za siri au njia ya haja kubwa
  • Kutokwa na majimaji puani
  • Ini au bandama kuwa kubwa
  • Ngozi kuwa ya njano na kupatwa na upungufu wa damu mwilini.

Dalili za ugonjwa wa kaswende kwa mtoto mkubwa huwa kuathirika kwa meno, Maumivu ya mifupa, upofu wa macho, kupungua kwa uwezo wa kusikia ama kuwa kiziwi. Kupatwa na ukungu kwenye mbozi za macho, kupatwa na vidonda sehemu ya njia ya haja kubwa au sehemu ya uke, ngozi kuwa na mabaka meusi kwenye midomo, sehemu za siri au njia ya haja kubwa, Maumivu kwenye mikono au miguu na kuvimba kwa viunganishi vya mifupa.

James Herbal Clinic tunazo dawa za asili zenye uwezo wa kutibu na kuondoa tatizo hili. Unahitaji huduma, naomba utupigie kwa namba hizi: 0752389252 au 0712181626