Ndugu msomaji nimeamua kulitoa somo hili kwa upana zaidi na kwa kulichanganua ili kila mmoja apate kuelewa kuwa PID ni nini, ina dalili gani, na madhara gani!
Kwanza neno PID ni neno la kiingereza ambalo kirefu chake ni “Pelvic Inflammatory Disease”, ambalo kwa Kiswahili maana yake ni maambukizi ya magonjwa katika via vya uzazi.
Maambukizi katika via vya uzazi kwa kawaida hujulikana kama PID, ni maambuki yanayoathiri viungo vya uzazi vya mwanamke. PID hakika hutokana na mchanganyiko mbalimbali wa magonjwa ya zinaa, hasa yaliyosababishwa na bacteria wa Pangusa(Chlamydia) au kisonono. Ugonjwa wa PID unapokaa muda mrefu bila kutibiwa, unaweza kusababisha uharibifu mkubwa usiobadirika katika mfumo wa uzazi wa mwanamke, hasa katika mfuko wa kizazi(uterus), vifuko vya mayai(Ovaries), na mirija ya mayai(fallopian tubes).
Ugonjwa huu unapokaa muda mrefu bila kutibiwa humfanya mwanamke kupatwa na ugumba. Inaonyesha asilimia kubwa leo katika jamii, wanawake wengi wamekuwa wakisumbuka na ugonjwa huu.
Je, Nini Kinachosababisha Ugonjwa Huu Wa PID?
Ugonjwa wa kisonono pamoja na Pangusa(Chlamydia) ndio vyanzo vikuu vya maambukizi katika via vya uzazi wa mwanamke.
Mwili wa mawanamke unapokuwa na afya kamili, mlango wa kizazi huwa na nguvu ya kuzuia bakteria wasiweze kuingia katika viungo vya ndani vya uzazi kutoka ukeni.
Hata hivyo wakati mlango wa kizazi unapokuwa wazi na kuruhusu magonjwa ya zinaa kuingia, hasa kisonono na pangusa, mlango wa kizazi hupata maambukizi na kisha hupoteza uwezo wake na hivyo kuruhusu maambukizi na bacteria kuingia na kufika juu kwenye viungo vya uzazi.
Je, Jinsi Gani PID inavyokupata?
Japo inakuwa tayari imesababishwa na magonjwa mengine ya zinaa, PID huambukizwa kwa urahisi ikiwa kama mtu atashindwa kufuata njia za kuepukana na mienendo ama tabia mbaya. Hapa kuna mambo ambayo huwafanya wanawake kupatwa na tatizo hili kwa urahisi sana, nazo ziko kama ifuatavyo:
- Kuwa na wapenzi wengi ama kutoka nje ya ndoa
- Kuanza mambo ya mapenzi mapema hasa chini ya miaka 25
- Kupiga bomba ukeni yaweza kusaidia vimelea kuingia ndani na kusababisha maambukizi katika viungo vya uzazi
Je, Nini Dalili Za Ugonjwa Wa PID?
Kama ilivyo katika magonjwa mengi ya zinaa, PID inaweza kuendelea kwa kuonyesha dalili za kawaida ama kutokuonyesha dalili zozote. Hali hii yaonyesha kuwa ni vyema sana kufanya uchunguzi wa vipimo mara kwa mara kwa daktari. Kama PID ikianza kuonyesha dalili zozote, zaweza kuwa kama ifuatavyo;
- Maumivu ya tumbo chini ya kitovu.
- Kutokwa na uchafu ukeni, hasa wenye rangi ya njano unaoelekea kuwa kijani kwa mbali ukiwa na harufu mbaya.
- Kuhisi Maumivu ama hali ya kuungua wakati wa kukojoa
- Homa
- Kuhisi kichefuchefu ama kutapika
- Kuhisi Maumivu wakati wa tendo la ndoa ama kutokwa na damu wakati wa tendo la ndoa.
- Kupata hedhi katikati ya hedhi, yaani waweza kupata hedhi mara 2 ndani ya mwezi 1.
Je, Unawezaje Kutambua Kuwa una PID?
Kadri inavyoonyesha kuwa huna dalili zozote za PID, ni vyema kila mara kwenda katika zahanati ama hospitali ili kupata vipimo kuweza kukuhakikishia kuwa uko salama, na hauna maambukizi yoyote ya zinaa.
Wanawake wadogo chini ya umri wa miaka 25, mara nyingi wanapatwa na janga la maambukizi haya kwa urahisi, na inafaa wapate vipimo angalau hata mara moja kwa mwaka. Pia unapoona dalili zozote tofauti, naomba usisite kufika hospitalini ili kufanya uchunguzi na kuhakiki tatizo lako.
.
