Katika mwili wa binadamu kuna tatizo la kiafya ambalo huambatana na dalili za mtu kuhisi maumivu, kuhisi kuwaka moto, na kufa ganzi kwa viungo vya pembezoni mwa mwili yaani miguu na mikono. Tatizo hili kitaalamu hujulikana kwa jina la Peripheral Neuropathy. Matatizo haya kiafya(miguu au miko kufa ganzi, baridi au maumivu) husababishwa na kuumia au kudhoofika kwa neva za pembezoni za mwili(miguu au mikono na hivyo kupotea kwa uwezo wa kufanya kazi wa neva katika sehemu husika miguu au mikono.
Dalili Zake
Dalili zinazoambatana na ugonjwa huu huwa kama ifuatavyo:
- Mtu kuhisi ganzi
- Kushindwa kushika ama kunyanyua kitu, kuchoka kwa misuli, nk
- Maumivu ama kuwaka moto maeneo ya miguuni au mikononi
Miongoni mwa mambo ambayo hupelekea neva hizi za pembezoni kushindwa kufanya kazi vizuri ni haya yafuatayo:
- Kupungua kwa virutubishi mwilini, hasa mkusanyiko wa vitamini B(Vitamini B complex).
- Matumizi ya dawa mfano dawa za kutibu kifua kikuu au za kupambana na virusi vya Ukimwi
- Uzito mkubwa wa mwili
- Ugonjwa wa kisukari
- Shinikizo la juu la damu
Ushauri
James Herbal Clinic tunapenda kukushauri kuwa uonapo dalili kama hizo, ni vyema ukafika katika hospitali za Wilaya au Mkoa ili kupata uchunguzi kupitia vipimo mbalimbali vya magonjwa ya moyo, kisukari, nk. Yafaa pia ukapata ushauri wa madaktari ili kutatua tatizo hilo.
MATIBABU
James Herbal Clinic tuna dawa nzuri za asili zenye uwezo wa kuondoa matatizo ya kufa ganzi miguu au kuhisi baridi, nazo ni NEOTONIC, PHYTOGUARD na CARD HERB.
Unahitaji huduma, tafadhali tupigie: 0752389252 au 0712181626
Thanks
Nasumbuliwa na ganz mikononi na miguu kuwaka moto,,ila mara nyingine nikiwa natumia cm ya mkonon ndo hyo ganz huwa inakuja shida n nn?
Tatizo la mwendo wa damu hilo naomba ukapime kwanza
Nasumbuliwa na ganzi mikononi na miguu kuwaka moto nahtaji vipimo nitawapataje?
John uko mkoa gani ndugu? Je, unaweza kutuma namba yako ya whatssap?
Dr Habari za leo..samahani mm nasumbuliwa na GANZI kuanzia mdomoni,mikono ,na miguu, inashindwa kutembea vzr,,na miguu na USO unavimba lkn sina sukari wala presha. Nakosa raha kabisa. Chanzo hakijulikani nilipima clinic muhimbili.. Dawa ni BEI gani ya kumaliza tatizo hilo.
Ahsante kwa huduma tumezijua athali na jinsi ya kutibu
Ahsante kwa huduma tumezijua athali na jinsi ya kupata tiba
Nashikwa ganzi kwa mkono wa left na mguu shida ineza kua gani
Mim ninaganzi ya mguu/mkono kwa upande mmoja nashindwa kutembea na kushika chochote. Sasa naomba ushauri kwako maana leo miaka miwili sasa
Pole mno ndugu, je utakuwa na namba ya Whatsap tuweze kukusaidia zaidi?