Hakuna kipimo maalumu cha PID, lakini hata hivyo daktari anaweza kupima maambukizi kwa kuchukua vitu vinavyotoka ukeni, ama mkojo. Vipimo hivi hupelekwa maabara kwa ajili ya uchunguzi ambao hubaini kuwa huenda una vimelea wanaosababisha maambukizi. Ikiwa kama daktari atakuwa amefikiria tu ama kudhania, unaweza kuambiwa uende ukapate vipimo vingine zaidi, vikiwemo;
- Vipimo vya Ultrasound ambavyo hurusu kuona picha ya viungo vyako vya uzazi kwa kutumia sauti za mawimbi.
- Kipimo cha Endometrial biopsy, ambacho kinamaanisha kuwa kwamba daktari wako atachukua ute ute kidogo kutoka ndani ya uke kwa ajili ya upimaji mwingine zaidi.
- Kipimo kupitia kifaa cha kuingiza ndani ya uke.
Je, Maambukizi Ya PID Yanaweza Kupona?
Ni vyema kufanya vipimo na kuanza matibabu mapema kadri iwezekanavyo. Vinginevy PID inaweza kuendelea na kukomaa na kusababisha madhara makubwa katika mfumo wa uzazi ambayo yaweza kushindwa kutibika. Lakini uanzapo kufanya matibabu yafaa pia hata mwenzi wako apate matibabu japo hajaonyesha dalili zozote. Ikiwa kama hatapata matibabu, anaweza kukufanya upate tena maambukizi mara unaporudi kufanya mapenzi na yeye. Hakikisha pia unamaliza matibabu yako kulingana na maelekezo ya tabibu wako ijapokuwa unaona dalili za maambukizi zinatoweka. Kumbuka pia unapotumia vidonge kwa muda mrefu na vikashindwa kukusaidia, PID huzidi kukua na kusababisha majipu ndani ya uzazi ambayo humfanya mgonjwa kutokwa na vitu kama usaha ukeni. Hali hii yaweza kusababisha madhara makubwa hasa katika vifuko vya mayai na kwenye mirija ya uzazi pia.
Je, Ugonjwa Huu Waweza Kutibika?
PID inapona kwa kutumia tiba za asili zenye uwezo wa antibiotic tu. Napenda kusisitiza kuwa JAMES HERBAL CLINIC tunazo dawa za antibiotic ambazo ni VITAMAKA, REDEEMER na FRESH HERB. Hata hivyo inafaa ieleweke kuwa upatikanaji wa tatizo hili hutegemeana na jinsi gani PID imeharibu mwili wako. Ikiwa kama mgonjwa kawahi kupata vipimo na kuanza matibabu, basi uponaji wake utakuwa ni wa haraka pia. Lakini kama tatizo litadumu muda mrefu, linaweza kusababisha madhara makubwa hasa ugumba kwa mwanamke.
Jinsi Gani Unaweza kuepukana na PID?
Asilimia 90% ya maambukizi katika via vya uzazi(PID) husababishwa na Kisonono pamoja na Pangusa(Chlamydia). Kama ilivyo magonjwa mengine ya zinaa, mara nyingi huambikizwa kwa njia ya kujamiiana. Japo kuepukana na maambukizi ya PID unashauriwa kuwa na mpenzi mmoja unayemwamini na kutumia Kondom wakati unapofanya tendo la ndoa. Kama nilivyosema awali pia, kuwa yafaa kutembelea katika vituo vya afya mara kwa mara ili kuhakiki afya yako. Hata kama umeshawahi kupata aina moja ya ugonjwa wa zinaa, bado inachukua mpaka kufikia kuwa PID, hivyo unapokuwa na mazoea ya kufanya uchunguzi wa vipimo kwa ajili ya afya yako, yaweza kukusaidia kujikinga na tatizo la PID.
Je, PID inaweza Kusababisha Nini?
Unapofanya vipimo na kuanza matibabu mapema, PID haiwezi kusababisha madhara yoyote mwilini mwako. Hata hivyo, ikiwa kama utazembea na kuliacha tatizo hili likakaa kwa muda mrefu, PID inaweza kusababisha madhara yafuatayo;
- Maumivu ya nyonga ama tumbo ya mara kwa mara, hasa wakati wa tendo la ndoa ama kipindi cha upevushaji mayai, kutokana na majeraha yanayokuwa katika mirija ya uzazi.
- Kusababisha majeraha ndani na nje ya mirija ya uzazi ambayo hupelekea mirija kuziba.
- Kubeba mimba nje ya kizazi. Yai lililorutubishwa hushindwa kufika kwenye mji wa uzazi kupitia mirija ya uzazi. Hali hii inaweza kumfanya mwanamke kuvuja damu nyingi sana.
- Ugumba kwa mwanamke: PID inapokuwa sugu humfanya mwanamke kushindwa kushika ujauzito.
Je, Wawezaje Kuiondoa PID?
James Herbal Clinic tuna dawa nzuri zenye mchanganyiko wa mimea ya asili, nazo ni antibiotic zenye uwezo wa kuua vimelea hao na kuondoa PID. Dawa hizo ni VITAMAKA, REDEEMER, na RESH HERB.
Je, unahitaji huduma? Kwa mawasiliano tupigie: 0752389252 au 0712181626